Matumizi Affidavit na deedpoll

Matumizi Affidavit na deedpoll

Mike Moe

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2019
Posts
319
Reaction score
335
Habari za wakati huu wanajami mwaka jana mwezi wa 11 niliemda utumishi kwa ajili ya usahili lakini kutokana na changamoto ya majina katika vyeti vyangu nikalazimika kutafuta affidavit ili iwe msaada katika kutatua hilo na kweli nilifanikiwa kufanya usahili sasa siku ya jana utumishi wameita watu kazini kwa msaada wake mola na mimi ni miongoni mwa watu walioitwa kazini, naomba kuuliza ndugu affidavit ile ile nilionayo naweza kwenda nayo kwa mwajiri au kuna kitu kingine cha kuwa nacho tofauti na hiyo affidavit huwa na skia kuhusu habari za deedpoll na kujuzwa kuhusu hili jambo
Asante!
 
Safi Nina shida kama yako
Na Mimi nilikuwa nahitaji kujua tofauti ya affidavit na deeppoll

Ngoja wenye uwelewa waje watusaidie
 
Safi Nina shida kama yako
Na Mimi nilikuwa nahitaji kujua tofauti ya affidavit na deeppoll

Ngoja wenye uwelewa waje watusaidie
Ni document tofauti hizo, Affidavit inatoka kwa wakili au mahakamani, lakini deedpol inaandaliwa na wakili na kusajiliwa kabisa wizarani.
 
Ni document tofauti hizo, Affidavit inatoka kwa wakili au mahakamani, lakini deedpol inaandaliwa na wakili na kusajiliwa kabisa wizarani.
Niliongea na Wakili mmoja kumueleza kuwa majina ya vyeti vyangu vya shule ni mawili ila kwenye Nida yapo matatu pamoja na cheti cha kuzaliwa

Akaniambia kuwa natakiwa kuwa deedpol ambayo wakili yeye ndiye anai draft Kisha inaenda kusajiliwa wizarani kwa gharama ya 32000.

Naona umefanana katika maelekezo yake
 
Yuko sahihi, fanya kama alivyokuelekeza.
 
Affidavit ni kama majina yanatofautiana herufi ndiyo mara nyingi hutumika.

Na kila unapohitaji kufanya jambo fulani lazima uchukue Affidavit nyingine kwa kazi husika.

Deedpoll ni hati ya kubadilisha jinaama kurekebisha majina yaliyokosewa na hii inakuwa ya kudumu tofauti na Affidavit ambayo utahitajika kuwa nayo kila mara litokeapo jambo linalohitaji Affidavit. Deedpoll lazima ufike ardhi tofauti na Affidavit ambayo ni kiapo cha mahakama unaweza kupata Affidavit kutoka kwa hakimu ama wakili.

Wengine wenye uelewa zaidi watanisaidia.
 
Back
Top Bottom