Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,734
- 5,750
Hili halina ubishi kabisa kwa sababu kila mtanzania anaona kwa macho yake namna serikali ya awamu ya tano ilivyoweza kufanya mambo makubwa kwa muda mfupi kabisa.
Mfano ni utekelezaji wa mradi mkubwa ambao utakuwa mfano mkubwa wa kuigwa mradi wa tril 6+ za kitanzania ambao umepewa jina la JNHPP.
Pia ujenzi wa reli ya Standard gauge ambao kama ukikamilika utakuwa ni mradi ambao utasaidia kusafirisha mizigo. Sio kwa watanzania tu bali hata kwa jirani zetu ukanda wa Africa mashariki. Na hivyo kuleta nafuu kwa wananchi wa nchi hizi.
Lakini kutekeleza miradi hii sio jambo rahisi kama chama dola hakiwezi kutumia dola vizuri ili kudhibiti wizi na ubadhirifu.
Mfano kwenye mradi wa Sgr polisi wamefanikiwa kiasi kikubwa kudhibiti wezi wa mafuta, vifaa na material ya kujengea na haya ndio matumizi sahihi ya dola.
Pia katika miradi mbali mbali ambayo imekuwa inatekelezwa PCCB wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa fedha zinazotolewa zinafanya kazi inayotakiwa. Hivyo ubadhirifu na ufisadi umedhibitiwa ndio maana tumeshuhudiab Zahanati,vituo vya afya hospital,madaraja n.k vikihengwa kwa kasi.
Kwa mantiki hii Chama tawala kikitumia dola vizuri kutekeleza ilani yake ya uchaguzi kinaweza kukaa madarakani kwa muda mrefu sababu wananchi wanataka matokeo chanya ili waweze kufurahia kodi zao.
Mimi Chagu wa Malunde nikiwa Igunga safarini kuja dar.
0787600790