Matumizi ya chumvi kuondoa mikosi

Matumizi ya chumvi kuondoa mikosi

Heshima kwenu wakuu.

Kuna hii dhana ya matumizi ya chumvi kuondoa mikosi katika maisha, hivi hii kitu ni kweli na inafanyaje kazi.niliona sehemu watu wakitoa ushuhuda kuhusu wao kuchoma chumvi na ikawatendea kama vile walivotamani iwe.

Nawasilisha na natamani kujua kama ni kwel.
Enzi za nabii Eliya,kuliwahi kutokea shida ya Wanawake kupata ujauzito na kutoka (Miscarriage/Contagious abortion),Nabii Eliya aliweka chumvi ktk visima walivyochota maji na tatizo hilo likaisha kabisa,kwa hiyo itakuwa ni kweli.
 
Hii hapana, kama unamuamini Yesu usiwaambie watu damu ya mnyama inapatanisha ukoo,

Soma Bible agano la kale kwa misingi ya aga jipya ukisoma kwa mtindo huo Bible itakupoteza mno,

Lazima uwe na macho ya ndani

Tofauti ya mila na desturi unazo sema jiulize swali
Kwa nguvu ipi wanaitumia ili kupata vyote hivyo

Kuna vitu viwili vinavyo tumika
Ukikosa kumtumia Mungu basi upo kwa shetani

Ndio maana siku hiz hatumwagi damu ya wanyama kuwasailiana na Mungu kama zamani na hii ndio ambayo ufalme wa giza wameweza kuiga na baba yao shetani

Sisi tunao amini tunatumia damu ya Yesu hii shetani kashindwa ku I copy

Sasa hiv tupo chini ya neema si chini ya sheria

Mwenye ukoma aliye ambiwa kaoge alikuwa naamani wakati wa agano la akale

Hawa wa agano jipya tofauti na naamani alicho ambiwa
Naamani

Kuna mila haziendani na neno la Mungu tena nyingi tu, ndani yake kuna nguvu za giza zimejificha,

Chumvi inatumika kwa upande wa Mungu sikatai kabisa hata mimi nikitaka kufanya kitu nikihitaji chumvi natumia kwa Neno la Mungu na naweka ktk matendo

Sababu wakati mwingine bila matendo imani imekufa, naweza kutamka au kuchukua kitendo husika
Mungu akulinde
Mkuu DIVINE naomba msaada hapa.

Kwa mfano nikawa naitumia lakini manuizi yangu yakahusisha Mwenyezi Mungu ''mfano nikasema ee Mwenyezi Mungu ninakuomba kwa kupitia chumvi hii unibarikie na uniondolee mikosi yote na baraka zifunguke kwangu, kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti naomba na kuamini. Amina''. Halafu nikaendelea kuyaoga hayo maji yenye chumvi

Je hapa nitakua nimetenda dhambi kwa kutumia chumvi?
 
KRISTO YESU alifundisha kwenye kitabu cha Mathayo 5:13 akisema, ninyi ni chumvi ya dunia.
Tena akasema kwenye, Marko 9:49-50 kwamba kila mtu atatiwa chumvi kwa Moto.
Akasema, chumvi ni njema, muwe na chumvi ndani yenu, mkakae kwa amani ninyi kwa ninyi.
Alafu akarudia tena kwenye kitabu cha Luka 14:34 akasema , Chumvi ni kitu chema.
Tena Hesabu 18:19
Lawi 2:13

Lakini kufanya toba na kusamehee ni muhimu .

Sent from my KIW-L24 using JamiiForums mobile app
Ahsante sana.
 
Hata hii kila anayefungua nawaangalia tu cz ndio njia yangu ya home, akifungua mtu hapo hamalizi miez miwili anakuwa kafunga,
Sikuomba siku moja nilikuwa napita namwaga kidogo tu, hapo nahakikisha home nimeombea kwa mistari ya kutosha na damu ya Yesu ya kutosha na nimejiwekea ulinzi kabla sijaenda cz sio kila kona unavamia.
Ahsante kwa ushuhuda mkuu
 
Dawa zipo na wala siyo kila dawa ni uchawi ama ushirikina. Kama ni hivyo basi nabii Elisha alipoyatibu Yale maji kwa chumvi alifanya ushirikina?! Hapana.

