Matumizi sahihi ya taa za gari.

Matumizi sahihi ya taa za gari.

Kuna road ambazo katikati n mstari wa njano pembeni ndo white hapo ni vepeeee
 
kuna indicator ya kulia,licha ya kuwa inakuonyesha kukata au kutokumruhusu aliyeko nyuma asiku overtake lakini pia inatumika kumtahadharisha dereva unayepishana nae muda wa usiku ajue upana wa gari yako ulipoishia ili mpishane vizuri..! Nawasilisha
 
Wengi mnaonyesha mmepata licence za kununuaa humu ndani sasa asante nyingi za nini na nyinyi mmepitia driving school??ndio maana watu mnaendesha bila mpangilio barabarani na kuwasha full beam full beam hamjui hata kazi yake


Hizo full beam zinatumia hasaa kukiwa na fog kwenye nchi kama uingereza sasa huku mtu utamkuta anaendesha gari lake na full beam mpaka mnaboa
 
Mstari mmoja wa njano unaruhusiwa kusimama bali mistari miwili ya njano ndio huruhusiwi kusimama muda wowote

Hiyo mistari miwili ya njano au mmoja ipo wapi hapa bongo au????
 
Wakuu nitawawekea Traffic Signs Regulations and General Directions (TSRGD) ambayo Wingereza wanatumia. Just stay tuned.
 
Wengi mnaonyesha mmepata licence za kununuaa humu ndani sasa asante nyingi za nini na nyinyi mmepitia driving school??ndio maana watu mnaendesha bila mpangilio barabarani na kuwasha full beam full beam hamjui hata kazi yake


Hizo full beam zinatumia hasaa kukiwa na fog kwenye nchi kama uingereza sasa huku mtu utamkuta anaendesha gari lake na full beam mpaka mnaboa

Wacha uongo.
 
Habari zenu wana jamvi...Mi napenda sana usalama barabarani....huwa naumia sana nikisikia ajali ambayo imetokana na uzembe au kutofuata sheria za barabarani....Haya ni matumizi ya taa za gari yakiyowekwa kisheria.

Tuanze na taa za mbele ya gari ambazo kimsingi zinatakiwa ziwepo taa za aina tatu....
1..>>>>>Taa kubwa za mbele ambazo hutumika kuanzia giza linapoanza kuingia mpaka giza linapoisha asubuhi pamoja na sehemu zenye tunnel na nyakati za ukungu au mvua..Taa mbili hizi kwa haraka unaweza ukasema zina matumizi sawa lakini kila taa ina kazi yake...yaani taa ya kulia ina kazi yake na ya kushoto pia....Taa ya kulia ambapo ndio upande wa dereva kazi yake ni kumulika kuanzia mstari mweupe wa katikati ya barabara kuelekea kushoto ili kumrahisishia dereva unaepishana nae asipate shida sana wakati mnapishana....na taa ya kushoto kazi yake ni kumulika kuanzia mstari wa njano kuelekea kushoto ili iwe rahisi kuwaona waendesha vyombo vya baridi na watembea kwa miguu......taa kubwa zina low beam(mwanga usiomulika mbali) na high beam ( mwanga unaomulika mbali)....matumiz ya low beam kisheria ni pale .....
@unapopita katika barabara yenye taa (taa za barabarani hasa mjini) .....
@unapopishana na gari nyingine ni lazima na sio ombi kutumia low beam.....
@unapotaka kulipita gari la mbele yako (over take) ni lazima kutumia low beam kabla hujaanza kulipita gari hilo....endapo utatumia high beam wakati wa kuover take basi mwanga wa taa zako utapiga moja kwa moja katika kioo cha cha gar ya mbele ( side mirror) then mwanga ule utakuwa reflected kwa dereva unaetaka kumpita na kumsababishia kuanza kuyumba na hatimaye unaweza ukakosa njia nzuri ya kumpita.

2. Kuna taa za kuegeshea gari ( parking light) ambazo hutumika ukiwa umepaka gari lako pembeni ya barabara nyakati za usiku ili liweze kuoneka kirahisi. Ni muhimu sana taa hizi.

