Mkuu naomba nipishane na wewe hapo. Kwanza mimi nilimuuliza
RRONDO kama amemaliza kisahani kwa sababu kuna uzi mmoja aliandika kuhusu top speed ya hiyo gari,na kulikuwa na mjadala kama amalize kisahani au vipi ndio maana mimi nikaamuliza,na muulizwaji mwenyewe nadhani alofahamu kwa nini nilimuuliza na akajibu vizuri sana.
Haya sasa narudi kwenye maelezo yako,kwanza kwa USA highway ambayo inaruhusu mwendo wa kasi zaidi kuliko zote kwa sasa ni I-130 iliyopo texas na speed limit ni 85mph zidisha kwa 1.6 kupata kph.Na hakuna highway ya montana inayozidi 75mph,kama nimekosea naomba tu unitajie hiyo highway. kwa USA labda uende race truck ndo unakuwa huru kupiga uwezavyo au sehemu kama Bonneville Salt flats huko Utah ndo unaweza.Kumbuka hiyo sio highway.
Ungeniambia Autobahn amabzo zipo German ndo ningekuelewa maana hazina speed limit.
hizo highway sehemu unazozisema mimi nimeshapita sana huko maana ndo makazi yangu huku kwa miaka mingi sana.