Matukio ya aibu yaliyotukuta kwenye maisha yetu

Matukio ya aibu yaliyotukuta kwenye maisha yetu

feyzal

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2016
Posts
7,683
Reaction score
15,128
Habari ya mchana wadau bila shaka wazima.

Mara nyingi hapa tumekuwa tukizungumzia mapenzi,utajiri nk. sasa hebu tutupie visa vya aibu ambavyo uliwahi kukutana navyo ukikumbuka unaishia kucheka au kuhuzunika.

Naanza na hivi viwili vyangu japo kuna vingi (samahani mimi sio mwandishi mzuri).

1. Mwaka 2010 wakati nipo kidato cha pili kipindi cha likizo nilikuwa na rafiki yangu anaitwa John, yeye alikuwa anasoma Mbagala Kuu na mimi nasoma Azania. Basi tulikubaliana hiyo likizo tuwe tunaenda shuleni kwao Mbagala Kuu asubuhi kwa ajili ya kusoma. Sasa siku ya tukio tulipofika Kijichi nikaanza kubanwa na tumbo lile la uharo aisee hali ikawa inazidi kuwa mbaya kadri muda unaenda, ndipo nikakumbuka kuwa pale Kijichi kuna wakwe zetu wanaishi (kaka yangu mkubwa wazazi wa mke wake wanaishi hapo).

Nikamwambia John twende fasta nisije haribu mambo kifika pale baada ya salamu haraka sana nikaomba nipewe maji niende chooni tumbo linauma. Ile nyumba choo chao kipo uwani na hakuna fensi,halafu mlango ulikuwa wa bati (yaani unaweka na kutoa) na mbaya zaidi tundu la chooni linaangaliana na mlango.Basi nimesaula ile kushusha suruali na boksa nikaanza kutoa vitu vyangu.

Pale uwani walikuwa wamekaa shemeji zangu wa kike 4 na wa kiume mmoja anakunywa chai, pia kulikuwa na wadada walikuwa wanasuka. In short kulikuwa na watu zaidi ya 10.bBasi bhana wakati natoa uharo huku nikiwa nimeupa mgongo mlango hamadi upepo ukaangusha ule mlango nje. Aisee wale wanawake walitimua mbio sio za kitoto pale alibaki shemeji yangu tu yule wa kiume na mimi pale pale uharo ulikata, nikainuka nikaokota mlango nikatawadha nilipotoka nje nikamuaga shemeji yeye mbavu hana huku ananipa pole nikasepa sikutaka kumuaga hata mama mkwe na sikwenda tena pale mpaka 2016 na nilipoenda shemeji zangu walinitania.

2. 2012 nilienda kwa Mama mdogo ilikuwa tarehe 26 mwezi 5 basi yeye alikuwa amepanga nyumba ambayo ina wapangaji wengi tu. Mimi nilienda kusalimia mara moja ila kutokana na kuwa sikuenda siku nyingi kwake yapata mwaka na ushehe alikataa nisiondoke nilale pale pale na kwa bahati alikuwa na kijana wake wa kiume ambaye tulilingana umri yuko pale alimpangia kimoja nyumba ile ile na huku yeye akiwa na chumba na sebule. Nilipoona mama mdogo amenimisi na roho safi nikaamua nikae kwa siku 5.

Sasa mule ndani kulikuwa na manzi anaitwa Rose. Alikuwa demu fulani wa kawaida tu ila amenivuka miaka 2 halafu anaishi na uncle wake, shangazi yake na mtoto wa uncle wake anaitwa Joyce. Walikua wanalala sebuleni, ndani ya siku mbili tu tukawa tumeshazoeana naweza sema kila mmoja alimvutia mwenzie lakini hakuna aliyekuwa tayari kusema.

Nifupishe stori usiku wa 29 May 2012 siku ya jumamosi ndio ilikuwa siku ya kukumbukwa sitaisahau tuliangalia fainali ya Chelsea vs Bayern Munich tukiwa mimi, uncle wa yule binti na shangazi yake, binti mwenyewe akiwa na Joyce tunaangalia mpira maana home pale mama mdogo alikuwa yupo na wifi yake alikuja kumtembelea na alilala pale so ikabidi niende kucheki hapo.

