Habari hiyo imeandikwa kwenye gazeti la Nipashe, Jumamosi Oktoba15, 2016.
Kwa kuwa mimi ni mpenzi na mwumini mwaminifu wa vyakula asilia na matunda, nimeona ni vyema niwashirikishe kujua ubora wa hivi vyakula na matunda kwa afya zetu, vijana na wazee. Hasa vijana acheni kula "junk food" hasa vilivyokaangizwa km chips mayai.
Makala ya NIPASHE kwa ufupi inanukuu ushuhuda wa madaktari kadhaa, kwamba:
1) Maziwa husaidia katika kuimarisha afya ya wanandoa, kwa sababu ya wingi wake wa protini.
2) Asali husaidia kuupa mwili nguvu ambayo ni muhimu kwa tendo la ndoa.
Ili kupata faida ya vyakula hivyo na nitakavyovitaja, ni sharti uwe mlo endelevu. Mtu yabidi ujenge tabia wa kutumia angalau kijiko kimoja cha asali kila asubuhi na jioni na/au glasi moja ya maziwa kila siku.
Kwa asali ni budi iwe ya asili, kwa kuwa ina madini ya chuma ambayo husaidia kutengeneza damu ndani ya mwili. Na kazi ya damu ni kusafirisha hewa ya oxygen kwenye viungo vya mwili (km uume) kwa uhai wake, kufanya kazi vizuri.
Orodha nyingine ya vyakula na matunda, kwa ajili ya kuimarisha uwezo wa tendo la ndoa, ni kama ifuatayo:
1) Mboga za majani: zina vitamini nyingi zinaongeza hisia za kujamiiana
2) Ini: lina wingi wa madini ya zinc ambayo ni muhimu kwa uzalishaji wa homone za kiume (testosterone).
3) Mvinyo mwekundu: husaidia kupunguza uume kukosa nguvu hivyo ni kama kichocheo cha kutahitaji tendo la ndoa.
4) Mayai: yana kiasi kikubwa cha vitamini B5 na B6, ambazo ni muhimu kudhibiti msongo wa mawazo.
5) Ndizi mbivu: japo ina mwonekano wa uume, imesheheni madini ya potassium, magbesium, Vitamini B ambavyo huongeza nguvu za kiume/ tendo la ndoa.
6) Mbegu za matunda kama vile tikiti maji, ubuyu, maboga, alizeti, nk pia karanga. Hizi pia huongeza nguvu za kiume. Na kwa huwa na madini ya zinc, mwili huzalisha mbegu za kiume nyingi.
7) Viazi vitamu: vina vitamini A ambayo husaidia mwanake kulinda umbile la k... na mfuko wa kizazi, na huzalisha homone za kike.
8) Samaki: mafuta yaliyomo kwenye samaki (omega -3) ni muhimu sana kwa nguvu za kiume/ tendo la ndoa.
9) Parachichi: lina umbo la mwili wa kike na lina vitamini B6 na madini ya potassium, muhimu kwa kuongeza nguvu za kiume/ tendo la ndoa.
10) Tikitimaji: pamoja kutumika mbadala wa maji, husaidia kulegeza mishipa ya damu hivyo kurahisisha mzunguko wa damu mwilini na hatimaye nguvu za kiume/tendo la ndoa.