Matumizi ya Diclofenac yadhibitiwe?

Matumizi ya Diclofenac yadhibitiwe?

nyamchele

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2014
Posts
1,325
Reaction score
1,034
diclo.jpgDiclofenac-Pills.jpgdiclofenc 2.jpg
Wengi wetu tunatumia diclofenac kwa ajili ya kutuliza maumivu na kushusha homa. Dawa hii hapa Tanzania ni 'over-counter drug' au 'non prescription medicine' yaani dawa aihitaji cheti cha daktari ili anayeihitaji kupewa, ipo kama vile Paracetamol.

Kumekuwa na chunguzi mbalimbali ambazo zimeainisha madhara ya kutumia diclofenac na mojawapo ya madhara hayo ni kusababisha magonjwa ya moyo. Madhara ya ugonjwa ya moyo yanayosababishwa na dicofenac yanaonekana kuwa tishio zaidi hivyo kupelekea UK kuibadili hiyo dawa kutoka kuwa dawa isiyo hitaji cheti cha daktari (non-prescription drug) mpaka kuwa dawa inayohitaji cheti cha daktari (prescription drug) ili matumizi yake yadhibitiwe na daktari.

Ninaamini Wizara ya Afya na TFDA wanalifuatlia jambo hili kwa karibu ili hatua mahsusi zichukuliwe ikizingatiwa ya kuwa diclofenac inatumiwa kama njugu huku kwetu na ongezeko ya non-communicable diseases ikiwemo magonjwa ya moyo.

Nashauri tutumie dawa nyingine ikiwemo diclofenac baada ya kupata ushauri kutoka kwa daktari na wataalamu wengine wa afya. Wataalamu mnashaurije?
 
Back
Top Bottom