Matumizi mabaya ya dawa ni hatari kwa afya zetu

Magnificient

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2013
Posts
1,162
Reaction score
705
Habari ndugu zangu watanzania! Kwa muda sasa nimechunguza na kugundua kwamba wengi wetu tunatumia vibaya dawa kwa ajili ya matumizi mbalimbali kwa afya zetu. Taarifa ni kwamba hii tabia ni hatari sana, kwa sasa na zaidi kwa baadae. Wengi wetu hatutumii dawa vizuri, kwa mfano
1. Mtu anapewa na kuchukua dawa dozi za kutosha kutibu ugonjwa wake, lakini hamalizi dozi; akipata afadhali tu anaacha kutumia dawa
2. Wengine hawanywi dawa kwa wakati, kama walivyopangiwa na wafamasia na madaktari
3. Kuna baadhi ya wafugaji wanalisha mifugo yao dawa za binadamu, na kupelekea dawa hizo kufika kwa binadamu wakila nyama zao. Mfano ni vidonge vya majira na dawa za ukimwi kupewa kuku, nguruwe, ng'ombe n.k.
4. Kunywa dawa kiasi kingi zaidi ili kupona haraka, au wengine kuharibu mimba
5. Kutumia dawa tofauti na matumizi tuliyopangiwa na wataalamu wetu

Hiyo ni mifano michache tu kati ya mingi iliyopo, na matokeo yake ni kwamba tunadhuru na kuharibu miili yetu taratibu, na baadae mwili hudhurika sana na tusijue sababu. Pia magonjwa yanakuwa ni magumu kupona na hata wadudu wake kuwa sugu, na dawa husika kushindwa kufaa. Kubwa zaidi ni kwamba ulemavu na kifo vinawezekana kutokea. Fikiria sasa wanaume wengi kuwa na matiti makubwa, malaria na magonjwa mengi ya bakteria kutotibiwa na dawa zilizokuwa zinafaa mwanzo, cancer, mimba kuharibika na kupoteza kizazi na kadhalika; yote haya ni matokeo ya tabia hii. Naomba nitumie fursa hii kujihusia mwenyewe na kuwahusia nyinyi watanzania wenzangu, tuache matumizi mabaya ya dawa kwani tunajiharibia sana afya zetu, kwa sasa na baadae. Tutumie dawa kama ilivyopangwa na kuelekezwa na wataalamu wa afya. Nawasilisha ......
 
Umesema kweli,asante sana kwa ushauri wako.
 
Back
Top Bottom