carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Inahuzunisha watu kupigwa risasi majumbani kwaoWakati taifa likiendelea kukumbuka na kujadili jeraha kubwa la kisiasa lilioachwa na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, mkazi wa Mkoa wa Mbeya, Ayubu Mwaisumo, ameibua mazito na kuikabili serikali bila kificho kuhusu umwagaji damu uliotokea kipindi hicho.
Akizungumza na SasaLive kutoka Uyole, jijini Mbeya, Oktoba 30, 2026, Mwaisumo amesema kuwa wananchi hawawezi kutakiwa "kuganga yajayo" wakati damu za ndugu zao waliouawa na kupotezwa mikononi mwa vyombo vya dola wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana bado zinalia, na hakuna kiongozi yeyote aliyeajibishwa.
Akielezea ukatili huo wa Uchaguzi Mkuu wa 2025 ulioshuhudiwa kwa macho yake, Mwaisumo ameeleza jinsi raia wasio na hatia walivyolengwa moja kwa moja majumbani na mitaani:
"Sisi hatukusema yatokee... mimi sisimuliwi, sihitaji ripoti sijui ya jaji nani, nimeikuta nimekiona kwa macho yangu. Mtu anapigwa akiwa kwenye fomu kabisa za polisi... mwenzetu Zawadi alipigwa nyumbani kwake ndani ya geti, risasi imepiga mpaka ndani amekufa tu. Walitekeleza hayo majukumu ilikuwa ni vyombo vya dola."
Aidha, ameonya kuwa ni unafiki mkubwa kuwataka wananchi kusonga mbele na kusahau matukio ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 wakati familia nyingi bado zinatafuta miili ya ndugu zao waliopotea au hawajui waliko, huku watawala wakiwa wamenyamaza kimya.
Mkaazi huyo amemalizia kwa kusisitiza kuwa ili taifa liweze kupona vidonda vya Uchaguzi Mkuu wa 2025, lazima viongozi na wakuu wa vyombo vya dola wakubali kuwajibika kwa maafa yaliyotokea, badala ya kuwataka wananchi wajifanye hakuna kilichoharibika.
Definitely wauaji walipewa amri kuwa ili kuwatisha, eg ingia hata majumbani wapige risasi humo humo...haiwezekani ika coincidence kuwa kote walikouawa watu , walipigwa majumbani. There was instructions to do that ndiyo maana mauaji yalitekelezwa in a uniform manner. There was a protocol that was followed or pit it in more technical language/science there was an SOP ie Standard Operating Procedure!Inahuzunisha watu kupigwa risasi majumbani kwao
Huyu mtu kasema yanayofahamika, lakini hayatakiwi kufahamika.Inahuzunisha watu kupigwa risasi majumbani kwao
Huutendei HAKI ubinaadam wako.Hii siku nilikua zangu kijiweni Kibo, nimewatembelea washikaji.
Sikupiga kura niliona badala ya kupoteza muda wangu bora Nika catch up na wana ambao hatuja onana kitambo baada ya kubadili harakati.
Nikiwa Kibo(Ofisi za Hakuna Kulala) niliona vijana wanaandamana mbele lilikua linaongoza gari la jw.
Ilikua around saa 4 asubuhi.
Vijana hawa walikua wanapita njia ya mwendokasi.
Lilivyo pita hili kundi kuelekea kimara, kundi la pili nalo lilikua linakuja maeneo ya lilipo kanisa la Gwajima. Hili sasa ndio chanzo cha vurugu, pale ndio ilikua kama ground zero.
Polisi walitokea walipo tokea, wakatangaza watu watawanyike maana walidai maandamano siyo halali.
Kilicho nishangaza dakika kumi nyingi risasi zikapigwa. Halafu gari ya polisi ikapita na watu imewakamata.
Wakaenda kuwaweka kwenye kituo cha Kibo pale. Kumbe wale watu wawili walikua wameuawa na mmoja amejeruhiwa.
Wale vijana waliokua wanaandamana wakawa wanaelekea polisi kujua hatima ya wenzao lakini walivyo fika polisi wakakuta wawili Kati ya watatu walio kua wamechukuliwa na polisi wamelazwa nje wakiwa wamefariki na mmoja alikua kawekwa sero.
Yule aliekua kawekwa sero akawa anapiga kelele nipo huku, nipo huku njooni mnisaidie.
Wale vijana walivyofika pale wakakodi bajaji wakapakia miili ya marehemu na wakavunja kituo wakamtoa mwenzao aliekua anajeraha la risasi.
Polisi walikimbia, vijana wakachoma kituo kile, pembeni ya kituo kulikua kuna kituo cha kupigia kura nacho wakakichoma.
Baada ya hapo ikawa VITA, Sikumbuki nilifikaje kwangu Ila nilio yaona baada ya hapo yalikua yanatisha.
People were massacred, pale suka miili ilitapakaa barabarani, maganda ya risasi za kivita ambayo niliokota manne na moja nimetengeneza kama kidani kwajili ya kunikumbusha unyama ambao Watanzania walifanyiwa na vyombo vya ulinzi na usalama.
Inahudhunisha kwa mtu yeyote kupigwa risasi mahali popote wakati kuna njia nyingi za kumdhibiti mtu huyo, hata kama anafanya uharibifu wa maliInahuzunisha watu kupigwa risasi majumbani kwao
Sijui ulitaka niiweke vipi ili ieleweke.Huutendei HAKI ubinaadam wako.
Taarifa kama hii haihitaji kuwa na makonakona mengi yasiyoeleweka.
Wewe ulishuhudia yote yaliyotokea Kimara hadi Ubungo huku ukiwa umejibanza kijiweni na washikaji wako uliowatembelea?Sijui ulitaka niiweke vipi ili ieleweke.