Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 11,557
- 33,535
Wadau mbalimbali wakiwemo wanasiasa na wajasiriamali, wamepongeza tozo mpya katika mitandao ya simu na mafuta zilizopitishwa mwaka wa fedha 2021/2022. Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wadau hao walisema tozo hizo zitachochea ukuaji wa uchumi hasa katika maeneo ya vijijini.
Walisema tozo hizo zitatumika kugharamia miradi ya kimkakati ya manedeleo iliyomo katika ilani ya uchaguzi ya CCM katika ujenzi wa barabara, elimu, maji na afya. Akizungumza na gazeti hili jana, Jaffery Kubecha ambaye ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM (MNEC) kupitia vijana, alisema kinachopaswa kutazamwa si tozo bali ni wapi fedha zitaelekezwa. Kubesha alisema serikali imeweka wazi kuwa tozo hizo zinakwenda kuchochea manedeleo ambapo ya miamala itaboresha barabara mjini na vijijini na mafuta itajikita katika sekta ya maji na umeme. Alisema katika kufanikisha dhamira ya kutoka huduma kwa wananchi, serikali kupitia bunge iliazimia kutafuta vyanzo vipya vya mapato, ambapo tozo hizo ni sehemu ya utekelezaji wake.
Alitolea mfano nchini China, ambapo mwaka 2013 walilazimika kuongeza tozo katika kodi kwa asilimia 3 kuchangia elimu, walifanya hivyo wakilenga kuboresha huduma kwa wananchi. Kubecha alisema lengo la ongezeko la tozo hizo ni kuiishi ile dhana ya wananchi wanawajibika kujenga nchi. "Ni kweli inaumiza lkaini kwa sababu imeelekezwa katika sekta muhimu zahuduma kwa wananachi wenyewe hatuna budi kufunga mkanda, kilio ni cha leo tu kesho tutacheka" alisisitiza.
Pia alieleza katika kuhakikisha wananchi wanakuwa na uwezo wa kulipa tozo hiyo, serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imeseama inatoa sh trillioni 15 kulipa wananchi fedha wanazodai. Alisema malipo hayo yataongeza mzunguko wa fedha nchini, hivyo wananchi watakuwa na vipato vitakavyowawezesha kumudu tozo hizo. Kubecha alisema maumivu ya tozo hizo ni ya muda mfupi amabpo hivi karibuni yatafikia ukingoni baada ya kuonekana faida zake.
Katibu wa Umoja wa Vijana waa CCM kata ya Msigani, Reinhad Chikando, alisema serikali imeeleza lengo la tozo hiyo, hiyvo wananchi wanapaswa kutekeleza. Alishauri ili kujenga hamasa kwa wananchi kuendelea kulipa, serikali ihakikishe inaimarisha usimamizi wa fedha hizo na zitumike katika shughuli zilizolengwa. Chkiando aliongeza kuwa si rahisi kwa taifa kupiga hatua ya maendeleo bila kupitia maumivuhivyo wanachopitia Watanzania ni hatua za kulikwamua taifa. Alisisitiza kuwa wananchi wanapaswa kutulia na kujenga imani kwa serikali yao ili kuisaidia kuifikisha nchi panapotarajiwa.
Naye Wafeba Kibode ambaye ni Katibu Hamasa na Chipukizi wa UVCCM kata hiyo alisema tozo hizo ni kilio cha leo lakini kicheko cha kesho, hivyo inahitaji uvumilivu wa muda mchache ili kufikia mafanikio.
Naye mjasiriamali wa soko la Kariakooo, Jasmine Kulwa alisema ana matumanini kuwa tozo hizo zitaleta manufaa kwa wancnchi, baada ya kuona zikitumika ipasavyo. "Sina ufahamu wa kutosha kuhusu masuaka ya tozo, lakini nimesoma nimeona kwamba serikali ina nia njema ya kuwaletea wananchi maendeleo. Nashauri watanzania tuwape muda viongozi wetu kwa ajili ya utekelezaji" alisema Jasmine. Mjasiriamali huyo alimtaka Waziri wa Fedha na Mipango Migulunchemba kuendelea na mikakati ya kuijenga nchi.
Mamalishe Amina Ndembo alisema licha ya maumivu hayo, anaamini serikali ina nia thabiti ya kuwaletea maendeleo wananchi na kuongeza kuwa jambo la msingi ni uwazi katika matumizi ya fedha hizo.
Maoni ya wadau hao uamekuja muda mfupi baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, awala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu, kueleza kuwa tozo hizo mpya zitaongeza kasi ya upatikanjai wa huduma muhimu kwa wananchi wa maeneno ya vijijini kwa lengo la kupunguza ukali wa maisha. Ummy alisema hayo wakati akizindua ujenzi wa barabara ya Santa Maria-Kabage yenye urefe wa km 16 katika Halmashauri ya Wiaya ya Tanganyika mkoani Katavi. Alisema tozo zilizoanza kutozwa tangu kwa mwaka huu wa fedha, zitatumika kugharamia miradi ya maendeleo kaitka sekta za barabara, maji, elimu na ujenzi wa vituo vya afya maeneo ya vijijini.