Elections 2015 Matukio na Matokeo toka maeneo mbalimbali ya Tanzania - Uchaguzi Mkuu 2015

Elections 2015 Matukio na Matokeo toka maeneo mbalimbali ya Tanzania - Uchaguzi Mkuu 2015

Nikiwa live katika redio chuchufm, wananchi wakilalamika kwa matendo ya sheha baada ya kumaliza kupiga kura kuwepo nje ya kituo, wakati huo huo kazi yake kuonesha vidole kwa jeshi la Polisi kuwakamata vijana na kuchukuliwa, hali hio mawakala hawakuridhika kwa sababu sheha sio kazi yake kutoa maelekezo yoyote katika Kituo wala haruhusiki kuwepo kwa mita 200.

Jengine tayari washaataarishwa vikosi kuja kupiga kura, hayo yameelewa na mtendaji mmoja wa chama ambae aliwapelekea chakula mawakala wake.
Ccm na sheha na police hio ndio mikakati yao kuvuruga uchaguzi
Eneo mtopepo. Kidatu
 
Nimeangalia ITV huko jimno la ubungo kuna watu wengi wameshindwa kupiga kura kwa sababu majina yao hayako kwenye daftari la kudumu la wapiga kura! Wenyewe wanasema wana vitambulisho, majina yao yanaonekana kwenye ubao yaliyobandikwa siku saba zilizopita, lakini hawako kwenye daftari. Changamoto hii haikuelezwa na Tume; na natumaini wataifanyia kazi ili wapiga kura wapate haki yao ya kuchagua wanaowataka
 
Nyie pigeni kura tu msihofu hakuna haki itakayo chukuliwa tumemuomba Mungu yuko kazini ku deal nao.
 
Hata haueleweki mkuu hebu shusha pumzi kwanza afu uje utupe hii habari vizuri maana sijui umepanik
 
Zoezi hili la uchaguzi linafanana kwa kiasi kikubwa na Zoezi la mitihani ya taifa. NECTA hawana huu upuuzi wa NEC. Eti usikie karatasi za maswali zimepelea Makongo Sec.. .. Hii ni dharau na kubwa
 
Kukataa kusaini matokeo ya kituoni ni kosa. Sheria ya uchaguzi (Cap. 343, RE 2010) inasema hivi:

Section 79A(2):{Where the candidate or his agent refuses to sign the prescribed form under this section the presiding officer or polling assistant shall require such candidate or agent to give reasons in writing for refusal}

nImeiweka hii makusidi kwani nimesikia kuna mawakala Sinza wamekataa kwa kuwa wameshindwa.
 
Kukataa kwa mawakala kuna vigezo.... Hapo lzma waskilizwe
 
Ukweli ni kuwa ccm na serikali yao wamejidhalilisha kwa hili. Mwanzoni tume ilisema form hizo zitakuwepo vituoni, so hakukuwa na sababu ya kusafirishwa kwenda ulipojiandikisha. Lakini cha ajabu tume wakaja na kauli kuwa hutaweza kupiga kura kwenye kituo ambacho hujajiandikisha. Huu ni undumilakuwili. Cha kushangaza nimemsikiliza kwenye media mgombea uraisi wa TLP aliejiandikishia dar ameruhusiwa kupiga kura kilimanjaro baada ya kuikomalia tume. So haki ya kupiga kula hadi kutunishiana misuli?
 
Sehemu nyingi Tanzania pamoja na zanzibar baadhi ya vituo kukosa paper za kupigia kura, tume zote mbili waliwapatia ccm papers hizo wakapige kura wenyewe na kuwapatia visanduku vya kura, wakati huo huo wakiomba radhi kwa vituo vilivyo kosa papers za kupigia kura.

Baada ya ukawa kuingia madarakani tuwafungulie case hawa wakuu wa tume, nchi imekuwa tafrani. Eti tume huru.
 
Washasema mkuu walipata mashambulizi ya kimtandao ila nilihisi hilo litatokea
 
Poleni sana JF.inatia huruma kuwa mtanzania mwenzako anaweza kukuhujumu usifanikiwe.
 
jamani anzeni kuweka update za ubunge na diwani nani kashinda na rais pia nan kaongoza kijimbo sio kwa kivituo
 
Back
Top Bottom