Yule Big mpumbavu sana alistahili alichokipata na kikundi chake,nadhani watakuwa walitumwa na lopolopo wao,
Haiwezekani uende umevaa jezi za timu yako ambayo haichezi siku husika,badala ya kufika kuangalia mpira wewe na wenzio mnaanza kuimba nyimbo na kuleta hamasa utafikiri timu yako ndio ipo uwanjani.
Ukiwaangalia wana mamifuko na chupa za maji sasa jiulize wameingia nazo vip uwanjani kinyume cha sheria na taratibu za viwanja vya mpira.
Yani Big na ubig wake alitulizwa na mdada mmoja mdogo sana kiumbo Jesca maana timbwili lake aliloletewa big kaondoka anachechemea.
Hatukatai ushabiki na utani wa simba na yanga ila lazima kuwe na mipaka na tuangalie mazingira la sivyo utahatarisha uhai wako kisa ushabiki.