Yule ndugu yangu wa kiume hiyo siku hakuwepo alienda kwa bibi yake upande wa baba yake tangu jana yake.

Basi bhana baada ya mechi kuisha nikaingia ndani kulala nikiwa peke yangu. Mara yule manzi akinitext tukaanza chat, akaniuliza unalala saa ngapi nikamwambia sina usingizi na yeye akajibu nami sina basi nikamwambia njoo tupige stori room basi, akasema sawa nakuja ila sikai sana nikamjibu haina tabu.

Manzi akaja mpaka room ila jinsi alivyokuja ni kihasara hasara aah taa ikazimwa nikala mambo. Huku nyuma shangazi yake akaenda sebuleni kuchukua maji usiku wa saa 7 na dakika zake (sebule na chumba vilikua havijaungana) basi kufika akakuta mlango uko wazi akaingia ndani akamkuta yuko Joyce peke yake akamuuliza mwenzie yuko wapi akasema hajui, akaenda mpaka chooni hola basi alichofanya akaufunga ule mlango na funguo kisha akamuamsha mumewe wakaweka mtego.

Huku nyuma baada ya raundi mbili demu akaona arudi room kufika mlango umefungwa sasa kosa alilolifanya ni kitendo cha yeye kurudi tena ghetto kuja kuniambia salale kumbe uncle wake alikuwa anamchora tu alipoingia ndani tu wakaja kugonga. Ile siku ilikuwa bonge la aibu shangazi na yule mjomba walikuwa mbogo hatari wakawaamsha nyumba nzima na mama mdogo akiwemo na uncle niliona aibu na mama mdogo alistaajabu maana nilikuwa mkimya sana.

Kwa aibu niliyoipata ile siku sikusubiri pakuche muda huo huo nilisepa kwa aibu japo usiku mkubwa, uncle alikuwa peace sana(alinisihi niondoke asubuhi ila nikakataa maana mother mdogo alikuwa mbogo kinoma alidai nimemfedhehesha sana kwa wapangaji wenzie).

Nawe tupia hapa aibu yako uliyokutana nayo.
 
huyo maza mdogo anamind nini kwani ye hajawahi kuliwa
 
Habari ya mchana wadau bila shaka wazima.

Mara nyingi hapa tumekuwa tukizungumzia mapenzi,utajiri nk,,sasa hebu tutupie visa vya aibu ambavyo uliwahi kukutana navyo ukikumbuka unaishia kucheka au kuhuzunika.

Naanza na hivi viwili vyangu japo kuna vingi(samahani mimi sio mwandishi mzuri)

1.Mwaka 2010 wakati nipo kidato cha pili kipindi cha likizo nilikua na rafiki yangu anaitwa John yeye alikua Anasoma mbagala kuu na mimi nasoma Azania.Basi tulikubaliana hiyo likizo tuwe tunaenda shuleni kwao Mbagala kuu asubuhi kwa ajili ya kusoma,sasa siku ya tukio tulipofika kijichi nikaanza kubanwa na tumbo lile la uharo aisee hali ikawa inazidi kuwa mbaya kadri muda unaenda,ndipo nikakumbuka kuwa pale kijichi kuna wakwe zetu wanaishi(kaka yangu mkubwa wazazi wa mke wake wanaishi hapo).

Nikamwambia john tuende fasta nisije haribu mambo kifika pale baada ya salamu haraka sana nikaomba nipewe maji niende chooni tumbo linauma..Ile nyumba choo chao kipo uwani na hakuna fensi,halafu mlango ulikuwa wa bati(yaani unaweka na kutoa) na mbaya zaidi tundu la chooni linaangaliana na mlango.Basi nimesaula ile kushusha suruali na boksa nikaanza kutoa vitu vyangu.

Pale uwani walikua wamekaa shemeji zangu wa kike 4 na wakiume mmoja anakunywa chai pia kulikua na wadada walikua wanasuka inshort kulikua na watu zaidi ya 10.Basi bhana wakati natoa uharo huku nikiwa nimeupa mgongo mlango hamadi upepo ukaangusha ule mlango nje...aise wale wanawake walitimua mbio sio za kitoto pale alibaki shemeji yangu tu yule wa kiume na mimi pale pale uharo ulikata ,nikainuka nikaokota mlango nikatawadha nilipotoka nje nikamuaga shemeji yeye mbavu hana huku ananipa pole nikasepa sikutaka kumuaga hata mama mkwe na sikwenda tena pale mpaka 2016 na nilipoenda shemeji zangu walinitania.

