Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Nimeshindwa kuelewa niiweke wapi thread hii baada ya kusoma makala moja pale Mwanachi kuhusu mada ambayo imekuwa inakera akili yangu muda mrefu sana. Thread ingeweza kuwa siasa, uchumi au kwenye falsafa; nikaamua kuiweka hapa kwenye falsafa.
Nimekuwa na bahati sana ya kutembea na kuishi katika nchi nyingi sana duniani, ila sijawahi kufika nchi ambako biashara zote zinafanyika katika dola za kimerakni zaidi ya marekani kwenyewe. Hata Kanada ambayo ni jirani kabisa na marekani na raia wake wanafanya manunuzi yao sehemu yoyote ya mpaka, ukishavuka kuingia Canada unatumia Canadian Dollar, na ukirudi Marekani unatumia American Dollar.
Je kinachotusumbua watanzania ni ulimbukeni au kweli ni udhaifu wa sarafu yetu? Nimeangalia trends kwa muda wa miaka kumi kuhusu mabadiliko ya thamani ya sarafu mbalimbali dhidi sarafu ya kimarekani na kugundua kuwa sarafu yetu ni stable kiasi cha kutosha, kwani haijawahi kubadilika ghafla ghafla. Ingawa kuna nchi nyingine kama Kenya na South Afrika zilikuwa stable zaidi yetu lakini mabadiliko ya sarafu ya Tanzania hayajawa so alarming kiasi kuwa biashara zetu tuziendeshe kwa hela ya kigeni; nikitoka Tabora na hela yangu ya madafu siwezi kulala hoteli za maana Tanzania mpaka ninunue dola za kimarekani na kumpa faida muuzaji wa dola hizo kabla sijampa faida mtu wa hoteli, je hiyo kweli halali kwa nchi?
Chini hapo nimeweka trends zinazoonyesha jinsi sarafu mbalimbali zilivyobadilika katika kipindi cha miaka kumi iliyopita. Ingawa sarafu ya Tanzania imekuwa inapoteza thamani, upotezu huo ni kwa currency investors tu wanaoinvest kwa muda mrefu kwani hauathiri kabisa katika biashara za kila siku kwa vile thamani hiyo ilikuwa inapotea kidogo kidogo. Mabadiliko ya thamani ya sarafu ya kitanzania hayatofautiani kabisa na yale ya sarafu ya Botswana lakini mpaka kesho hutakuta Botswana wanaendesha biashara ya ndani kwa kutumia dola ya kimarekani. India vile vile mambo ni hayo hayo.
Wataalamu wa mambo ya pesa mtusaidie kwenye tatizo hio.
Sarafu ya Tanzania

Sarafu ya Kenya

Sarafu ya Afrika ya kusini

Sarafu ya India

Sarafu ya Botswana

Sarafu ya Canada

Wabunge wakerwa matumizi ya dola
![]()
Dola ya Marekani.PICHA|MAKTABA
Kwa ufupi
Matumizi ya sarafu ya Marekani yanadaiwa kuchangia kushuka kwa thamani ya sarafu ya Tanzania
Dodoma.Wabunge wameonyesha kukerwa na mtindo unaoshamiri wa matumizi ya Dola ya Marekani nchini, jambo ambalo linasababisha kuporomoka kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania.
Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya (BoT) ya mwaka 2006, imebainisha wazi kuwa shilingi ya Tanzania ndiyo fedha halali kwa malipo ya bidhaa na huduma ikiwamo hotelini, maduka makubwa na taasisi nyingine.
Mjadala huo ulichochewa na taarifa ya Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara kwa kipindi cha Machi hadi Desemba 15 iliyowasilishwa na Mwenyekiti wake, Mahmoud Mgimwa.
"Matangazo mengi na ulipaji huduma na bidhaa nchini yamewekwa kwa fedha za kigeni, kitendo ambacho ni kinyume cha sheria," alisema Mgimwa.
Pia, Mgimwa alisema uchunguzi wao umebaini baadhi ya maduka ya kubadilisha fedha (Bureau de Change) yamekuwa yakijihusisha na uhamishaji fedha kwenda nchi za nje.
"Maduka hayo yanatumika kama uchochoro wa kutorosha fedha nje ya nchi na kusababisha kupotea kwa mapato ya Serikali, huku thamani ya shilingi ya Tanzania ikishuka thamani," alisema.
Kamati hiyo inaitaka Serikali kuwachukulia hatua wafanyabiashara wanaomiliki maduka hayo na kwamba, iongeze usimamizi ili kukomesha tatizo hilo lenye athari kwa uchumi wa nchi.
"Uzoefu wa nchi nyingi kama Afrika ya Kusini, Kenya na Ethiopia unaonyesha huwezi kupata fedha za kigeni kama hujaonyesha sababu, kitambulisho na hati ya kusafiria," alisema.
Akichangia taarifa hiyo, Mbunge wa Kisesa, Lwaga Mpina alisema hakuna nchi duniani inayoweza kufanya mambo ya kitoto kama Tanzania kudhibiti matumizi holela ya fedha za kigeni.
Sarafu ya Tanzania
Sarafu ya Kenya
Sarafu ya Afrika ya kusini
Sarafu ya India
Sarafu ya Botswana
Sarafu ya Canada