realMamy
JF-Expert Member
- Apr 28, 2024
- 3,925
- 8,853
Imeripotiwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuhusu Mtoto aliyechinjwa na Dada wa kazi. Watu wanaishia kulalamika tu bila kutoa suluhisho ya kitu gani kifanyike kupunguza huu ukatili Mkubwa kwa watoto wasio na hatia.
Tumeshuhudia hivi karibuni kukamatwa haraka kwa kijana aliyechana picha ya Rais.
Kwa nini zisichukuliwe hatua za haraka kukinusuru kizazi kijacho.
Waziri Mwenye dhamana tunaomba hatua za haraka zichukuliwe ili wananchi waishi maisha ya furaha.
Nchi itapata vipi maendeleo kama wazazi wanafanya kazi kwa hofu wakiwaza usalama wa watoto nyumbani.
Ni kitu gani kinashindikana kuanzishwa au kuongeza taaluma ya mafunzo kwa dada wa kazi za nyumbani kwenye Vyuo vya Veta au kuwe na chuo maalumu cha mafunzo kwa ajili yao.
Hii itasaidia thamani yao kupanda lakini pia watafanya kazi kwa mikataba hata serikali itakuwa na takwimu za wadada wote na mahali walipo.
Hili suala haliumi hadi likufike wewe au mtu wa karibu yako.
Tunaomba serikali ichukue hatua za haraka kwa matukio haya ya kutisha kwa watoto wetu.
Mfumo mzuri wa upatikanaji wa Dada wa kazi nyumbani utasaidia kwa kiasi kikubwa sana kuliko sasa hivi wananchi wanaishi kwa hofu.
Dada wengi waliosomea mambo ya Hotel wako nyumbani kutokana na kukosa ajira, lakini kama wataongezewa taaluma ya kazi za nyumbani na mshahara ukawa mzuri kutokana na mikataba mizuri itasaidia Jamani.
Serikali mko wapi? Tunaomba mtusaidie.
Mwandishi wa Habari.