3. Taa za kuonesha uelekeo yaani indicators lights...hiz ni taa ambazo kisheria zinatakiwa ziwe mbili mbele ya gari yako..yaani kulia na kushoto....utawasha ya kulia kuonesha unaingia kulia na kushoto kuonesha unaingia kushoto angalau mita 30 kabla ya kufanya kitendo hicho..... Taa hiz zinaweza kutumika pia wakati ukivunja sheria kwa kuziwasha zote mbili kwa wakati mmoja yaani HAZARD ukionesha kuwa gari yako inaweza kusababisha maafa au ajali hivyo basi watumiaji wengine kuwa makini au na tahadhari dhidi ya gari yako...kuna aina tatu ya uvunjaji wa sheria kwa kutumia HAZARD.....
Moja..kama gari yako ipo kwenye mwendo wa kasi kuliko mwendo ulioainishwa katika eneo husika( labda ni eneo la mjini mwisho 50 kmh lakin wew una dharula ya mgonjwa unamuwaisha itabidi utumie HAZARD.....
pili...kama unaenda kwa mwendo wa polepole sana kiasi ambacho unaweza kusababisha ajali...mfano njia za nje ya mji magari huwa yakienda kwa mwendo wa kasi...hivyo basi kama gari ina tatizo labda imeshindwa kuingiza gia zaid ya namba moja na kukulazimu kutembea mwendo wa gia moja ni lazima uwashe HAZARD.
Tatu...kama gari yako imeharibika barabarani na sehemu hiyo huruhusiwi kuegesha gari...mfano barabara zote ambazo zina mstari wa njano pembeni huruhisi kusimama bali unatakiwa uendelee mbele tu. Ukipata tatizo katika maeneo haya basi utavunja sheria ya kutokusimama kwa kuwasha HAZARD pamoja na kuweka vibao vya tahadhari.(triangles)

Uzi huu ni kwa ajili ya taa za mbele tu....nitaandaa uzi mwingine kwa ajili ya taa za nyuma ambazo jumla yake zipo sita...ni vyema ukajua matumizi yake kuepuka/kuepusha ajali na mambo mengine. Aksante kwa kusoma.

Nitarudi
 
Ahsante kwa somo lenye manufaa zaidi kuliko kila wakati ngono ngono ngono ...
 
Kuna uhusiano gani wa kuwasha hazard katika makutano ya barabara kama unataka kunyoosha.
 
Wakuu sheria na alama za barabarani ni pdf (Traffic Signs Regulations and General Directions (TSRGD) document ndefu kidogo, UK walikuwa wanatumia hii wamechapisha mpya hivi sasa current ni 2006. Ninayoweka ni 2002 ambayo imefanyiwa marekebisho madogomadogo ili kwenda na wakati.
 

Attachments

Wakuu sheria na alama za barabarani ni pdf (Traffic Signs Regulations and General Directions (TSRGD) document ndefu kidogo, UK walikuwa wanatumia hii wamechapisha mpya hivi sasa current ni 2006. Ninayoweka ni 2002 ambayo imefanyiwa marekebisho madogomadogo ili kwenda na wakati.

Achana na mambo ya kucopy na ku paste bana me naongea kutokana na halisi ya mambo maana hiyo pdf ni tofauti na sheria za bongo umeona mataa ya bongo yanavyofanya kazi umeona ni sawa na UK??so ongea vitu ambavyo unajuwa na sio kukurupuka....
 
