KERO Matumizi holela ya Vilipuzi vya kupasua Mawe eneo la Wikichi, Njombe

KERO Matumizi holela ya Vilipuzi vya kupasua Mawe eneo la Wikichi, Njombe

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Blessed Agent

Member
Joined
Nov 16, 2020
Posts
31
Reaction score
34
Habari JF,

Kuna kero kubwa katika Mtaa wa Wikichi, Halmashauri ya Mji wa Njombe, inayosababishwa na wachimbaji na wapasuaji wa miamba ya mawe kwa ajili ya ujenzi.

Wachimbaji hao wanatumia vilipuzi kama baruti vinavyosababisha milipuko mikubwa na mitetemo inayofanana na milipuko ya mabomu. Kinachotia wasiwasi zaidi ni kwamba shughuli hizo zinafanyika karibu na makazi ya watu, takribani mita 200 kutoka kwenye nyumba za wakazi.

Milipuko hiyo inasikika kwa nguvu kiasi cha kutikisa nyumba na kusababisha hofu miongoni mwa wakazi. Watoto hukimbia kwa taharuki kila milipuko inapotokea, huku baadhi ya wakazi wakilalamikia maumivu ya masikio kutokana na sauti hizo kali.

Jambo la kusikitisha ni kwamba shughuli hizo zinaonekana kufanyika bila tahadhari za kutosha kuzingatia afya na usalama wa watu wanaoishi jirani na machimbo hayo.

Tunaomba Serikali na mamlaka husika zifike eneo hilo kuchunguza shughuli hizo na kuhakikisha kuwa vilipuzi vinatumika kwa kuzingatia sheria, taratibu na viwango vya usalama vinavyotakiwa
 
Ila watu mnakuwaga hamna akili, unakuta mtu kajenga mlimani hata kufika tu kipengele, karibu na shule tena ya msingi, sehemu kama hiyo ya machimbo ya mawe, karibu na machinjio ya ng'ombe, karibu na dampo, karibu na mto

Hivi matahira tutaisha lini
 
Back
Top Bottom