Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
HISTORIA YA MKOA
Mkoa wa Tanga ni moja kati ya mikoa 31wenye eneo la 27,348 km² na upo Kaskazini Mashariki mwa Tanzania ukipakana na Kenya upande wa Kaskazini, Bahari Hindi upande wa mashariki na mikoa yaTANGA Morogoro, Manyara na Kilimanjaro. Mpaka upande wa kusini unafuata mto wa Mligaji. Mkoa wa Tanga unaunganisha sehemu za pwani pamoja na milima ya ndani kama Usambara.
Tanga inasemekana imeanzishwa na wafanyabiashara Waajemi katika karne ya 14 baada ya kristo, Baada ya kuanzishwa kwa ukoloni wa Kijerumani (DOA) mji ulikuwa makao makuu ya mkoa wa Tanga.
Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 yanaonesha kuwa idadi ya watu katika Mkoa wa Tanga ni 2,615,597; wanaume 1,275,665 na wanawake 1,339,932.
SOMA PIA
MUHTASARI WA MAENEO YA UTAWALA, MKOA WA TANGA
Mkoa wa Tanga ni moja ya mikoa ya kaskazini mwa Tanzania, ukiwa na mfumo wa utawala unaojumuisha mamlaka za miji na wilaya. Mkoa huu umejigawa katika maeneo tofauti ya kiutawala kwa lengo la kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi na kusimamia maendeleo.
Chanzo: TAMISEMI
Kwenye upande wa mamlaka za miji;
1. Mji wa Handeni una kata 12 na mitaa 60.
2. Mji wa Korogwe una kata 11 na mitaa 29.
3. Jiji la Tanga lina kata 27 na mitaa 181.
Jumla kwa mamlaka hizi za miji ni kata 50 na mitaa 270.
Mamlaka za Wilaya
Kwa mamlaka za wilaya, kuna wilaya nane ambazo zinasimamia maeneo ya vijijini.
1. Wilaya ya Bumbuli ina kata 18, vijiji 83, na vitongoji 673.
2. Wilaya ya Handeni ina kata 21, vijiji 91, na vitongoji 770
3. Wilaya ya Kilindi ina kata 21, vijiji 102, na vitongoji 611.
4. Wilaya ya Korogwe ina kata 29, vijiji 118, na vitongoji 610.
5. Wilaya ya Lushoto ina kata 33, vijiji 125, na vitongoji 942.
6. Wilaya ya Mkinga ina kata 22, vijiji 85, na vitongoji 335.
7. Wilaya ya Muheza ina kata 37, vijiji 126, na vitongoji 494
8. Wilaya ya Pangani ina kata 14, vijiji 33, na vitongoji 96.
Kwa ujumla, wilaya za mkoa wa Tanga zina jumla ya kata 195, vijiji 763, na vitongoji 4,531, wakati mamlaka za miji zina kata 50 na mitaa 270.
Mkoa wa Tanga unafikia jumla kuu ya kata 245, mitaa 270, vijiji 763, na vitongoji 4,531, ukionyesha muundo wa utawala unaolenga kuleta uwiano mzuri kati ya maeneo ya mijini na vijijini katika utoaji wa huduma na maendeleo ya kijamii.
MAJIMBO YA KIUCHAGUZI
Mkoa wa Tanga una jumla ya majimbo 12 ya kiuchaguzi. Majimbo haya ni Tanga Mjini, Muheza, Pangani, Korogwe Mjini, na Korogwe Vijijini. Pia kuna majimbo ya Handeni Mjini, Handeni Vijijini, na Kilindi, ambayo yanapatikana katika maeneo ya katikati ya mkoa. Vilevile, majimbo ya Lushoto, Mkinga, Mlalo na Bumbuli yanakamilisha idadi ya majimbo ya kiuchaguzi katika mkoa huu.
HALI YA KISIASA
Mkoa wa Tanga ni miongoni mwa mikoa ambayo kwa kiwango kikubwa nafasi za uongozi katika ngazi za serikali za mitaa, udiwani na ubunge zinashikiliwa na Chama cha Mapinduzi CCM ambapo hali hiyo ilisababishwa na uchaguzi wa serikali za Mitaa mwaka 2019 na uchaguzi mkuu 2020.
uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 uliwapitisha bila kupingwa wagombea wa CCM huku mikoa mingine ambayo wagombea wake walipita bila kupingwa ni Katavi, Ruvuma na Njombe
Katika uchaguzi wa serikali za mitaa watia nia wa nafasi za uongozi katika nafasi hizo kutoka vyama vya upinzani walienguliwa kwa madai ya kukosa sifa za kugombea nafasi hizo na hivyo kupelekea kuondoa ushindani katika uchaguzi huo na kuacha wagombea wa Chama tawala CCM kupita bila kupingwa.
Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024, inatarajiwa kuwepo kwa mabadiliko na uimarishwaji wa demokrasia ili kutoa nafasi kwa vyama vyote kushiriki kikamilifu kwa uhuru na haki katika uchaguzi huo ili kutoa fursa kwa wananchi wote wenye mitazamo na milengo tofauti kugombea nafasi hizo.
MATUKIO KUELEKEA NOVEMBA 27
- Rais Samia Kuzindua Rasmi Zoezi la Kuandikisha Wapiga Kura wa Serikali za Mitaa
- LIVE - Rais Samia anashiriki zoezi la Uandikishaji kwenye Daftari la Wapiga Kura kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
- LGE2024 - News Alert: - Waziri Mchengerwa afafanua kuhusu mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mtaa, leo Oktoba 15, 2024
- LGE2024 - Waziri Mchengerwa: Jumla ya wapiga kura milioni 31, 282,331 wamejiandikisha kupiga kura Uchaguzi Serikali za Mitaa 2024
- Kuelekea 2025 - LGE2024 - Mahakama yaipa Ruhusa TAMISEMI kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
- Wananchi wataka vikwazo vya ushiriki mdogo chaguzi za 2019 na 2020 vishughulikiwe kuongeza ushiriki chaguzi za 2024 na 2025
- Katibu Mkuu NLD ampongeza Rais Samia kwa 4R zilizoleta matumaini kwa vingine vya siasa, awaasa wapinzani kufata sheria wakati wa uchaguzi
- CCM: TAMISEMI itambue demokrasia yetu ni changa, ipuuze makosa madogomadogo katika hatua ya rufaa uchaguzi Serikali za mitaa
- Tanga: Mrakibu Msaidizi wa Polisi Michael Kaniki awataka wananchi kujiepusha na vurugu wakati wa Uchaguzi 2024 na 2025
- Mchengerwa: Wagombea ambao hawajaridhishwa na uteuzi, waweke pingamizi
- Polisi: Kuna chama cha Siasa kinapanga kufanya Vurugu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
- Mkuu wa mkoa Tanga: Wasimamizi wa uchaguzi Tumieni 4R za Rais Samia
- Makalla: Chagueni wagombea wa CCM wale wa CHADEMA Mbowe kasema hawana ILANI ni hatari kuwa na kiongozi bila kuwa na Mkataba wa atakufanyia nini
- Jussa: Chama cha upinzani chenye muelekeo ni ACT- WAZALENDO
- Chama cha NLD chatoa ahadi ya kushughulikia changamoto za migogoro ya ardhi wilayani Handeni
- Mwenyekiti wa UVCCM Tanga, Ramadhan Omar awataka wananchi kuchagua viongozi wa CCM katika nafasi zote "Ndio Chama chenye dira"
- Askofu Tanga: Siku kabla ya kupiga kura msisahau kuombea Uchaguzi wa mwaka huu kwani ni maandalizi ya uchaguzi wa mwakani
- Tanga: Katibu mkuu wa chama cha sauti ya umma(SAU), Majalio kyara amewasihi Wananchi kutokuuza utu wao Serali za Mitaa
- Juma Aweso: Wananchi jitokezeni kwa wingi kupiga kura tarehe 27 Nov 2024
- Shamira Mshangama: Tusifanye makosa, Siasa ni maisha na CCM ndio Chama pekee kinachoweza kutatua kero za Watanzania
- Chama cha NLD chatoa ahadi ya kushughulikia changamoto za migogoro ya ardhi wilayani Handeni
- Tanga: Mkuu wa Mkoa Batilda Buriani atoa wito kwa Wananchi kuondoka Vituoni baada ya Kupiga Kura
- Tanga: Waziri Aweso ajitokeza kupiga Kura
- Bumbuli: January Makamba ajitokeza kupiga kura
- Mchengerwa: Matokeo ya uchaguzi kutangazwa ndani ya saa 72
- ACT Wazalendo waelezea rafu walizokutana nazo katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
- Tanga: Watu wanne wakamatwa na Jeshi la Polisi kwa kufanya vurugu kwenye vituo vya kupigia kura
- Viongozi wa Dini na Siasa Tanga waridhishwa na Uchaguzi Serikali za Mitaa