SoC04 Matumizi ya Elimu kidigitali kwa wanafunzi wa sekondari Tanzania hasa wanapokuwa nyumbani

SoC04 Matumizi ya Elimu kidigitali kwa wanafunzi wa sekondari Tanzania hasa wanapokuwa nyumbani

Tanzania Tuitakayo competition threads

Mr Mlokozi

Member
Joined
Jun 1, 2024
Posts
21
Reaction score
16
Ufafanuzi wa Elimu Kidegitali

Elimu kidigitali ni mchakato wa kujifunza na kufundisha unaotumia teknolojia za kidigitali kama kompyuta, vifaa vya mkononi simu janja, vishikwambi na mtandao ili kuboresha na kurahisisha upatikanaji wa maarifa na ujuzi. Elimu hii inajumuisha matumizi ya zana na majukwaa mbalimbali ya kidigitali ambayo yanawezesha wanafunzi na walimu kuwasiliana, kushirikiana, na kufikia rasilimali za elimu kwa urahisi zaidi.

Mfumo huu wa elimu umekuwa ukitumiwa na baadhi ya vyuo vikuu kama Open Unirversity of Tanzania ambapo wanafunzi wanapata elimu stahiki wakiwa popote pale walipo huku wakiendelea na shughuri zao nyingine bila kuhitajika kwenda katika mazingira ya chuo

Mfumo huu tunaweza kuutimia pia kwa wanafunzi wa sekondari hasa wanapokuwa nyumbani kipindi cha likizo na kwa wale walio katika xhule za kutwa mda ule wakiwa nyumbani.

Utafiti unaonesha kuwa asilimia Zaidi ya sitini 60% ya wanafunzi wa sekondari wanatumia simu janja wambazo wamenunuliwa na wazazi au walezi wao (hii ni kutokana na kukua kwa utandawazi) hivyo basi wanapopata mda wakiwa nyumbani hutumia simu hizo kuingia katika mitandao ya kujamii kufatialia maudhui yasiyofaa na hivyo kuporomosha maadili katika jamii

Mamlaka husika kupitia wizara ya elimu inaweza kutumia fulsa ya ukuaji wa utandawazi huu kuunda mfumo thabiti ambao utawawezesha wanafunzi hawa kutumiia simu zao wakiwa nyumbani lakini kwa manufaa Zaidi kielimu na kijamii na kuachana kufatilia mambo yanayoweza kuwaangusha kielimu na kimaadili

Faida za Elimu Kidijitali
Kuna faida nyingi za kutumia Elimu kidigitali kwa wanafunzi wa sekondari hasa wanapokuwa nyumbani ambapo wanakuwa na uwezekano wa kupata vifaa vya kujifunzia kama simu janja, kompyuta na tablets ikiwa ni pamoja na hizi zifuatazo

Upatikanaji wa Rasilimali: Teknolojia inawapa wanafunzi upatikanaji rahisi wa vitabu, makala, na video za elimu kutoka sehemu yoyote duniani hivyo kuwasaidia kupanua eliwa wao katika maeneo tofauti tafauti ya masomo yao.

Kupunguza upotevu wa raslimali za shule; wanafunzi wengi hupoteza raslimali za shule kama vitabu kutokana na kwamba wanapaswa kuazima vitabu vingi vya masomo tofauti laakini kwa kutumia elimu kidigitali mwanafunzi ataweza kupata vitabu vyota vya kiada na ziada katika mfumo wa nakala raini (soft copy) katika kishikwambi chake

Kupunguza upotoshwaji wa maadili kwa wanafunzi; kwa sababu wanfunzi hutumia simu janja wakiwa nyumbani kufuatilia mambooo yasiyofaa katika mitandao ya kijamii na kusababisha mmonyoko wa maadili, kwahiyo kuanzishwa kwa elimu kidigitali itawaruhusu wanfunzi hawa kutumia simu zao lakin kwa matumizi yatakayowasaidia kielimu na kijamii

Ubunifu na Ushirikiano: Inaruhusu wanafunzi kushirikiana na wenzao na walimu wao kutoka katika maeneo tofauti na itawaruhusu kupata mwanya wa kushirikiana na wanafunzi wa shule zingine kupitia majukwaa ya mtandaoni ili kupanua uwelewa.

