Unamlipa elfu 30 ya masimango na manyanyaso kama mtumwa wako utegemee yeye akutendee wema.
Ni kweli serikali inapswa kuweka mkono wake hapo ila wananchi nasi tu wazinguaji sana.
Dada wa kazi umemtoa mpitumbwi huko wala hamjuani umeunganishwa tu na mtu usiyemjua ambae namba uneipata kwa rafiki wa rafiki yako.
Huyo dada ndo aje akuangalizie mtoto wako mdogo wa miaka miwili na mali zako wakati mwingine, huyo dada utamlipa 30-60k. Afanye kazi zote za hapo nyumbani.
Huku bosi ukijitetea kwa utetezi dhaifu ati anakula bure na kulala bure.
Wakati mwingine unatweza utu wa huyo dada kwa kumtamkia maneno makali mbele haya wageni, muonekano wake na mavazi yake kuukuu yanamtambulisha moja kwa moja kua huyo ni dada wa kazi.
Mkiwajali nao pia watawajali.