KERO Matukio ya wizi na kuvunja nyumba za watu Miembe 7B, Kibaha yamekuwa mengi

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Zamani, Kibaha kwa Mfipa ndiyo iliyokuwa ikijulikana kwa matukio ya wizi, lakini kwa sasa hali hiyo imeanza kujitokeza pia katika maeneo ya kuanzia Miembe 7B hadi Mikoo.

Wananchi wa maeneo hayo wanakabiliwa na wimbi la wizi, ambapo wezi huvunja milango ya nyumba na kuiba vitu mbalimbali, ikiwemo kuku, televisheni na mali nyingine za nyumbani.

Tunaomba mamlaka husika, hususan Jeshi la Polisi, zifuatilie hali hii na kuchukua hatua za kukomesha wimbi hilo la uhalifu ili kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao.
 
Chomeni mmoja au wawili. Mtaona.
Haiwezekani kwa sababu Picha, kwa mathias, msangani, kwa mfipa, tanita, mwendapole hadi kongowe kuna makazi mengi ya wanajeshi wanaoishi uraiani na hao wezi ni ndugu zao wanaowalea majumbani mwao.

Hajasema tu kingine eneo lao lina wizi mkubwa wa mita za maji na hamna kitu watafanya
 
Sasa kama mnawafukuza kariakoo na kubomoa biashara zao mnategemea waende wapi?
 
Haiwezekani kwa sababu Picha, kwa mathias, msangani, kwa mfipa, tanita, mwendapole hadi kongowe kuna makazi mengi ya wanajeshi wanaoishi uraiani na hao wezi ni ndugu zao wanaowalea majumbani mwao.

Hajasema tu kingine eneo lao lina wizi mkubwa wa mita za maji na hamna kitu watafanya
Bora umesema wewe.
 
Kwan kuwepo wajeda ndo kufanye wezi wasiibe wajeda wenyewe wanaibiwa ..usikariri maisha kijana
 
Back
Top Bottom