LENGISHO
Senior Member
- Sep 15, 2017
- 169
- 265
TUKIO laKushambuliwa kwa kujaribu kuuawa kwa Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa wanasheria Tanganyika na Mwanasheria Mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo ( CHADEMA), yanarudisha kumbukumbu za matukio makubwa ya ugaidi na mengine yenye viashiria vyake, ambayo yamewahi kutokea nchini.
MASHAMBULIZI YA KIGAIDI NA KIHALIFU
Agosti 7, 1998: Jengo la ofisi za Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, lilishambuliwa na kusababisha vifo vya watu 11. Tukio hilo linahesabiwa kuwa uhalifu mkubwa wa kigaidi kuwahi kufanyika nchini.
Tukio la kushambuliwa kwa Ubalozi wa Marekani nchini, lilikwenda sambamba na mashambulizi dhidi ya ubalozi wa nchi hiyo nchini Kenya, ambako watu 222 walipoteza maisha.
Kundi la kigaidi la Al Qaeda ndilo lililotuhumiwa kuhusika na mashambulizi hayo.
Novemba 2011: Serikali ya Tanzania ilitoa tahadhari kuhusu uwezekano wa mashambulizi ya kigaidi, baada ya Watanzania 10 kukamatwa wakati wakivuka mpaka wa Kenya na Somalia kwenda kujiunga na kundi la kigaidi la Al Shabaab. Kundi hilo linaendesha vitendo vya kigaidi nchini Marekani.
Juni 2012: Raia wa Ujerumani alikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam, akituhumiwa kuwa mfuasi wa Al-Shabaab.
Oktoba 2012: Askari wa Jeshi la Polisi alishambuliwa na kuuawa na watu wasiojulikana kwa panga huko Zanzibar.
Oktoba 2012: Makanisa sita yalichomwa moto jijini Dar es Salaam kwa siku moja eneo la Mbagala wilayani Temeke.
Novemba 2012: Imam mmoja mwenye msimamo wa wastani visiwani Zanzibar, alimwagiwa tindikali na watu wasiojulikana.
Desemba 2012: Padri Ambrose Mkenda wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Mpendae Zanzibar alipigwa risasi wakati anafungua geti ili kuingia nyumbani kwake katika eneo la Kitomondo.
Februari 2013: Mchungaji wa Kanisa la Pentecoste Assemblies of God Tanzania (PAGT) katika eneo la Buseresere, wilaya ya Chato, Mathayo Kachila (45) aliuawa katika mzozo wa nani mwenye haki ya kuchinja kati ya wafuasi wa dini za Kiislamu na Kikristo.
Februari 2013: Padri wa Kanisa Katoliki Minara Miwili Zanzibar, Evarist Mushi, aliuawa kwa kupigwa risasi.
Mei 2013: Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, jijini Arusha, lilishambuliwa kwa bomu na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine 63 kujeruhiwa.
Februari 2015: Polisi walilazimika kuomba msaada wa askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kukabiliana na watu waliokuwa wamejificha kwenye mapango ya Amboni mkoani Tanga. Askari hao wa polisi na JWTZ walipiga kambi hadi walipokisambaratisha kikundi hicho kilichoelezwa kuwa na sura ya ugaidi.
Mapambano hayo yaliyodumu kwa siku kadhaa, yaliisha bila askari hao kukamata wahusika ambao walikuwa wakidaiwa walikuwa wanakaa kwenye maeneo hayo wakijfunza vitendo vya ugaidi.
WATANZANIA KUHUSISHWA NA UGAIDI
Aprili 2015: Mwanafunzi wa kidato cha tano katika Shule ya Sekondari ya Bihawana, Dodoma, Rashid Charles Mberesero, alikamatwa kwa kuhusika na mauaji ya kigaidi kwenye Chuo Kikuu cha Garissa, Kenya.
Katika tukio hilo, Mberesero na wenzake wanadaiwa kuhusika kwenye shambulio la kigaidi lililoua watu 148.
