Matumizi ya dola ya kimarekani kama sarafu ya Tanzania

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Nimeshindwa kuelewa niiweke wapi thread hii baada ya kusoma makala moja pale Mwanachi kuhusu mada ambayo imekuwa inakera akili yangu muda mrefu sana. Thread ingeweza kuwa siasa, uchumi au kwenye falsafa; nikaamua kuiweka hapa kwenye falsafa.

Nimekuwa na bahati sana ya kutembea na kuishi katika nchi nyingi sana duniani, ila sijawahi kufika nchi ambako biashara zote zinafanyika katika dola za kimerakni zaidi ya marekani kwenyewe. Hata Kanada ambayo ni jirani kabisa na marekani na raia wake wanafanya manunuzi yao sehemu yoyote ya mpaka, ukishavuka kuingia Canada unatumia Canadian Dollar, na ukirudi Marekani unatumia American Dollar.

Je kinachotusumbua watanzania ni ulimbukeni au kweli ni udhaifu wa sarafu yetu? Nimeangalia trends kwa muda wa miaka kumi kuhusu mabadiliko ya thamani ya sarafu mbalimbali dhidi sarafu ya kimarekani na kugundua kuwa sarafu yetu ni stable kiasi cha kutosha, kwani haijawahi kubadilika ghafla ghafla. Ingawa kuna nchi nyingine kama Kenya na South Afrika zilikuwa stable zaidi yetu lakini mabadiliko ya sarafu ya Tanzania hayajawa so alarming kiasi kuwa biashara zetu tuziendeshe kwa hela ya kigeni; nikitoka Tabora na hela yangu ya madafu siwezi kulala hoteli za maana Tanzania mpaka ninunue dola za kimarekani na kumpa faida muuzaji wa dola hizo kabla sijampa faida mtu wa hoteli, je hiyo kweli halali kwa nchi?

Chini hapo nimeweka trends zinazoonyesha jinsi sarafu mbalimbali zilivyobadilika katika kipindi cha miaka kumi iliyopita. Ingawa sarafu ya Tanzania imekuwa inapoteza thamani, upotezu huo ni kwa currency investors tu wanaoinvest kwa muda mrefu kwani hauathiri kabisa katika biashara za kila siku kwa vile thamani hiyo ilikuwa inapotea kidogo kidogo. Mabadiliko ya thamani ya sarafu ya kitanzania hayatofautiani kabisa na yale ya sarafu ya Botswana lakini mpaka kesho hutakuta Botswana wanaendesha biashara ya ndani kwa kutumia dola ya kimarekani. India vile vile mambo ni hayo hayo.

Wataalamu wa mambo ya pesa mtusaidie kwenye tatizo hio.



Sarafu ya Tanzania



Sarafu ya Kenya




Sarafu ya Afrika ya kusini



Sarafu ya India



Sarafu ya Botswana


Sarafu ya Canada
 
Kichuguu;

Mwenyewe una makosa. Kwanini unaita sarafu ya Tanzania ni ya madafu wakati hiyo ndio pesa halali ya malipo nchini? Bila kuwepo na hiyo sarafu, mwenye akiba za dola za kimarekani nchini Tanzania hawezi kufaidi akiba yake. Hivyo ni lazima tuipe heshima hiyo sarafu.
 

Hapana mimi siiiti kuwa ni ya madafu. Ninaiheshimu!
 
Hapana mimi siiiti kuwa ni ya madafu. Ninaiheshimu!

Sarafu ya nchi ni commodity na kuna watu wanaoishi kwa kufanya biashara ya sarafu. Vilevile sarafu ya nchi inatumika katika kuweka akiba za watu. Hivyo kuna logic explanations zinazowafanya watanzania kutumia dola.

Moja ya explanation hizo ni uncertainity. Japokuwa shilingi ya Tanzania imekuwa katika kiwango kinachoeleweka kwa muda mrefu, hiyo haitokani kwa sehemu kubwa na sera za pesa za Tanzania. Inatokana na ukweli kuwa sera za pesa za Marekani katika miaka ya karibuni ni kushusha thamani ya dola.
 