Mfano mwingine ni ule wa Kuponywa kwa binti Sara mchumba wa Tobia. (Biblia takatifu kitabu cha TOBITI 6: 17).

Tunaona jinsi malaika Rafael anavyomwongoza Tobia juu ya namna ya kumwondoa jini mbaya aliyemsumbua Sara kwa miaka kadhaa. Kwa kuchoma ubani na kisha kuweka vipande vya ini vya samaki kisha yule jini akaskia harufu ile akakimbia na wala hakurudi tena.

Tunajifunza kwamba; kwanza siyo kwamba Mungu au yule malaika (Rafael) alishindwa kumfukuzia mbali jini Bali kusudio ni kumwambia mwanadamu kuwa solutions za mambo mengi anazo hapahapa katika nchi.

Pili, Jinsi dunia ilivyoumbwa iko very balanced. Ndiyo maana Baada ya uumbaji biblia inasema :" Basi mbingu na nchi zikakamilika". (Mwanzo 2:1). Huko kukamilika maana yake ni kuwa ndani ya nchi kuna kila kitu kwa ajiri maisha yote ya Mwanadamu. E.g kama kuna kutiwa nuksi basi kuna njia za kinyume chake. Namna ya kuondoa nuksi.

Sasa kama kumtia MTU nuksi ni dhambi na kuondoa nuksi ni dhambi, ni lipi lenye kumpendeza Bwana Mungu?!

Tunafahamu Mungu anao uwezo mkuu. Angeweza kuyatibu Yale maji kwa kusema tu bila kuweka chumvi kwa mkono wa Elisha au angeweza kumponya binti Sara (Tobiti 6:17) vile vile pasipo hivyo vitu vya kidunia. Sasa kwa nini avitumie? Yule jini hakutaka Sara aolewe ndiyo maana akawa anaua kila mwanaume aliyemsogelea Sara. Kwa maneno mengine Sara alikuwa na nuksi!

Ndiyo kusema kwamba hayo yote Mungu anayafanya ili kutwambia kuwa solutions za mambo mengi tunayo hapahapa katika nchi.

Shida ni ufahamu wetu tu mdogo. Ndiyo maana akaongeza kusema kuwa :" WATU WANGU WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA". Unadhani ni maarifa yapi?!

Tatizo ni kwamba tulio wengi kama hatujui kitu Fulani basi hicho siyo cha kweli. Na tunadhani kwamba maarifa tuliyonayo ndiyo ukomo wa maarifa kwa watu wote.

Find knowledge usidhani umeimaliza dunia.

- JODEO-
Kuna logic hapa🙏
 
Mkuu DIVINE naomba msaada hapa.

Kwa mfano nikawa naitumia lakini manuizi yangu yakahusisha Mwenyezi Mungu ''mfano nikasema ee Mwenyezi Mungu ninakuomba kwa kupitia chumvi hii unibarikie na uniondolee mikosi yote na baraka zifunguke kwangu, kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti naomba na kuamini. Amina''. Halafu nikaendelea kuyaoga hayo maji yenye chumvi

Je hapa nitakua nimetenda dhambi kwa kutumia chumvi?
Hiyo ndiyo yenyewe haswaa! Na ndio tiba haswaa chumvi haina shida na yesu au mungu ila ina shida sana na shetani na mawakala wake hao ndio hawapatani na chumvi kabisaa
 
Kanisa Katoliki tunatumia chumvi na kuchanganya na maji...Mchanganyiko huo unabarikiwa kwa kutamka sala maalum..Tukitumia rehea ya maandiko pale Elisha alipochanganya maji na chumvi na kuponya miscariage na pooza...

Haya ndio tunaita maji ya Baraka.....Ni karne na karne Ritual hii ilifanyika mpaka leo
Hata KKKT hutumia chumvi na maji
 
Back
Top Bottom