SoC04 Matumizi fanisi katika teknolojia ya kidijitali ili kuchochea ukuaji wa mfumo wa elimu Tanzania (e-Student App)

SoC04 Matumizi fanisi katika teknolojia ya kidijitali ili kuchochea ukuaji wa mfumo wa elimu Tanzania (e-Student App)

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
Apr 20, 2024
Posts
25
Reaction score
26
UTANGULIZI.
Taifa lolote ili liendelee linahitaji watu ambao watapandikizwa elimu sahihi, Elimu sahihi inajengwa na mfumo bora wa elimu. Kulingana na ulimwengu tuliopo sasa ili kupiga hatua tunahitaji matumizi ya sahihi ya kiteknologia katika mfumo wa elimu ili kuchochea ukuaji wa elimu yetu.
Andiko langu linajikita zaidi katika kuwa na application kwenye sekita ya elimu (mashuleni) itakayo toa taarifa za maendeleo ya mwanafunzi na taarifa za shule kwa mzazi/mlezi kwa wepesi na wakati kupitia ujumbe mfupi wa maandishi. Application hii inafahamika kama, e-Students (Students Performance Tracker).

e-Students (STUDENT PERFORMANCE TRACKER) ni nini??
Ni mfumo wa kidijitali ambao unafuatilia maendeleo ya mwanafunzi kwa ushirikishwaji na ushirikiano wa Mwalimu/Mwanasaikolojia, Mwanafunzi na Mzazi/Mlezi. Mfumo huu unatumika kufikisha ujumbe mfupi wa maandishi kwa Mzazi/Mlezi kupitia simu ya mkononi (Whatsapp Messages), Pia Mzazi/Mlezi ataweza kuingia (Log in) kwenye mfumo na kuangalia maendeleo ya mwanafunzi na taarifa mbalimbali zinazo husu shule husika.
Application itahusisha taarifa zifuatazo:-
{1}. Kupima Matokeo ya Ufaulu (Results) ya mwanafunzi.
{2}. Kupima Matokeo ya Uelewa (Thinking Ability) ya mwanafunzi.
{3}. Kupima hali ya kisaikolojia ya mwanafunzi (Tabia/Mwenendo).
{4}. Kuomba kukutana na Mwalimu/Mwanasaikolojia. (Appointment arrangements btn parties).
{5}. Kutoa taarifa muhimu za shule husika, ambazo zinahitajika kumfikia Mzazi/Mlezi.

e-Stundents Application inajumuisha/Inahitaji mambo yafuatayo ili kutenda sawa sawa na lengo tarajiwa:-
{a}.- Kuwa na Wana/Mwanasaikolojia mashuleni.
Ndani ya e-Students application kutakuwa na taarifa ya upimaji wa hali ya kisaikolojia ya mwanafunzi, Hivyo napendekeza kila shule kuwa na mwanasaikologia, ambae atakuwa akitathimini na kuwasaidia watoto katika changamoto zozote za afya ya akili. Watoto wamekuwa wakipitia changamoto nyingi ambazo zinawaathili sana kisaikolojia ila hawana sehemu ambayo watakuwa huru kueleza changamoto zao, hivyo Mwanasaikolojia anakuja kutatua changamoto za afya ya akili na kuwajenga kiakili wanafunzi, na hizi taarifa za hali ya kisaikolojia zitakuwa zikiambatanishwa kwenye ripoti ya matokeo ya mwanafunzi.
{b}.- Wanafunzi kupimwa kwa uelewa (Thinking Ability) na si ufaulu pekee, kama ilivyo sasa.
Ndani ya e-Students application kutakuwa upimaji wa uelewa darasani kwa mwanafunzi. Napendekeza wanafunzi kupimwa kwa uelewa pia sio ufaulu tu, Upimaji huu wa uelewa, utasaidia kukijenga kizazi kuwa na uwezo wa kufikiria, kukabiliana/kumudu mazingira na kutokuwa na kizazi tegemezi. Taarifa za uelewa zitaambatanishwa kwenye ripoti ya mwanafunzi husika.

Msimamizi wa mfumo wa e-Students.
Mfumo utakuwa chini ya uangalizi/usimamizi wa Wizara ya Elimu, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Wilaya na Mikoa itapewa usimamizi mdogo kwa ajili ya kuratibu shughuli za maeneo husika (Shule husika).

e-Student (STUDENT PERFORMANCE TRACKER).
Mfano wa Application ya e-Students.
e-student_all@willgraphicstz_092538.jpg

Chanzo: willy GraphicsTz

Utendaji/Yaliyomo kwenye Application ya e-Student (STUDENT PERFORMANCE TRACKER).
1. Kila mwanafunzi atasajiliwa katika mfumo wa e-Student application.
2. Application itaonyesha taarifa zifuatazo za mwanafunzi.
-• Picha ya mwanafunzi.
-• Majina ya mwanafunzi.
-• Umri wa mwanafunzi.
-• Jinsia ya mwanafunzi.
-• Darasa la mwanafunzi.

