Matumizi na uhifadhi sahihi wa silaha kwa wamiliki Tanzania

Matumizi na uhifadhi sahihi wa silaha kwa wamiliki Tanzania

Mbute na chai

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2012
Posts
564
Reaction score
593
Nimeshawishika kushiriki maarifa haya baada ya kuwepo kwa taarifa za matumizi na uhifadhi mbaya wa silaha hasa kwa raia.

Kila mtu Tanzania anayo haki ya kumiliki silaha kwa matumizi binafsi kama vile ulinzi binafsi, kuwinda n.k. Leo sitaongelea namna ya upatikanaji wa haki hii bali vitu vya kuzingatia ili waliyopata haki hii wasije wakajikuta wanaijutia.

1. KANUNI ZA USALAMA WA SILAHA YA MOTO (FIREARM SAFETY RULES).

A
. Kila silaha huwa ipo tayari kupiga hadi utakapojiridhisha vinginevyo. Dhana hii ikikukaa akilini kamwe hautaweka mzaa kwenye silaha. Hivyo, unaposhika silaha, ikague na jiridhishe kuwa iko salama.

B. Kila unaposhika silaha elekeza mtutu mahali salama ambapo hata risasi ikitoka kwa bahati mbaya haitaleta madhara kwa binadamu, wanyama na mali. Fanya hivi hata kama silaha haina risasi. Ukiwa na mazoea haya kamwe hautadhuru mtu au kitu kwa bahati mbaya.

C. Unaposhika silaha usiguse, kwa namna yoyote, kitufe cha kufyatulia (finger off the trigger) hadi pale utakapokuwa tayari kupiga. Fanya hivi hata kama silaha haina risasi. Madhara ya bahati mbaya mara nyingi huusishwa na ubonyezaji wa kitufe cha kufyatulia kwa bahati mbaya.

D. Unapokuwa tayari kupiga hakikisha nini kipo nyuma ya mtu au kitu unachotaka kukipiga. Baadhi ya risasi kama vile full metal jacket (FMJ) huweza kupenya na kutokea upande wa pili hivyo kudhuru kilichopo nyuma ya kilengwa.

E. Unapohifadhi risasi zako hakikisha kileta madhara (bullet) kinaangalia chini. Risasi (cartridge/round) ni mjumuiko wa vitu vitatu; kilipuzi (primer), kilipuka kilicho ndani ya ganda ( casing) (explosive powder) na kileta madhara (bullet). kilipuzi hugongwa na pini ya kufyatulia na huwasha moto unaopelekea kilipuka kulipuka na kuondosha kileta madhara kwa kasi isiyoonekana kwa macho. Hivyo, unapohifadhi risasi huku kileta madhara kikielekea chini utaepuka mdhara ya tokanayo na risasi kulipuka kwa namna yoyote ile.

F. Unapohifadhi silaha yako, hakikisha unaiacha kwenye hali ambayo haiwezi kutumika kwa haraka (incapable of immediate use). Hivyo, hakikisha unatenganisha risasi na silaha. Mfano; kijana aliyechukua silaha ya baba yake kilimanjaro (taarifa ya zamani kidogo) na kujiua asingeweza kufanya hivyo kama mmiliki wa sila hiyo angezingatia kanuni hii.

LEO TUKOMEE HAPA. ANDIKO JINGINE LITAHUSU UHIFADHI NA MATUMIZI SAHII.
 
Mimi ghetto paa lina vitobo tobo. Yani nikisikia mkwaruzo wowote kwenye bati nalala chalii na kunyoosha mkono na kufyatua vitu vyenye ncha kali na butu vinavyoruka hewani kwa kasi ya ajabu. Kitu kinakooa pah pah pah.

Mzungu hajakariri kasoma na kuelewa!
 
HABARI WANAJAMVINI
Leo ninazungumzia matumizi ya silaha, kwa raia, kwa mujibu wa sheria.

ULINZI BINAFSI (SELF DEFENSE)
Hapa ninamaanisha uhai wako, wapendwa wako (loved ones) na mali. Ni kosa kumtishia mtu kwa kutumia silaha. Silaha hutumika pale tu unapojiridhisha kuwa bila kuitumia, maisha yako au ya wapendwa wako na mali uliyonayo vitadhurika.

Hivyo, unavyotoa silaha yako kwenye maficho (concealed carriage) lazima uitumie. Hauitoi kwa ajili ya maonesho au kwa sababu tu mtu amekuhudhi. Hii ina maana kuwa unapaswa kutathmini mazingira yanayokukabili na kujiridhisha kuwa uhai wako na wapendwa wako au mali yako iko hatarini. Mali lazima iwe na thamani kubwa kidogo, siyo mtu kakwapua simu ya elf 30 unaondoa uhai wake. Hii itakuwa matumizi ya nguvu kupitiliza.

Mtakubaliana na mimi kuwa mazingira yatakayokufanya kutoa na kutumia silaha ni machache sana. Hii husababisha wamiliki wengi kutotumia silaha zao kwa muda mrefu na hata kujitafakari kama kweli walikuwa na sababu ya kuomba na kupewa kibali cha kumiliki silaha.

Hakuna sabubu ya raia mwenye kibali cha kumiliki silaha kumudu dhana ya ulengaji shabaha (art of marksmanship). waarifu wengi, ukiondoa magaidi, wanapokutana na mtu mwenye silaha huwa wanajitahidi sana kutopata majeraha ya risasi. Jambazi anapojeruhiwa na risasi hasa eneo la kichwa na kiwiliwili (torso/trunk) huwa mara nyingi anaenda kufa. Hawezi kwenda hospitali kwani anahofia kukamatwa hivyo huishia kwa waganga wa kienyeji au watabibu wasiyo zingatia kanuni na maadili ya utabibu.

Kwa sababu tajwa hapo juu, jambazi, anapokutana na mtu mwenye silaha huwa anajibu mapigo kwa minajili ya kupata upenyo wa kuondoka eneo hilo na siyo kushinda hiyo vita ya kurushiana risasi. Hata kama ana AK47 rifle. Polisi wanapokabiliana na majambazi yenye silaha huwa wanafanya uzingiro (sieged ambush) kiasi kwamba majambazi yanakuwa hayana exit point. Hivyo, uheri wao unakuwa ni kuweka silaha chini na kujisalimisha au kupambana hadi wapate forced exit point. Hapa ndiyo wengi huuawa.

Kwa sababu zilizotajwa hapo juu, sheria yetu inaruhusu raia kumiliki silaha nyepesi kama pisto, shotgun na rifle za kuwindia tu. Raia hahitaji silaha nzito kwani kamwe hatakutana na jambazi ambaye atageuza makutano yao kuwa uwanja wa vita. Kuhusu magaidi, hakuna raia anayeweza kudhibiti gaidi hata kama raia huyo anayo silaha nzito. Magaidi ni watu wenye mafunzo ya kijeshi.

Hivyo, unapovamiwa, kupiga risasi hewani (warning shots) inatosha kuondoa hatari inayokukabili.

TUTAENDELEA………….
Nakufuatilia kwa ukaribu sana endelea kututoa ujinga
 
Ukifika kwenye umiliki elezea kwa kina ni kheri uandike siku nzima lakini tupate kitu.
 
Back
Top Bottom