2.2012 nilienda kwa Mama mdogo ilikua tarehe 26 mwezi 5 basi,yeye alikua amepanga nyumba ambayo ina wapangaji wengi tu,mimi nilienda kusalimia mara moja ila kutokana na kuwa sikuenda siku nyingi kwake yapata mwaka na ushehe alikataa nisiondoke nilale pale pale na kwa bahati alikua na kijana wake wa kiume ambaye tulilingana umri yuko pale alimpangia kimoja nyumba ile ile na huku yeye akiwa na chumba na sebule.Nilipoona mama mdogo amenimisi na roho safi nikaamua nikae kwa siku 5.

Sasa mule ndani kulikua na Manzi anaitwa Rose alikua demu fulani wakawaida tu ila amenivuka miaka 2 halafu anaishi na uncle wake,Shangazi yake na mtoto wa uncle wake anaitwa Joyce walikua wanalala sebuleni,ndani ya siku mbili tu tukawa tumeshazoeana naweza sema kila mmoja alimvutia mwenzie lakini hakuna aliyekua tayari kusema.Nifupishe stori usikuwa 29 May 2012 siku ya j'mosi ndio ilikua siku ya kukumbukwa sitaisahu tuliangalia fainali ya Chelsea vs Bayern Munich tukiwa mimi,uncle wa yule bint na shangazi yake,binti mwenyewe akiwa na Joyce tunaangalia mpira maana home pale Mama mdogo alikuwa yupo na wifi yake alikuja kimtembelea na alila pale so ikabidi niende kucheki hapo,,yule ndugu yangu wa kiume hiyo siku hakuwepo alienda kwa bibi yake upande wa baba yake tangu jana yake.

Basi bhana baada ya mechi kuisha nikaingia ndani kulala nikiwa peke yangu..mara Yule Manzi akinitext tukaanza chat,akaniuliza unalala saa ngapi nikamwambia sina usingizi na yeye akajibu nami sina basi nikamwambia njoo tupige stori room basi,akasema sawa nakuja ila sikai sana nikamjibu haina tabu.Manzi akaja mpaka room ila jinsi alivyokuja ni kihasara hasara aah taa ikazimwa nikala mambo..huku nyuma shangazi yake akaenda sebuleni kuchukua maji usiku wa saa 7 na dk zake (sebule na chumba vilikua havijaungana) basi kufika akakuta mlango uko wazi akaingia ndani akamkuta yuko Joyce peke yake akamuuliza mwenzie yuko wapi akasema hajui,akaenda mpaka chooni hola basi alichofanya akaufunga ule mlango na funguo kisha akamuamsha mumewe wakaweka mtego.

Huku nyuma baada ya raundi mbili demu akaona arudi room kifika mlango umefungwa sasa kosa alilolifanya ni kitendo cha yeye kurudi tena gheto kuja kuniambia salale kumbe uncle wake alikua anamchora tu alipoingia ndani tu wakaja kugonga ile siku ilikua bonge la aibu Shangazi na yule mjomba walikua mbogo hatari wakawaamsha nyumba nzima na mama mdogo akiwemo na uncle niliona aibu na mama mdogo alistaajabu maana nilikua mkimya sana,kwa aibu niliyoipata ile siku sikusubiri pakuche mda huo huo nilisepa kwa aibu japo usiku mkubwa, uncle alikua peace sana(alinisihi niondoke asubuhi ila nikakataa maan mother mdogo alikua mbogo kinoma alidai nimemfedhehesha sana kwa wapangaji wenzie.

Nawe tupia hapa aibu yako uliyokutana nayo.
Du baharia safi sana
 
Luna nilienda kwa jamaa zangu tukawa tumekaa seating room story zimekolea htari jamaa zangu wakawa wanacheka sna nikawa najiuliza kulikoni duu! Kumbe nimevaa soksi rangi tofauti ikanilazimu nivue nitie mfukoni
 
Back
Top Bottom