3. Application itaonyesha matokeo ya mwanafunzi.
-• Ufaulu wa Mwanafunzi.
-• Uelewa wa Mwanafunzi.
-• Hali ya kisaikolojia ya mwanafunzi.

4. Ujumbe mfupi wa maandishi.
Ujumbe mfupi wa maandishi, utafika kwenye simu ya mzazi/mlezi husika ili kumfahamisha juu ya Matokeo ya mtoto wake na taarifa za kikao (shuleni).
5. Ndani ya application kutakuwa na Matokeo yote ya mwanafunzi, toka alipoanza shule mpaka darasa alilopo sasa.
6. Mzazi/Mlezi anaweza kuomba kukutana (Appointment arrangements) na mwalimu/mwanasaikolojia kupitia Application/Ujumbe mfupi wa maandishi ili kujadili juu ya maendeleo ya mwanafunzi.
7. Mzazi/Mlezi anaweza kutoa taarifa kwa mwalimu kwa niaba ya mwanafunzi, kama kuomba ruhusu na dharura yoyote.

Kwanini e-Students (Students Performance Tracker).?
Application hii inakuja kutatua changamoto zilizopo katika mfumo elimu tulionao sasa.​
  1. Wazazi/walezi kushindwa kuhudhuria vikao shuleni, kufuatilia maendeleo ya watoto wao shuleni, kutokana na kutingwa na majukumu ya utafutaji, wazazi wamejikuta wakiweka mkazo na nguvu nyingi katika kutafuta fedha zaidi na kushindwa kufuatilia maendeleo ya watoto shuleni.​
  2. Malezi ya mtotoWanafunzi kushindwa kufikisha matokeo ya masomo yao kwa wazazi/walezi na muda mwingine kutoa ripoti za uongo zisizo na uhalisia kwa wazazi/walezi wao.​
  3. Ushirikiano/ Ushirikishwaji hafifu baina ya Mwalimu, Mwanafunzi na Mzazi/Mlezi.​
  4. Kukithiri kwa utovu wa nidhamu na utoro (Wanafunzi kuishia mtaani huku wazazi wakijua kuwa wako shuleni).​
  5. Changamoto za matatizo ya kisaikolojia kwa wanafunzi bila kupata sehemu ya msaada.​

e-Student itaboresha mfumo wa ELIMU kama ifuatavyo.
Matokeo chanya ya kuwepo huu mfumo yanakuja kuchochea na kukuza elimu ya Tanzania kama ifuatavyo;-​
  1. Itasaidia katika ushirikiano na ushirikishwaji kati ya Mwalimu/Mwanasaikolojia, Mwanafuzi na Mzazi/Mlezi ili kuhakikisha maendeleo ya mwanafunzi na maenedeleo ya shule kiujumla.​
  2. Mzazi/Mlezi anaweza kupata taarifa kwa wakati na wepesi, Taarifa zote zinazo husu shule na Maendeleo ya mwanafunzi kwa wakati kupitia application na ujumbe mfupi wa maandishi (Whatsapp Messages).​
  3. Mfumo utawezesha kuomba kukutana (Appointment arrangements) kati ya Mwalimu/Mwanasaikolojia na Mzazi/Mlezi ili kujadili maendeleo ya mwanafunzi na shule kiujumla.​
  4. Inakuja kutatua tatizo la kisaikolojia kwa wanafunzi na kujenga kizazi katika misingi imara ya kiakili/kisaikolojia.​
  5. Itaongeza uwajibikaji na uaminifu wa wanafunzi kwa kujua kuwa taarifa zote za maendeleo yao zinafika moja kwa moja kwa wazazi/walezi wao.​
  6. Hailengi tu wale wenye simu Janja (Smartphones) ila hata wenye simu kitochi, wanaweza kupokea taarifa za mwenendo wa mtoto shuleni na taarifa mbalimbali zinazohuau shule.​
  7. Mzazi/Mlezi ataweza kutoa taarifa kupitia simu yake ya mkononi ya dharura kuhusu mtoto na taarifa itawafikia walimu.​

HITIMISHO.
Teknolojia ya kidigitali imekuja ili kurahisisha kazi na kasi ya maendeleo zaidi. Tuhakikishe tunaitumia ipasavyo kwani itatusukuma zaidi kimaendeleo katika sekta zote.​
 
Upvote 1
Back
Top Bottom