Matumizi makubwa ya Kungumanga huweza kusababisha kuchanganyikiwa

Matumizi makubwa ya Kungumanga huweza kusababisha kuchanganyikiwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
MATUMIZI ya muda mrefu kwa kiwango cha uzito wa gramu 120 ya kungumanga, inaweza kuleta madhara kwa mtumiaji, kama kuchanganyikiwa, matatizo kwenye mapigo ya moyo na kusababisha kifo.

Hayo yameelezwa bungeni jana katika majibu ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa swali la Mbunge wa Viti Maalum, Angelina Malembeka (CCM) aliyetaka kujua kama matumizi ya tambuu, mirungi na kungumanga yana madhara kiafya.

Wizara hiyo ilifafanua kuwa ingawa kungumanga inaonesha kuwa na madhara machache zaidi, ikitumika kwa muda mrefu kwa kiwango cha uzito wa gramu 120 inaweza kuleta madhara kama kuchanganyikiwa, kichefuchefu, kizunguzungu, matatizo kwenye mapigo ya moyo na hata kusababisha kifo.

“Matumizi ya tambuu, mirungi na kungumanga ni miongoni mwa vilevi ambavyo vimekuwa vikitumika kwa wingi hasa na watu wanaoishi maeneo ya ukanda wa Pwani ya nchi yetu.

“Kungumanga imekuwa maarufu kama kiungo katika baadhi ya utamaduni hususani watu wenye asili ya Kiasia, lakini imekuwa pia ikitumika kama kilevi kichangamshi kwa baadhi ya watu,” ilisema sehemu ya majibu ya wizara.

Kwa upande wake, tambuu na mirungi vimekuwa vikitumika kama vilevi vichangamshi muda wote na mara nyingi watumiaji wamekuwa wakitumia ili kuwafanya wasilale na kufanya kazi muda mrefu na kuleta uchangamfu ndani ya mwili, hata pale miili yao inapochoka kupita kiasi na kuleta madhara makubwa kimwili na kisaikolojia.

“Matumizi ya mirungi na tambuu huhusishwa na kutopata usingizi, kuchanganyikiwa, presha kupanda, moyo kusimama ghafla.

Matumizi ya tambuu pia yanahusishwa na ongezeko la saratani ya kinywa na njia ya chakula, pia ugumba au utasa, matatizo ya moyo, kisukari, ongezeko la ugonjwa wa tezi dume na matatizo ya ini na figo,” ilisema wizara hiyo.
 
Kwa nini kungumanga inaruhusiwa na mirungi inaharamishwa??
 
Back
Top Bottom