666 chata
JF-Expert Member
- Mar 14, 2013
- 1,700
- 3,921
Nchi kubwa hii na ina mambo mengi, hapa tutagusia machache ya kusisimua sana yalio acha maswala mpaka leo, mengine mtaongezea, lengo tukumbushane tulipotoka;
TUKIO LA UFO SARO
Hii ilikua 2013, nchi ilistushwa na taarifa ya kupigwa risasi kwa mwandishi wa habari maarufu sana wakati huo, katika taarifa yao jeshi la Polisi kwa kupitia kamanda Wambura, walisema siku ya tukio Ufo Saro na mume wake aitwae Mushi walienda kumtembelea mama yake mzazi na ufo saro, kufika huko ugomvi ukaanza na bwana Mushi akamlalamikia mama mkwe wake kwamba amekua akimtetea sana mwanae na hapo hapo akatoa pistol yake akampiga mama mkwe wake risasi za kichwa, akampiga risasi za tumbo na mguu mkewe ufo, na yeye akajipiga ya kidevu akafa. Ufo bado yuko hai mpaka sasa, ni Mungu tu.
SCORPION MTOBOA MACHO
Mwaka 2016 pale buguruni kulitokea tukio la kutisha sana, yawezekana kwa miaka hii mingi matulio ya kutisha yalikua yametokea mengi ila hili lilikua na upekee sana, kijana mmoja aitwae Said Ally alitobolewa macho mbele ya wananchi waliokua wanatizama na hakuna aliemsaidia lolote, Said hakua mwizi wala muhalifu, anasema alishuka zake hapo Buguruni kujinunulia kuku tu ale afurahi, ghafla akatokea mtu mmoja alieanza kumgasi, ghafla akaanza kumpiga na kisha akaanza kumchoma visu, hadharani mbele za watu, aliekua akifanya jambo ilo hadharani hakuishia hapo bali alichukua kisu kisha akaanza kumtoboa macho kijana Said, wananchi wakiwa wanatizama na hakuna aliefanya lolote na huu ndio upekee wa tukio ilo, na hapa maswali mengi sana ya kazuka, je inawezekanaje wanadamu wengi wakawa wamekaa wanamtizama tu mwanadamu mmoja akimfanyia ukatili mwanadamu mwenzake wao wakiwa wamekaa tu? cha ajabu zaidi aliekua anafanya ukatili huo Bwana Salum Njwete 'Scorpion' alikua ni mtu maarufu kiasi kwani miaka michache nyuma yake aliwai kushinda milion 20 ktk shindano moja maarufu la dume challenge.
UCHAGUZI WA AJABU WA MWAKA 2020
Uchaguzi huu kwanza ulitawaliwa na kampeni ambazo hazijapata kutokea ktk nchi hii, aliekua mgombea urais kwa tiket ya CCM akiwa mikoa ya mbeya na musoma alitamka hadharani mchana kweupe kwamba wananchi wa maeneo hayo kama wakiwachagua wagombea wa upinzani yeye hatoleta maji au maendeleo kwenye majimbo hayo, mgombea huyu sio kwamba yeye alikua amekwisha shinda, hapana ila na yeye alikua anawategemea hao hao wananchi waweze kumchagua ndo aweze kuleta hayo maendeleo au vp😂😂, ilifikia hatua watu 400 wa chama kimoja walitangaza nia ya kugombea ubunge kwenye jimbo moja, vilikua ni vi hoja vya karne, ni kama kulikua kuna uhakika mtu wa ccm ni lazima ashinde. na baada ya uchaguzi wenyewe Mwenyekiti wa Chadema, Mheshimiwa Mbowe alisikila akihoji kwamba inawezekanaje nchi nzima yaani wapinzani wasipate hata diwani mmoja tu?😂😂 lakini Mweshimiwa mkuu wa nchi hapo kabla alikwisha toa tangazo tena akiwa mkoani Singida akisema wazi kwamba "yaani ukurugenzi nikuteue mimi alaf umtangaze wa upinzani kua ameshinda hiiii".
KUPIGWA RISASI kwa LISSU
Hii ilikua 2017, story kila mtu anaijua, ila tu wakati anapigwa Risasi alikua ni mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, na mwanasheria mkuu wa chama cha Chadema, story yake inasisimua kwamba iliwezekanaje mtu huyu akipigwa risasi ndani ya makazi ya viongozi wa nchi yanayolindwa sana 24/7, lakini pia yeye ndio alikua mwanasiasa wa kwanza nchini kwetu kupigwa risasi saa saba mchana wakati wa jua kali😂. Chuma bado kipo, Mungu anampenda sana Antipas.
WATU WAZITO WATAJWA KUJIHUSISHA na MADAWA YA KULEVYA
Aliekua mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam wakati huo, mwaka 2017, aliwataja kwa majina watu zaidi ya 65 akisema kwamba wamekua wakijihusisha na uuzwaji wa madawa ya kulevya ndani ya nchi yetu, akiwataja watu hao maarufu na viongozi wakubwa, bila kupepesa macho alisema watu hao wanao uza dawa za kulevya ni pamoja na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, Askofu Josephat Gwajima, mfanyabiashara Yousuf Manji, mbunge wa zamani Idd Azan, mmiliki wa efm bw. Francis Majizo. Habari hii ilikua haijapata kutokea tangia nchi ipate uhuru, hawa watu aliowataja hasa Mheshimiwa Mbowe kwa wakati alikua ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni akilindwa na kupewa stahiki zote na serikali, Mbowe mwenyewe alishangaa sana na kuhoji nchi inapoelekea.
KIFO CHA RAIS wa TANZANIA MADARAKANI, na UJIO WA RAIS MPYA MWANAMKE
March 17, 2021. R.I.P John Pombe Maghufuli, rais mzalendo na mchapakazi wa aina yake. Mungu amrehemu.
Hili la Rais mwanamke halikua limewai hata kutazamiwa, yawezekana ingewezekana labda mwaka 2050 huko kwenda mbele, Mungu muamuzi wa haki kila jambo upanga yeye.
matukio yapo mengi, mengine mtaweka tukumbushane tulipotoka, tujifunze, twende mbele na tumshukuru Mungu kwa yote.