Matukio ya Mkutano Mkuu wa Mwaka na Uchaguzi wa Yanga. Eng Hersi Rais kwa miaka 4 mingine

Matukio ya Mkutano Mkuu wa Mwaka na Uchaguzi wa Yanga. Eng Hersi Rais kwa miaka 4 mingine

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mabingwa wa NBC mara 5 Mfululuzi Yanga SC leo wanafanya Mkutano wao Mkuu wa Mwaka na Uchaguzi , katika Ukumbi wa Super Dome, Masaki, .

Na mojawapo ya Ajenda kuu ni Uchaguzi wa kuchagua viongozi katika miaka mingine minne.

Nafasi ya Urais ambaye mgombea ni Eng. Hersi Said akiwa yupo pekee yake kwenye nafasi hii

Makamu wa Rais ambaye Mgombea wake ni Arafat Hajji naye yupo pekee yake. Hawa wote wanatete nafasi zao Na hii imetokana na kile walichokifanya kwenye miaka 4 waliopo madarakani na kuifanya Yanga kuwa bora zaidi na mafanikio makubwa zaidi Ikiwemo kubeba kombe la NBC mara 5 mfululizo Ngao za jamii 4 CRDB Bank mara 4 na hata kucheza hatua ya Robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika kwa mara ya kwanza.

Lakini moja ya mafanikio kuifanya Klabu kuwa yenye thamani zaidi katika kufanya usajili mzuri wa wachezaji na hata kuvutia wadhamini wengi zaidi huku kitengo chao cha Habari kikiwa bora zaidi kwa Afrika.

Mbali na hayo pia wamefanikisha mchakato wa mabadiliko wa Yanga kuwa kampuni ambapo itawaruhusu wawekezaji kwa asilimia 49. Ambapo mchakato huu pia upo mwishoni.

Lakini kuanza kwa ujenzi wa uwanja wao mpya pale eneo la Kaunda yalipo makao Makuu ya Klabu. Ambapo walisani mkataba na GSM katika ujenzi wa uwanja huu ambao utakuwa 50 kwa 50.

Lakini leo pia Watachaguliwa wajumbe wa kamati ya utendaji ambapo waliojitokeza kupita katika mchujo huo wapo 16 licha wanaopewa kipaumbele ni wale waliokuwepo miaka 4 iliyopita.

Mbali na mafanikio hayo yote ya Yanga uwezi kusahau mchango mkubwa wa Bilionea GSM ambaye amemwaga pesa nyingi sana na kuwa moja ya Wafadhili wakubwa wa Yanga.

Soma Pia: Yanga na GSM zasaini mkataba wa ujenzi wa uwanja wa Yanga

All Best Yanga.. . YANGA Bingwa . Mwakani Tena

Screenshot_20260802_104543_Instagram.jpg
Screenshot_20260802_103547_Instagram.jpg

Updates
Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila amekabidhiwa Kadi ya uwanachama wa Yanga katika mkutano mkuu uliofanyika leo

Young Africans ikishinda napata furaha zaidi” Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, anasema klabu za Dar es Salaam, zikishinda huwa anafurahi, lakini Yanga ikishinda hufurahi zaidi.

Bajeti ya msimu ujao kwa klabu ya Yanga ni Bilioni 36,013,671,595

Muhtasari wa Ripoti ya Fedha ya Young Africans Sports Club Katika Mkutano Mkuu wa Wanachama Yanga SC, Mkurugenzi wa Fedha, Justina Ernest amewasilisha taarifa ya mapato na matumizi ya msimu wa 2025/2026 Kwa msimu wa 2025/2026, klabu ilikusanya jumla ya TSh 29.36 bilioni.

Matumizi ya klabu yalifikia TSh 29.34 bilioni, ambapo sehemu kubwa ilielekezwa kwenye mishahara na marupurupu ya watumishi, usajili na uhamisho wa wachezaji, maandalizi ya mechi, usafiri, chakula na malazi.

Baada ya matumizi hayo, klabu ilibaki na bakaa ya TSh 17.5 milioni. Kwa msimu wa 2026/2027, klabu imepanga kukusanya TSh 20.70 bilioni, huku ikitarajia kutumia TSh 36.01 bilioni.

“Katika kipindi Hiki cha miaka minne, tumefanikiwa pia kuweka rekodi mbalimbali katika historia ya Ligi Kuu Tanzania, YANGA imecheza mechi 120, tukishinda mechi 101, sare 12 na kufungwa mechi 7 tu, tukiweka rekodi ya kukusanya POINTI 315. YANGA imefunga jumla ya magoli 286 na kufungwa 51 tu, hivyo kufanya tofauti ya magoli ya kufunga na Kufungwa kuwa magoli 235.” Injinia Hersi Ally Said.

Taarifa kwa Wanachama kuhusiana na Baraza la wadhamini Bodi yetu ya wadhamini ilikuwa imeundwa na wajumbe watano kama ifuatavyo: Mwenyekiti: Mheshimiwa George Mkuchika Wajumbe: * Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba * Bi. Fatma Karume * Mheshimiwa Anthony Peter Mavunde * Mheshimiwa Abbas Tarimba

Kwa heshima kubwa, klabu inatambua nafasi ya kwenye taifa letu, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ambaye aliteuliwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kutokana na majukumu hayo makubwa ya wadhifa huo, Waziri Mkuu ameomba kujiondoa katika nafasi yake ya ujumbe wa Kamati ya Uchaguzi ili kupata wasaa wa kutumikia taifa. Kutokana na mabadiliko hayo, Kamati tendaji, imeridhia kujaza nafasi yake na Mheshimiwa Ridhiwani Jakaya Kikwete, ambaye sasa atahudumu kama mjumbe wa Baraza la Wadhamini

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Yanga SC, kwa pamoja wamempitisha Hersi Said, kuwa Rais wa klabu hiyo kwa miaka minne mingine

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Yanga SC, kwa pamoja wamempitisha Arafat Haji, kuwa Makamu wa Rais wa klabu hiyo kwa miaka minne mingine.

Screenshot_20260803_072720_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom