Matumizi ya akili unde katika huduma za ultrasound kuboresha afya ya mama na mtoto

Matumizi ya akili unde katika huduma za ultrasound kuboresha afya ya mama na mtoto

University of Dodoma (UDOM)

Public Institution
Joined
Feb 24, 2024
Posts
50
Reaction score
55
WhatsApp Image 2026-06-16 at 08.16.11 (2).jpeg

Mwongozo wa matumizi ya teknolojia ya akili unde (Artificial Intelligence – AI) katika huduma za utra sound kwa afya ya mama na mtoto unatarajiwa kuwa suluhisho muhimu katika kuboresha ubora na upatikanaji wa huduma za afya nchini Tanzania.

Mwongozo huo unaandaliwa kwa lengo la kuweka viwango vya kitaalamu vitakavyowaongoza wahudumu wa afya katika ngazi mbalimbali, kuanzia hospitali za rufaa hadi zahanati, ili kuhakikisha huduma za utra sound zinatolewa kwa usahihi, ubora na kwa wakati unaofaa.

WhatsApp Image 2026-06-16 at 08.16.11.jpeg

Akizungumza mjini Morogoro katika kikao kazi cha wataalamu wa afya kinachojadili maandalizi ya mwongozo huo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Profesa Lughano Kusiluka, amesema mradi huo unalenga kutumia teknolojia ya akili unde kuboresha uchunguzi wa utrasound kwa wajawazito na kusaidia kugundua mapema changamoto zinazoweza kuhatarisha afya ya mama na mtoto.

Profesa Kusiluka amesema matumizi ya teknolojia hiyo yataongeza ufanisi wa huduma za afya, hususan katika maeneo yenye upungufu wa wataalamu wa mionzi na uchunguzi wa ultrasound.

Aidha, amesema mradi huo umetokana na tafiti zilizofanywa na Chuo Kikuu cha Dodoma zenye lengo la kuboresha huduma za afya ya uzazi kupitia matumizi ya teknolojia ya kisasa, hatua ambayo itarahisisha utoaji wa huduma pamoja na kuongeza usahihi wa vipimo.

WhatsApp Image 2026-06-16 at 08.16.10 (1).jpeg

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afya ya Mama na Mtoto kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Mzee Nassoro, amesema mwongozo huo utaendana na sera na miongozo ya kitaifa inayohimiza wajawazito kufanyiwa uchunguzi wa ultrasound angalau mara moja katika kipindi cha ujauzito.

Dkt. Nassoro ameongeza kuwa matumizi ya akili unde katika huduma za afya yatasaidia kupunguza changamoto ya uhaba wa wataalamu pamoja na kuimarisha huduma katika vituo vya afya vya pembezoni.

Amesema kukamilika kwa mwongozo huo kutachangia kuimarika kwa huduma za afya ya mama na mtoto, kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika, na kuboresha kwa ujumla mfumo wa huduma za afya nchini Tanzania.
 
Back
Top Bottom