Chiwa
JF-Expert Member
- Apr 17, 2008
- 4,116
- 4,979
si mzuri sana katika kuandika vichwa vya habari na kwa hapa naomba nikiri lile swali la kwanza enzi zetu la kiswahili nililiruka sikuwa mzuri kwa upande huo hivyo mnaweza kunisahisha ili wakati mwingine niandike vizuri.
muhimu ninachotaka kusema ni kwamba tunaposherehekea sikukuu zetu za kuzaliwa tunaelewa maana yake na tafsiri yake kwa maisha tunayoishi? au tunasherehekea kwa mazoea? sasa leo tuangalie kidogo ni kwajinsi gani muda au miaka yetu inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa kufanikiwa kwetu.
kikawaida kijana anaonekana kuwa mtu mzima anapofikisha miaka 18 na katika kipindi hiki anatakiwa awe tayari amemaliza elimu ya msingi na ikiwezekana kidato cha nne.
kwa kuanzia tuangalie matukio muhimu ambayo anatakiwa kuyafanya kijana aliyeishia darasa la saba na hasa kwa wavulana kwa kuwa kwa kiasi kikubwa waschana hawana maamuzi kulingana na tamaduni zetu.

- kati ya miaka 14-16 anatakiwa awe amemaliza darasa la saba.
- kati ya miaka 18-21 awe ameanza kujitegemea na kipindi hiki pia anaweza kuanza kufikiria kuoa.
- kati ya miaka 19-27 anaweza kuoa japo
- mtoto wa kwanza akimpata akiwa na umri wa chini ya miaka 25 itapendeza na hapa iko hivi:-
- kikawaida kijana mwenye umri huu kazi zake nyingi hutumia nguvu hivyo afikishapo umri wa miaka 45 hawezi kufanya kazi kama mwanzo uwezo wake wa uzalishaji unashuka. hivyo ni kipindi kizuri cha yeye kupunguza majukumu na kutegemea uwekezaji alioufanya akiwa kijana.
- akimpata mtoto akiwa na umri wa miaka 25, atakuwa na umri wa miaka 20 wa kumtunza akiwa na nguvu kwakuwa
- atahitaji miaka 7 ili mtoto aanze darasa la kwanza
- atahitaji miaka 7 mtoto amalize elimu ya msingi
- atahitaji miaka 4 kwa sekondari ya awali
- atahitaji miaka 2 kwa sekondari ya kidato cha tano na sita
- na angehitaji miaka isiyopungua 3 ili aweze kumaliza elimu ya chuo kikuu.
- kwa hiyo mzazi anapofikisha miaka 45 mtoto wake wa kwanza anakuwa ndo kwanza yuko mwaka wa kwanza na bado anaweza kuwa na mzigo mwingine wa kusomesha huku nyuma.
- matokeo yake uwekezaji unaweza kuwa na changamoto kwa kuwa bado anayo mengi yanayo mkabiri na kama tujuavyo watu wenye kipato cha chini hawana starehe nyingi hivyo wanajikuta kuwa na watoto wengi (japo kwa kweli napenda watoto wengi)waliopishana umri mdogo.
- mwisho wa siku mzazi anashindwa kutegemeza familia na kuanza kumtegemea mtoto tokea mkopo wa chuo kulipia ada wadogo zake na yeye kuchelewa kumudu majukumu yake binafsi na matokeo yake umaskini unaendelea kuwazunguka.
- wakati mwingine inafikia baba amestaafu lakini kashindwa kumalizia vyumba viwili alivyoanza kwa kiwanja alichonunua kwa kujinyima.
- hivyo ili tuweze kuwekeza na kuingia vizuri katika biashara lazima tuwe na malengo mazuri huku tukiangalia muda wetu katika kufanikiwa. nimeeleza kwa kifupi lakini tunaweza kupata picha jinsi gani tunavyochelewa fursa zinapungua japo ipo mipango ya MUNGU anavyomfanikisha mwanadamu.
- wakati mwingine tutaangalia kwa elimu ya kidato cha nne ,sita pamoja na chuo.