BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Siku za hivi karibuni kumekuwa na wimbi la Watu kupotea katika mazingira ya kutatanisha hasa ya Vijana wenzetu.
Yalianza mdogomdogo lakini kadiri siku zinavyozidi Kwenda mbele kumekuwa na taarifa za hapa na pale kuhusu fulani na fulani kupotea, binafsi nimeanza kupata hofu licha ya kuwa Jeshi la Polisi limekuwa likitoa kauli flani za kuonesha hakuna kitu kibaya.
Hivi nini kinaendelea?
Unajua hizi mambo za matukio ya “kutisha” tulishaanza kuyasahau lakini yameanza kurejea.
Hivi karibuni tumeona baadhi ya Vyombo vya Habari na Mitandao ikizungumza kuhusu yule Sativa alivyopotea na kupatikana akiwa amechakazwa kwa kujeruhiwa vibaya.
Kiukweli sisi Wananchi tunaumizwa na kutishwa na hali inayoendelea kwasasa. Imefika hatua tunaanza kuogopa hata kukutana na watu tusiowafahamu huku mitaani.
Soma Pia: Freeman Mbowe: Viongozi wa CHADEMA na Watanzania wasio na Vyama wanaoendelea kutekwa na Vyombo vya Usalama vya Nchi yetu
Tunaomba Mamlaka zikomeshe haya matukio kwakuwa yanatishia usalama wetu, yanachafua taswira ya nchi yetu kitaifa na kimataifa. Pia, huu sio utamaduni wetu Watanzania.
Pia soma ~ Vijana Kariakoo wanapotea sana, Serikali iingilie kati