Ben Zen Tarot
JF-Expert Member
- Dec 13, 2014
- 4,298
- 7,612
Moja kati ya Matukio ya kufedhehesha na ambayo hayatasahaulika aliyoyafanya Idd Amin kule Nchini Uganda ni lile tukio la kuwauwa Omba Omba vilema waliokuwa wakiishi mjini kampala baada ya kuwakusanya na kwenda kuwamwaga ndani ya mto Nile.
Sababu kubwa ya Idd Amin kuwamwaga ombaomba hao ndani ya mto Nile ni kutokana mmoja wa vilema hao Ombaomba kufikia hatua ya kumlaumu Idd Amin hadharani walipokutana uso kwa uso mjini Kampala, Idd Amin alilaumiwa juu ya hatua yake ya kuwafukuza wawekezaji nchini humo bila sababu za msingi.
Idd Amin aliulizwa nchi itaendeleaje bila wawekezaji ? Na sisi s itutakufa kwa njaa kwa sababu ajira hazitakuwepo? watu hawatakuwa na pesa hata zakutusaidia sisi ombaomba, alimalizia kwa kumuambia wewe Idd Amini ni zaidi ya kichaa. Baada ya kumwambia Amin maneno yale makali ndipo Maliyamungu aliyekuwa mtu wa karibu sana na Amin alichomoa silaha aina ya Pistol kwa lengo la kumuua lakini Amin alimtuliza asifanye hivyo kisha wakaondoka.
Siku iliyofuata wanajeshi wa Idd Amin walimtafuta na kumkamata yule ombaomba na kuondoka nae na hapo ukawa mwisho wakujua historia ya ombaomba yule, hata hivyo inasadikika aliuwawa. Wiki moja baadae ndipo taarifa zikatolewa kwamba vilema ombaomba waishio mjini Kampala waripoti kwenye vituo vya polisi ili wapatiwe misaada.
Mamia ya ombaomba walikwenda kuripoti vituo vya polisi ili kusubiri misaada ya Amin lakini walipofika huko mambo yalikuwa tofauti na vile walivyoambiwa, kwani walikusanywa kwa pamoja na kupandishwa kwenye magari Aina ya Tipper kisha kupelekwa hadi lilipokuwa Daraja la Karuma Falls ambapo ni umbali wa km 200 kutoka Kampala kwenda Gulu, Daraja hilo la Nkurumah Falls lipo umbali wa takriban mita 100 kutoka kwenye maporomoko hayo.
Hapo Askari waliamriwa kuwamwaga ombaomba hao wasiojiweza ambapo walisafirishwa na maporomoko hayo hadi Mto Nile na huo ukawa mwisho wa historia yao. Idd Amin alisema kwamba aliamua kufanya Vile ili kuondoa kero na usumbufu wa Ombaomba mjini kampala.
Nb: hizi ninazoandika siyo propaganda ni ukweli kabisa wa matukio aliyoyafanya Amin.