Kujifunza kwa Kila Mtu: Inatoa fursa ya kujifunza kwa kasi na muda unaomfaa mwanafunzi binafsi. Maana ni kweli kwamba wanafunzi wanatofautiana katika mazingira wanyohitaji kwaajiri ya kujifunza hivyo Elimu kidigitali itamuwezesha mwanafunzi kutafuta mazingira rafiki kwa ajiri yake binafsi kujifunza

Kuwawezesha walimu kufanya ufuatialiaji wa kazi walizotoa kipindi cha likizo (home package); ili kuwafanya wanafunzi waweze kujisomea kipindi cha likizo shule zimekuwa zikitoa kazi za nyumbani ambapo maswali kadhaa utolewa na baadae hukusanywa na kusahihishwa baada ya likizo yaani shule zikifunguliwa. Hii inakosa ufanisi maana utafiti umeonesha kuwa asilimia kubwa ya wanafunzi wanakuwa bize na mitandao ya kijamii na siku mbii kabla ya likizo kuisha ndipo wanafanya kazi hizo kwa kunakiri bila kujisomesea ili kuwaridhisha walimu wanaporudi shule. Hivyo basi elimu kidigitali itawawezesha walimu kufatilia kwa karibbu na hivyo kufanya wanafunzi wawe na usomaji endelevu.

Changamoto za Elimu Kidijitali
zifuatazo ni changamoto zinazoweza kuukumba mfumo wa elimu kidigitali

Mgawanyo wa Kidigitali: Tofauti ya upatikanaji wa teknolojia kati ya maeneo mbalimbali (kijijini vs. mijini) na kati ya familia maskini na tajiri. Maana kuna maeneo kuna upatikanaji hafifu wa mtandao ambao nahitajika kwa ajiri ya elimu kidigitali kufanyika pia kuna familia maskini ambazo hawawezi kumudu gharama za kuwa nunulia watoto wao vifaa vya kieletroniki kama simu janja na vishikwambi

Ulinzi na Usalama: Masuala ya usalama wa mtandaoni na faragha ya wanafunzi maana wadukuzi wanaweza kudukua taarifa muhimu za wanafunzi kupitia mfumo huu wa elimu kidigitali.

Uaminifu na Maadili: Changamoto za kudhibiti udanganyifu na kuhakikisha uadilifu katika mitihani na kazi za wanafunzi maana wanaweza kutumia hii kama fursa ya kunadiliana majibu na hivyo kupunguza ufanisi.

Namna ya kushughulikia changamoto za elimu kidigitali

Serikari kupitia wizara husika kuingia ubia na makampuni ya simu na vishikwambi;
Serikali kupitia wizara husika yaani wizara ya Elimu pamoja na wizara ya Sayansi na Teknolojia kuingia ubia na makampuni ya simu na vishikwambi ili waweze kutoa vishikwambi shule ambapo shule itakuwa ikiviiazimisha kwa wanafunzi kutoka maktaba nah ii itasaidia ili kwamba vishikwambi hivi vinaweza kuwekwa ndani yake nakara lrainni za vitabu vya masomo yote na hivyo kurahishia mwanafunzi kupata vitabu vyote kwa kuazima kishikwambi kimoja badala ya kuazima kitabu cha kila somo.

Kubuni mfumo imara wa kudhibiti udanganyifu. Mfumo wa utoaji elimu kidigtali unapaswa kuuboreshwa kwa namna ambyo inappunguza udanganyifu mfano kumpata uwezo mwalimu kuuliza maswali kwa tofauti tofauti kwa kila mwanfunzi au kila mwanafunzi akawa na maswali yake binafsi ambayo yote yamelenga kupima kitu kimoja

Mifano na Matumizi Halisi

Vifaa na Programu Maalum
:
ili kuweza kufanikisha elimu kidigitali panahitajika vifaa maalumu na program za kujifunnzia vinavoweza kutumia mtandao hivyo napendekeza vishkwambi vitumike kwaajiri ya kufundishia kujifunzia elimu mtandaoni.