Tunazihitaji sana dola za kimarekani kwa sababu tuna-import zaidi kuliko tuwezavyo ku-export, katika hali kama hii hauna option zaidi ya kuitafuta dola kwa namna yeyote ile.
 
Tunazihitaji sana dola za kimarekani kwa sababu tuna-import zaidi kuliko tuwezavyo ku-export, katika hali kama hii hauna option zaidi ya kuitafuta dola kwa namna yeyote ile.

Kwani unapo-import huwa unalipa hela taslimu, yaani unatuma boksi la manoti au unatuma karatasi tu inayoonyesha kuwa pesa zinatoka katika benki yako hapa Tanzania na kwenda kwenye benki ya anayekuuzia bidhaa huko aliko ?
 

Maisha ya sarafu duniani kote ni uncertain, hakuna sarafu duniani ambayo haibadiliki thamani, kila sarafu including dolar ya kimarekani, hubadilika thamani yake karibu kila siku. Kinachokosekana ni watanzania kutokuwa na imani na sarafu yao tu. Inflation ndiyo jambo ambalo linalosababisha watu wasiwe na imani na sarafu yoyote ile, kwa Tanzania inflation rate ni ya chini sana ukilinganisha na nchi nyingi duniani ambazo hazitumii dola ya kimarekani. Hebu angalia hiyo post ya Nyani Ngabu hapo chini.

Miaka kama kumi na mbili iliyopita nilikuwa natafuta viza (H1B) kwenye ubalozi wa marekani nikaambiwa nilipe ada ya dola 400, nikatoa dola hizo lakini wakanikatalia kwa kunitaka nilipe katika shilingi za kitanzania ambazo exchange rate waliyonipa ilikuwa ni nzuri hata kuliko hata ile ya kwenye Bureau de Change. Iwapo wamarekani wenyewe waliona hawana haja ya kutumia dola katika nchi nyingine inakuwaje sisi tunaishobokea namna hiyo?
 
Last edited by a moderator:
Bitcoin drove the point home. The point being all monetary systems - from the most primitive shell systems to the microsecond crunching trades on NYSE- and conventions are arbitrary, backed by intransigent high priests prone to the temptation to rig the LIBOR.

But that's just paraphrasing J. M Keynes.

Where is John Mashaka when you need him?
 
Last edited by a moderator:
 
Mkuu mijadala ya hapa ni muhimu sana kwa mambo mbali mbali kuhusu nchi yetu. Hawa Watawala wangekuwa wanakuja hapa kuiba mawazo ya GTs mbali mbali hapa jamvini na kuyaingiza katika sera zao na kuhakikisha yanafanyiwa kazi basi madudu katika utendaji yangepunguzwa sana kama siyo kutokomezwa kabisa, lakini wako busy kujikusanyia mabilioni na kupanga mikakati ya kuisambaratisha CHADEMA!!!!

BUBU BAK Umenikumbusha kuwa tuliwahi kuliongelea jambo hili miaka sita iliyopita, lakini serikali yetu haijawahi kulifanyia kazi muda wote huo.
 


Son;

Wakati mwingine kuna tatizo la capability. Tanzania ilitumia miaka ya mwanzo ya uhuru wake kujenga uchumi wa kijamaa ambao ulisema pesa si msingi wa maendeleo. Nchi haikusomesha financiers kwa sababu ilikuwa ni kujifunza ubepari. Sasa mnataka nchi ifanye miujiza kwa kitu ambacho haikujiandaa? Endelea kula matunda ya Chuo Kikuu Cha Chama Kigamboni.
 
Son hili la kuzuia dollarization nchini halihitaji kuwa na financiers. Kama ingekuwa ni Serikali makini basi ingesimamia kauli zake chungu nzima ilizozitoa tangu mwaka 2007 wakati wa Meghji kama Waziri wa Fedha hili tatizo lingeshakuwa ni history miaka 6 iliyopita, lakini kwa kuwa utendaji ni SIFURI limeendelea kuwepo hadi hii leo. Hao financiers unaowazungumzia hawahusiani kwa namna yoyote na tatizo hili.

 
 
 

Leaders aren't born. They are made. Kikwete alitumia muda mwingi kukimbiza mwenge. Je unategemea nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…