carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Wakati taifa likiendelea kukumbuka na kujadili jeraha kubwa la kisiasa lilioachwa na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, mkazi wa Mkoa wa Mbeya, Ayubu Mwaisumo, ameibua mazito na kuikabili serikali bila kificho kuhusu umwagaji damu uliotokea kipindi hicho.
Akizungumza na SasaLive kutoka Uyole, jijini Mbeya, Oktoba 30, 2026, Mwaisumo amesema kuwa wananchi hawawezi kutakiwa "kuganga yajayo" wakati damu za ndugu zao waliouawa na kupotezwa mikononi mwa vyombo vya dola wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana bado zinalia, na hakuna kiongozi yeyote aliyeajibishwa.
Akielezea ukatili huo wa Uchaguzi Mkuu wa 2025 ulioshuhudiwa kwa macho yake, Mwaisumo ameeleza jinsi raia wasio na hatia walivyolengwa moja kwa moja majumbani na mitaani:
"Sisi hatukusema yatokee... mimi sisimuliwi, sihitaji ripoti sijui ya jaji nani, nimeikuta nimekiona kwa macho yangu. Mtu anapigwa akiwa kwenye fomu kabisa za polisi... mwenzetu Zawadi alipigwa nyumbani kwake ndani ya geti, risasi imepiga mpaka ndani amekufa tu. Walitekeleza hayo majukumu ilikuwa ni vyombo vya dola."
Aidha, ameonya kuwa ni unafiki mkubwa kuwataka wananchi kusonga mbele na kusahau matukio ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 wakati familia nyingi bado zinatafuta miili ya ndugu zao waliopotea au hawajui waliko, huku watawala wakiwa wamenyamaza kimya.
Mkaazi huyo amemalizia kwa kusisitiza kuwa ili taifa liweze kupona vidonda vya Uchaguzi Mkuu wa 2025, lazima viongozi na wakuu wa vyombo vya dola wakubali kuwajibika kwa maafa yaliyotokea, badala ya kuwataka wananchi wajifanye hakuna kilichoharibika.
Soma Pia: Tume ya Jaji Lila: Tutachunguza nguvu iliyotumika kudhibiti ghasia za Oktoba 29