ni ishara ya kuwa hukati kulia wala kushoto bali unanyoosha tu

*SWALI: JE NIWASHE HAZARDS NINAPOKATIKA KWENYE MAKUTANO YA MSALABA YASIYO NA TAA, HASA NAPOTAKA KUNYOOSHA MOJA KWA MOJA?*
BALOZI Heri Nderingo ANAJIBU.
Kwenye makutano ya barabara ukiwasha hazard unaweza kusababisha ajali kwa sababu anayetokea kulia kwako ataona indicator moja ya kulia na hivyo kudhania unaenda kulia. Hivyohivyo kwa aliye kushoto kwako. Sasa imagine unatokea St. Peters unaekea International School of Tanganyika halafu ukifika njia panda ya Chole ukawasha hazard. Anayetokea coco beach atafikiri unaenda coco beach na anayetokea slipway atafikiri unaingia chole kuelekea slipway. Hapo vumbi litatimka.
Kimsingi gari linalotembea bila kuwasha indicator inakuwa assumed linaenda moja kwa moja, otherwise tungekuwa tunawasha hazard throughout.
Hazard inatumika wakati wa dharura ili ku attract attention ya watumiaji wengine wa barabara. I stand to be corrected.
HIVYO JIBU NI USIWASHE HAZARDS, PITA MOJA KWA MOJA.
 
kwaio mkuu ukiwasha taa mchana kama sio msafara maalum ni kosa? mana mi napenda kuwasha mchana wakati nikiwa mwendo wa kasi kidogo na wala sio msafara maalum. nauliza kwa sababu siku moja askari alitaka kunihukumu kwa kuwasha taa mchana nkamwambia nimesahau kama zipo on 😀
 
watu wengi washashindwa kutumia taa hasa hawa wa masemi highways kama wanawinda digidigi,nami nimefunga li watts 120 mwanga mweupe kama hujui kutumia taa zako nakustua nalo,mwenyewe utanywea maana linakuziba kabisa!kuna watu ye all time yupo full bora umewafundisha
 
Ni mojawapo ya ishara ambazo madereva huzitumia.....japokuwa sio rasmi sana.

1. Inaweza ikawa salamu
2. lakini taa zinaongea...kwa mfano unaweza ukawasha hivyo ukimaanisha unamruhusu mtumiaji mwingine wa barabara aendelee kwenda au apite au asubiri kwanza wew upite lakini pia unaweza kuziwasha hivyo kumuomba dereva mwenzako akuruhusu kupita kwanza.

Kwa kifupi inategemea na eneo au na wakati....kwa mfano mmi huwa nafanya hivyo nikiona gari ya mbele yangu ipo mwendo wa taratibu sana hasa mjini unakuta mtu anapiga story au anachezea simu....unaweza ukamshtua kwa kupiga honi au ukawasha taa(high beam) kumshtua.

Kwahiyo inategemea unataka kumaanisha nin na madereva wazoefu watakuelewa tu.
Kwa kuongezea, kwa nyakati za usiku inatumika kumshtua dereva wa gari ya mbele yako abadili high beam to low beam ili mpishane kwa usalama
 
Hii nayo ipo katika tahadhari lakin kwa makundi maalumu kama vile misafara ya misiba ya kijeshi na misafara mingine maalumu.
Nitakuwa nje kidogo ya mada lakini ni katika masuala mazima ya barabarani.

Naulizia mistari ya barabarani ya katikati.

1)Kuna sehemu za barabara ukipita unakuta mstari umepigwa mmoja lakini ukienda mbele inakuta ipo miwili. Hapo inaashiria nini?

2)Pia,katikati ya barabara kuna sehemu mistari yake ni dash-line style upande mmoja mf.kulia na kushoto ni mstari wa moja kwa moja then kwa mbele unakuta ule uliokuwa dash-line kulia umewekwa kushoto tena na mstari wa moja kwa moja upo kulia. Hii maana yake nini?

3)Sehemu mistari yake ni dash-line tu inamaanisha nini? Ukiwa mmoja au miwili.
 
watu wengi washashindwa kutumia taa hasa hawa wa masemi highways kama wanawinda digidigi,nami nimefunga li watts 120 mwanga mweupe kama hujui kutumia taa zako nakustua nalo,mwenyewe utanywea maana linakuziba kabisa!kuna watu ye all time yupo full bora umewafundisha
Ndo zimepigwa marufuku hizo taa zako, sasa sijui utawashtua na nini labda uweke chemli sasa
 
Back
Top Bottom