JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mwanasaikolojia wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Mkoani Dar es Salaam, Zainabu Rashid amezungumzia kuhusu migogoro ya wapendanao wakiwemo wanandoa na wapenzi.
Zainabu anasema: "Sababu inaweza kuwa ni mrundikano wa migogoro. Mtu anapolimbikiza matatizo, yale matatizo ni kama kidonda, kile kidonda usipokitibu kwa wakati kinaendelea kukua na kinapokua, mwisho wa siku kinaweza kukuletea madhara.
"Inapotokea mume amemkosea mke wake au mke amemkosea mume wake kwa muda mrefu na amekaa bila kusuluhisha jambo hilo, inatengeneza kama kidonda kinakua.
"Kitakapolipuka, akili ya binadamu ina namna fulani ya kufanya kazi kulingana na vile ulivyotunza taarifa. Hivyo, mtu anaweza kufanya jambo bila kujua, lakini ni matokeo ya uzoefu alioupata baada ya kufanya jambo fulani.
"Kuna kitu kinaitwa haiba, mwingine anaweza kusamehe, mwingine ni rahisi kusahau, mwingine anatunza. Mwisho wa siku anakuja kufanya tukio kubwa kwa sababu ametunza matukio mbalimbali.
"Kitu kingine ni malezi, hasa ya kihisia. Familia nyingi hazilei watoto katika ukuaji wa kihisia katika kuhimili hisia zao, kwa sababu siyo kila haki yake atapewa. Kwa hiyo, wanandoa au wapenzi wanaingia kwenye mauaji kwa sababu wameshindwa kuhimili hisia zao za hasira au wivu."
Shekhe azungumza
Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, hayuko mbali katika kukimulika kilicho nyuma ya pazia kuhusu mauaji miongoni mwa wapendanao.
Kiongozi huyo wa kiroho anasema: "Ni wimbi tu la shetani linapita, kwa sababu mambo kama haya huwa yanatokea kwa kipindi fulani kisha yanapotea. Lakini kama ni elimu, viongozi tunatoa juu ya uharamu wa kujiua na kuua mtu mwingine."
Akiwa mkoani Iringa juzi, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, alilaani vitendo vya mauaji vinavyofanywa na baadhi ya watu kwenye jamii, yakiwamo yanayohusisha wapendanao.
Alisema jeshi hilo litaendelea kuwachukulia hatua za kisheria watu watakaobainika ikiwamo kuwafikisha mahakamani, akisisitiza kuwa kumekuwa na matukio ya mauaji aliyoyaita ya ovyo ambayo yanasababishwa na ukosefu wa maadili na hata imani za kishirikina.
"Tufike mahali tuseme basi, tujue kuwa Mungu yupo na kwamba kuna siku tutakwenda kuwajibika," IGP Sirro alionya.
Nini kifanyike?
Ili kukabiliana na tatizo hilo, Mwanasaikolojia Zainabu ana angalizo kwa wazazi na walezi kuwa chimbuko la mauaji haya miongoni mwa wapendanao ni makosa yaliyochagizwa na wazazi na walezi kutowajibika katika malezi ya watoto wao.
"Wazazi wazingatie malezi ya ukuaji wa watoto kihisia, watoto wanakua na hisia tangu wanapozaliwa. Kwa hiyo, mpaka wanapokuwa watu wazima, watakuwa wanajua namna ya kuhimili hisia zao," anasisitiza.
Mwanasaikolojia huyo pia ana rai yake kwa jamii, akiitaka kuchukua hatua inapoona mtoto anakwenda kinyume cha maadili mema yaliyowekwa kwenye jamii anayoishi.
Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum, anaelezea mustakabali wa tatizo la mauaji yanayotikisa ya wapendanao nchini, anashauri:
"Inawezekana hata mawaidha yanayotokana na viongozi wa dini siyo watu wote yanawafikia huko maeneo waliko. Kwa hiyo, inatakiwa kuongeza vyombo vya mawasiliano katika vijiji, kwenye miji mbalimbali na watu wawe wanafuatilia vyombo hivi ambavyo vitawaelimisha kwa namna moja au nyingine.
"Pia watu wafuate misingi yao ya dini na miongozo yao ya kiimani ili kujiepusha na majaribu ya shetani."
Ni muhimu wanandoa wawe wepesi kujifunza, kujikosoa, kujisahihisha na kuombana msamaha pale mtu anapohisi kumkosea mwenzake. Ni vema ifahamike kuwa, hakuna ndoa yenye afya njema bila zoezi la msamaha.
“Msamaha ni dawa ya furaha ya familia. Msamaha ni muhimu kwa afya yetu ya kihisia na kuendelea kuishi kwa heri. Asiyeomba msamaha na asiyesamehe hana amani katika nafsi yake na hawezi kuwa na ushirika na Mungu. Pia, mtu wa aina hiyo hawezi kuwa na uhusiano mwema na binadamu mwenzake.
Watu wasioomba msamaha na wasiosamehe ni wagonjwa wa kimwili, kihisia na kiroho. Siku zote huteseka na kuishi kwa vinyongo na roho ya visasi na maangamizi. Bila msamaha, familia inakuwa uwanja wa migogoro, ngome ya uovu na maafa.
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kilirekodi matukio ya mauaji ya kikatili 20, yakiwamo ya wapendanao, kwa mwezi Januari mwaka huu.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Anna Henga, matukio hayo yaliripotiwa katika mikoa ya Mtwara, Rukwa, Njombe, Katavi, Mwanza, Dodoma, Ruvuma, Dar es Salaam na Mara.
Chanzo: Nipashe