Matumizi sahihi ya taa za gari.

Kuna road ambazo katikati n mstari wa njano pembeni ndo white hapo ni vepeeee
 
kuna indicator ya kulia,licha ya kuwa inakuonyesha kukata au kutokumruhusu aliyeko nyuma asiku overtake lakini pia inatumika kumtahadharisha dereva unayepishana nae muda wa usiku ajue upana wa gari yako ulipoishia ili mpishane vizuri..! Nawasilisha
 
Wengi mnaonyesha mmepata licence za kununuaa humu ndani sasa asante nyingi za nini na nyinyi mmepitia driving school??ndio maana watu mnaendesha bila mpangilio barabarani na kuwasha full beam full beam hamjui hata kazi yake


Hizo full beam zinatumia hasaa kukiwa na fog kwenye nchi kama uingereza sasa huku mtu utamkuta anaendesha gari lake na full beam mpaka mnaboa
 
Mstari mmoja wa njano unaruhusiwa kusimama bali mistari miwili ya njano ndio huruhusiwi kusimama muda wowote

Hiyo mistari miwili ya njano au mmoja ipo wapi hapa bongo au????
 
Wakuu nitawawekea Traffic Signs Regulations and General Directions (TSRGD) ambayo Wingereza wanatumia. Just stay tuned.
 

Wacha uongo.
 

Nitarudi
 
Ahsante kwa somo lenye manufaa zaidi kuliko kila wakati ngono ngono ngono ...
 
Kuna uhusiano gani wa kuwasha hazard katika makutano ya barabara kama unataka kunyoosha.
 
Wakuu sheria na alama za barabarani ni pdf (Traffic Signs Regulations and General Directions (TSRGD) document ndefu kidogo, UK walikuwa wanatumia hii wamechapisha mpya hivi sasa current ni 2006. Ninayoweka ni 2002 ambayo imefanyiwa marekebisho madogomadogo ili kwenda na wakati.
 

Attachments


Achana na mambo ya kucopy na ku paste bana me naongea kutokana na halisi ya mambo maana hiyo pdf ni tofauti na sheria za bongo umeona mataa ya bongo yanavyofanya kazi umeona ni sawa na UK??so ongea vitu ambavyo unajuwa na sio kukurupuka....
 
ni ishara ya kuwa hukati kulia wala kushoto bali unanyoosha tu

*SWALI: JE NIWASHE HAZARDS NINAPOKATIKA KWENYE MAKUTANO YA MSALABA YASIYO NA TAA, HASA NAPOTAKA KUNYOOSHA MOJA KWA MOJA?*
BALOZI Heri Nderingo ANAJIBU.
Kwenye makutano ya barabara ukiwasha hazard unaweza kusababisha ajali kwa sababu anayetokea kulia kwako ataona indicator moja ya kulia na hivyo kudhania unaenda kulia. Hivyohivyo kwa aliye kushoto kwako. Sasa imagine unatokea St. Peters unaekea International School of Tanganyika halafu ukifika njia panda ya Chole ukawasha hazard. Anayetokea coco beach atafikiri unaenda coco beach na anayetokea slipway atafikiri unaingia chole kuelekea slipway. Hapo vumbi litatimka.
Kimsingi gari linalotembea bila kuwasha indicator inakuwa assumed linaenda moja kwa moja, otherwise tungekuwa tunawasha hazard throughout.
Hazard inatumika wakati wa dharura ili ku attract attention ya watumiaji wengine wa barabara. I stand to be corrected.
HIVYO JIBU NI USIWASHE HAZARDS, PITA MOJA KWA MOJA.
 
kwaio mkuu ukiwasha taa mchana kama sio msafara maalum ni kosa? mana mi napenda kuwasha mchana wakati nikiwa mwendo wa kasi kidogo na wala sio msafara maalum. nauliza kwa sababu siku moja askari alitaka kunihukumu kwa kuwasha taa mchana nkamwambia nimesahau kama zipo on 😀
 
watu wengi washashindwa kutumia taa hasa hawa wa masemi highways kama wanawinda digidigi,nami nimefunga li watts 120 mwanga mweupe kama hujui kutumia taa zako nakustua nalo,mwenyewe utanywea maana linakuziba kabisa!kuna watu ye all time yupo full bora umewafundisha
 
Kwa kuongezea, kwa nyakati za usiku inatumika kumshtua dereva wa gari ya mbele yako abadili high beam to low beam ili mpishane kwa usalama
 
Hii nayo ipo katika tahadhari lakin kwa makundi maalumu kama vile misafara ya misiba ya kijeshi na misafara mingine maalumu.
Nitakuwa nje kidogo ya mada lakini ni katika masuala mazima ya barabarani.

Naulizia mistari ya barabarani ya katikati.

1)Kuna sehemu za barabara ukipita unakuta mstari umepigwa mmoja lakini ukienda mbele inakuta ipo miwili. Hapo inaashiria nini?

2)Pia,katikati ya barabara kuna sehemu mistari yake ni dash-line style upande mmoja mf.kulia na kushoto ni mstari wa moja kwa moja then kwa mbele unakuta ule uliokuwa dash-line kulia umewekwa kushoto tena na mstari wa moja kwa moja upo kulia. Hii maana yake nini?

3)Sehemu mistari yake ni dash-line tu inamaanisha nini? Ukiwa mmoja au miwili.
 
Ndo zimepigwa marufuku hizo taa zako, sasa sijui utawashtua na nini labda uweke chemli sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…