Matumizi mabaya ya Media kwa Viongozi Wateule Serikalini

Matumizi mabaya ya Media kwa Viongozi Wateule Serikalini

AeIoU

Senior Member
Joined
Mar 14, 2008
Posts
178
Reaction score
139
Ndani ya miezi miwili tumeshuhudia viongozi wakubwa wawili toka enzi za awamu ya mwendazake wakikutana na madhila makubwa tu kutokana na tabia yao ya kujikomba/kujipendekeza/kujiparata kwa kiongozi anayehusika na teuzi na mamlaka ya kinidhamu dhidi yao.

Hawa ni wafuatao:
1. Lengai ole Sabaya - Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai
2. Albert Chalamila - Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza.

Walitumia media ili kutafuta kiki lakini wote waliumbuka. Toa maoni yako!!!!
 
Huyu mwingine Paul Christian Makonda Yeye si tu alivitumia bali alivitisha huku akivilazimisha anapokuwa ( hata Usiku wa manane ) viwe vinamfuata katika Matukio na ambao walikuwa hawaendi wanajua Kisasi walichofanyiwa hadi wengine kwa Kumuogopa na Kujipendekeza Kwake wakaanza hata Kumlamba Miguu yake.
 
Gentamycine umenena ukweli
Media huwapandisha na kuwaangamiza hakika
 
Ogopeni kitu kilichoundwa na mzungu, au kilichotoka kwa mzungu...
 
Bado tuna safari mdefu sana....yule wa jalalani yu wapi na mimacho yake
 
Back
Top Bottom