BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha TLP, Augustino Mrema amefariki duninia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Dar es Salaam alikokuwa anapatiwa matibabu.
Mrema (77) aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, amefariki dunia leo Jumapili, Agosti 21, 2022, asubuhi, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.
Muda mfupi baada ya taarifa za kifo cha Mwenyekiti huyo chama cha TLP, Rais Samia Suluhu Hassan alituma salamu za pole kwa familia na TLP.
Pia baadhi ya vyama vya siasa navyo vilituma salamu za pole kwa familia na Chama cha TLP kufuatia kifo hicho.
Mrema alizaliwa katika kijiji cha Kiraracha, Marangu mkoani Kilimanjaro Desemba 31, 1944 na alipata elimu ya awali katika shule ya kati mwaka 1955-63 kabla ya kujiunga na Chuo cha Ualimu cha Mtakatifu Patrick 1964-65.
Mwaka 1970-71 Mrema alijiunga kwenye mafunzo maalumu ya siasa na uongozi katika Chuo cha Kivukoni na baadaye alikwenda kusoma nchini Bulgaria ambako alitunukiwa Diploma ya Sayansi ya Ustawi wa Jamii na Utawala mwaka 1980-81.
Mrema alianza kazi ya ualimu mwaka 1966 na kufundisha shule mbalimbali za mkoa wa Kilimajaro ambapo mwaka 1972 aliteuliwa kuwa mratibu wa elimu wa Kata hadi 1973.
Baada ya kuhudumu katika nafasi hiyo, mwaka 1974 alichaguliwa kuwa mwalimu wa siasa katika wilaya mbalimbali kwa niaba ya TANU na baadaye Chama cha Mapinduzi (CCM) hadi mwaka 1980.
Mreka aliteuliwa kuwa Kaimu Mkuu wa Usalama wa Taifa kwa mkoa wa Dodoma mwaka 1982-84 na baadaye mwaka 1984 akateuliwa tena kuwa Katibu wa kikosi cha ulinzi na usalama makao makuu Dodoma.
Oktoba 1985 Mrema aligombea ubunge Jimbo la Moshi Vijijini na kushinda kwa kupata kura 38,984 dhidi ya mpinzani wake Peter Macha aliyepata kura 34,709 na aligombea tena kwa awamu ya pili Oktoba 28, 1990, Mrema ambapo alifanikiwa kutetea kiti hicho.
Novemba 9, 1990 Rais Ali Hassan Mwinyi, alimteua Mrema kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanyika Desemba 7, 1994 aliondolewa Wizara ya Mambo ya Ndani na kupelekwa katika Wizara ya Kazi, Maendeleo ya Vijana na Michezo.
Februari 25, 1995: Rais Mwinyi, alimfukuza Mrema kwenye Baraza la Mawaziri kwa kuikana Serikali bungeni kutokana na mjadala bungeni mjini Dodoma baada ya kuchapishwa kwa Ripoti ya Kamati ya Bunge kuhusu masuala ya mfanyabiashara maarufu ambaye si raia na mmiliki wa mashamba kadhaa Vidyadhar Girdharlal (V.G.) Chavda.
Machi 3, 1995: Mrema alijitoa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na NCCR-Mageuzi.
Mrema aligombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi ulifanyika nchini uliofanyika Oktoba 29, 1995. Hata hivyo, Mrema alishindwa na Benjamin Mkapa katika uchaguzi huo. Wagombea urais katika uchaguzi huo walikuwa ni Benjamin Mkapa (CCM) aliyepata kura 4,026,422 (61.82%), Augustine Mrema (NCCR-Mageuzi) kura 1,808,616 (27.77%), Profesa Ibrahim Lipumba (CUF) kura 418,973 (6.43%) na John Cheyo (UDP) kura 258,734 (3.97%).
Oktoba 6, 1996 aligombea na kushinda ubunge Jimbo la Temeke kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi kwa kupata kura 54,840 ambazo ni sawa na asilimia 59 ya kura zote. Abdul Cisco Mtiro kwa tiketi ya CCM (33,113) ambazo ni sawa na asilimia 36 ya kura zote, Hiza Tambwe kwa tiketi ya CUF (3,324), Alec Che Mponda kwa tiketi ya TPP (515) na Mege Omar kwa tiketi ya UMD (422).
Mwaka 1999, Mrema alijiuzulu ubunge wa Temeke na kuamua kuhamia chama cha Tanzania Labour Party (TLP).
Oktoba 25, 2015: Mrema aliangushwa ubunge katika Jimbo la Vunjo na James Mbatia wa NCCR-Mageuzi aliyepata kura 60,187 dhidi ya kura 16,617 za Mrema.
Mei 7, 2020, Mkutano Mkuu wa Taifa TLP ulimpitisha Dk John Magufuli kuwa mgombea pekee anayeungwa mkono na TLP 2020.
Septemba 16, 2021: Mke wake, Rose Mrema, alifariki dunia saa nane mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua ghafla baada ya kupata mshtuko wa moyo kutokana na mishipa mitatu kuziba kwa muda mrefu.
Machi 24, 2022 Mrema alifunga ndoa na Doreen Kimbi baada ya mke wake wa kwanza kufariki mwaka 2021.
Agosti 21, 2022, Mrema anafariki dunia akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.