Matumizi ya connect za Upwork

Lee Swagger

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2018
Posts
1,063
Reaction score
1,815
Kwa Wale wapambanaji Wenzangu wa Mitandaoni nikiongelea Upwork nafkiri sio Kitu Kigeni. Kwa Wale Ambao Hawafahamu kuhusu Fursa za Upwork fuatlia Uzi Mbali mbali upate Mwanga.

Moja Kwa Moja Kuna Zile Connect za Kuombea Kazi kule Upwork, Kuna ambazo ni za Bure Kila Mwezi Na Kuna Zile Zinauzwa Kwa Bundle.

Mimi Sio mzoefu Sana Kwenye Upwork ndio Kwanza Nimejiunga, nimepokea invitation moja ya Kazi. Sasa huyu bwana ameniambia tutafanya kikao, kama navutiwa Kufanya Kazi, Haya Mimi nikamwambia Nipo Available. Akapotea Baada ya Siku Mbili Mimi Hata Sikumcheki. Akarudi akaniuliza mbona Kimya Kuhusu Kikao/meeting. Sasa Ndugu Zangu Hapa Mimi nikashindwa Kuelewa Nani anatakiwa Amcheki Mwenzake. Na Hivi Vikao/Meeting Inakuaje Wazoefu Mnipange. Kama Nimezingua. Akanipanga Akasema Ijumaa Hii Ndio Atakua Na Nafasi Ya Kikao. Na Mimi Nikamwambia Fresh Mimi nipo Tu.

Swala lingine: Je Hizi Bando za Upwork ninunue au nipambane na Zile Za Bure Tu?

Swala Lingine: Kitufe Cha Availability kuwaka pale mabayo Inatumia 6 connect Kwa wiki Je Yafaa kuiweka Hyo Huduma Au ni kiherehere. Kwasababu Mimi ni Beginner naa Nataka nIpate Wateja/clients Kwa Namna yoyote kama Waliofanikiwa wanavyofanya Kwenye hyo Platform.

Swala Lingine: Nimeona Unaweza Kupata Kazi hapa Upwork alafu ukaenda Kuipeleka Fiver Kutafuta mtu mwingine aifanye Kwa Kukosaa Muda, Swala linakuja Kule Fivver wakati unaingia Contract na Muuzaji/seller inapaswa Hela Ulipe Kabisa, Hela ikae Kwenye Escrow. Sasa kwa Kazi ya $1000 hii Utafanyaje Au Inabidi Uwe na Kamtaji Pembeni Cha kumaliza Hizi Dili Kule Fivver. Hapa Wenzangu Mnafanyaje, Kwasababu kuendana na Fani yangu Kuna Kazi Mpka Za $1500.

Swala Lingine: Kwenye Portfolio Yangu Kuna Projects zaidi Ya 60 ambazo Nimeweka Na Nimezifanya Mimi. Na Nina uzoefu wa Muda mrefu Nimeweka Rate ya $35/hr ambapo Ukitoa Commission nachukua $28/hr. Na Hii Nimeweka baada ya Kufanya Tafiti Za Wadau Wengine Wenye Fani Kama Yangu alafu nikashusha Bei Kidogo.

Swala Lingine: Kitu Gani Cha Kuzingatia unapochukua Kazi Upwork na Kwenda Kuiuza Fivver.

Naomba Michango YENU Wadau.
 
Kuelewa Nani anatakiwa Amcheki Mwenzake
Yeye ndiye akucheki, kama ni 'reputable employer', unaweza kumkumbusha ni wa nchi gani? kama ni India, Pakistan, Bangladesh, etc wengi mizinguo angalia 'reviews' zake, angalia amespend how much tangu ajiunge kuna wapigaji pia hasa ukiwa beginner kwa platform (najua unatambua hili)
 
Jana Alinicheki Akaniachia Huo Ujumbe Hiyo ni Saa 4 kibongobongo si ndio?????

 
Pitia Pia Kuna Nyuzi Zinaelimisha Huku Wadau Walishaweka. Na Mimi niligundua Hili Jambo Humu Humu nilikua Sina Habari ya Hyo UPWORK kabisa. Katika Pita Pita Zangu Nikakutana nayo.
Unafanya kwa kutumia simu janja au kompyuta?
 
Wandugu hii mada nimeipenda na nimefatilia ila sijapata mtu au uzi mzuri unaoelezea kuhusu hii platform, ningeomba ambae ameielewa vizuri anielekeze.Asanteni
 
Mrejesho: Mteja Wa Kwanza UPWORK. $150 fixed price. Kazi ya Siku 6.

Sasa Kikao cha Kwanza huko UPWORK nikawa nimejipanga na Nimeazima mpaka laptop. Alinipa Muda na Mualiko Wa Zoom Tukutane Kwa Kikao

Muda Ukawa Umekaribia PC ikaanza Ku stuck. Kuwaka. Zikapita Dakika Mbili nikaon amsg yake inbox akaniuliza Utakuja. Kwa Lugha ya Kingereza.

Pale Pale inbox Alipokua amenitumia link ya Zoom nikabonyeza Nikapanda Hewani Na Simu kwenye Hicho Kikao Zoom. Baada ya laptop Kunichelewesha. Kumbe Jamaa Hana Hata Mbili. Akanza Kunipa Maelekezo Ya Kazi Moja Kwa Moja.

Yeye mwenyewe ngeli anaunga Unga.

Akanipa Maelekezo ya Kazi anayohitaji na Muda. Akaniambia Mimi ndio atakae nipa Hyo Kazi Rasmi. Nikafurahi Sana.

Sasa Hivi Napambana na Hyo Kazi nijaribu Kufika Deadline.

Kazi ni ya fixed price.

Mimi pia Sikua Na Muda Wa Kuifanya Hyo Kazi Nimeipeleka Fivver Kuna mtaalamu Wangu Kutoka Bangladesh ataipiga. Tayari Kazi Imeanza.

Nitawapa Mrejesho nikifanikiwa Kumaliza Kazi na Kuchomoa Mpunga Wangu Wa Kwanza UPWORK..

Itaendelea...
 
Mkuu nipo apa dar waweza nielekeza kiundani au ata kukutana ikiwezekana
 
#Marejesho Kazi Mpya fixed Price $60 Kazi ya Siku 2. Aisee Hii UPWORK ni Hatari. Ndio Kwanza Sina Hata Mwezi kujiunga Mzigoni.

Hii Kazi Imetoka Mbele, Marekani.

Kwa Ambao hamfahamu Hizi Fursa za Kujiajiri Upwork Fuatlia Nyuzi za Wakuu Watangulizi Wangu.

Tuzidi Kuombeana Bado Sijadeliver Kazi Ata Moja Deadline ya Kwanza ndo Kesho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…