Aprili 2015: Wasichana watatu, akiwamo Mtanzania, walikamatwa mpakani mwa Kenya na Somalia wakati wakienda kujiunga na kundi la Al –Shabab, kuwatumikia kingono.
Mtanzania huyo anayedaiwa kuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika, nchini Sudan, anaitwa Ummul-Khayr Sadir Abdul (19), mwenyeji wa Zanzibar. Alikamatwa pamoja na raia wawili wa Kenya, Maryam Said Aboud na Khadija Abubakar Abdulkadir.
Aprili 14, 2015
Watu 10 walikamatwa na polisi mkoani Morogoro msikitini huku wakiwa na milipuko 30, sare za jeshi na bendera nyeusi inayodaiwa kutumiwa na kundi la wapiganaji wa Al Shabaab.
Katika tukio hilo, mtu mmoja anayesadikiwa kuhusiana na watu hao waliokamatwa, aliuawa na wananchi wenye hasira baada ya kumjeruhi kwa panga askari polisi aliyekuwa akipambana naye katika kitongoji cha Nyandero, Kidatu wilayani Kilombero.
Novemba 2010
Mtanzania Ahmed Khalfan Ghailani, alihukumiwa kifungo cha maisha baada ya mahakama ya kiraia nchini Marekani kumpata na hatia ya kuhusika na mashambulizi ya kigaidi kwenye balozi za Marekani za nchini Tanzania na Kenya mwaka 1998.
POLISI KUNYANGANYWA SILAHA
Machi 24, 2016: Watu saba wanaosadikiwa kuwa majambazi majira ya saa nane usiku wa kuamkia Machi 25, mwaka huu, walivamia ofisi za kampuni ya simu za mikononi ya Halotel katika eneo la Medelii, Manispaa ya Dodoma wakiwa na mapanga na nondo, kisha kutoboa ukuta na kuwajeruhi askari polisi kwa mapanga na kupora bunduki aina ya SMG.
Mei 29, 2015: Majambazi yalivamia lindo la askari wa kikosi cha Tazara na kupora bunduki moja aina ya SMG.
Julai 12, 2015: Watu waliokuwa na silaha za moto, walivamia kituo cha polisi Stakishari, jijini Dar es Salaam, na kuua watu saba wakiwamo polisi. Aidha watu hao waliiba silaha 21, zikiwamo bunduki za aina ya SMG 15 na SAR sita na risasi.
Machi 30, 2015: Katika eneo la Kongowe jijini Dar es Salaam, majambazi yalivamia askari wawili kwenye kizuizi cha barabarani na kuwapora bunduki mbili aina ya SMG, zenye risasi 60.
Februari 3, mwaka 2015: Kilombero mkoani Morogoro, majambazi yalivamia na kuvunja ghala ya silaha kwenye kituo cha polisi Mgeta na kuiba silaha aina ya SMG na risasi 30.
Februari 3, 2015: Katika kituo cha polisi cha Geita, majambazi yalipora SMG 10 na pia yalivamia kituo cha polisi Ikwiriri, Rufiji mkoani Pwani na kupora bunduki tano na risasi 60.
Juni 12, 2014: Kimanzichana mkoani Pwani, majambazi sita yakiwa na pikipiki tatu, yalikivamia kituo cha polisi Mkamba, wilayani Mkuranga na kuua askari mmoja, mgambo wawili na kupora bunduki tano na risasi 60.
Septemba 7, 2010: Majambazi yalivamia kituo cha Polisi Bukombe mkoani Shinyanga na kupora SMG 10.
2016: Mauaji ya Kibiti mkoani Pwani na rufiji , zaidi ya watu 40 waliuawa wakiwemo maafsa wa polisi, viongozi wa serikal za mitaa na wananchi wa kawaida, Jeshi la polisi lilipambana na kufanikiwa kukisambaratisha kikundi hicho .