Mifumo ya kujifunza mtandaoni (Online Learning Systems), inayojulikana pia kama Mifumo ya Kudhibiti Kujifunza (Learning Management Systems, LMS), ni majukwaa ambayo yatatumika kusaidia mchakato wa elimu kwa njia ya kidigitali nayo ni haya yafuatayo.

1. Khan Academy
Maelezo
: Khan Academy ni jukwaa la elimu lisilo la faida linalotoa masomo ya bure mtandaoni kwa wanafunzi wa viwango vyote.

Vipengele: Video za masomo, mazoezi ya vitendo, rasilimali za walimu, na dashibodi ya kufuatilia maendeleo ya mwanafunzi.

Faida: Upatinaji wa rasilimali za bure kwa wanafunzi na walimu, zenye lengo la kuboresha uelewa na umahiri wa wanafunzi.

2. Udemy
Maelezo
: Udemy ni jukwaa la kujifunza mtandaoni linalotoa kozi mbalimbali zilizoandaliwa na wataalamu kutoka sekta tofauti.

Vipengele: Kozi za kulipia, kozi katika nyanja tofauti kama teknolojia, biashara, na maendeleo binafsi.
Faida: Utoaji wa kozi nyingi na zinazoendana na mahitaji ya soko, upatikanaji wa kozi zilizoandaliwa na wataalamu.

3. Google Classroom
Maelezo
: Google Classroom ni jukwaa la kudhibiti madarasa mtandaoni linalotumiwa na walimu na wanafunzi.
Vipengele: Kudhibiti kazi za wanafunzi, kuwasilisha majukumu, kutoa maoni, na kushirikiana kupitia Google Drive na Google Docs.

Faida: Urahisi wa matumizi, ushirikiano kupitia zana za Google, na upatikanaji wa bure kwa shule na taasisi za elimu.

Mustakabali wa Elimu Kidijitali
Katika mazingira ya elimu kidigitali, mitindo ya kujifunza ni anuwai na inaweza kubadilishwa ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi mbalimbali. Hapa kuna mitindo tofauti ya kujifunza katika elimu kidigitali:

Mitindo inayoweza kutumika kujifunza elimu kidigitali
Ifuatayo ni mitindo inayoweza kutumika kufundishia wanafunzi elimu kidigitali hasa wakiwa nyumbani bila kuathiri maana halisi ya likizo ikiwa ni kupumzika

1. Kujifunza kwa Kutumia Michezo (Gamified Learning)
Kujifunza ambapo vipengele vya michezo vinatumika kuongeza motisha na ushiriki wa wanafunzi kwa kutumia michezo mbali mbali ambayo ndani yake kuna maudhui ya kujenga uelewa kwa mwanafunzi. Faida yake ni kwamba uongeza motisha kwa wanafunzi kujifunza kupitia ushindani na michezo.

2. Kujifunza kwa Kutumia Simulizi (Simulated Learning)
Maudhui ya ufundishaji yanaweza kuwekwa katika simulizi mbalimbali za kusisimua na kufurahisha na kuchekesha ambapo wanafunzi watavutiwa Zaidi kusikiliza badala ya kufuatilia mambo yasiyofaa kwenye mitandao ya kijamii

3. Kujifunza kwa Kutumia Majukwaa ya Mitandao ya Kijamii (Social Learning)
Kujifunza ambapo wanafunzi wanashirikiana na kujifunza kutoka kwa wenzao kupitia mitandao ya kijamii. Vikundi vya kujifunza mtandaoni, mijadala kwenye majukwaa ya kijamii, na kubadilishana rasilimali. Faida ya kutumia majukwaa ni kwamba wanafunzi kutoka shule mbalimbali wanaweza kushirikiana na kupanua uelewa

4. Kujifunza kwa Kutumia Video na Maudhui ya Multimedia (Video and Multimedia Learning) Kujifunza ambapo video na maudhui ya multimedia yanatumika kufundisha na kuelezea dhana. Mihadhara ya video, maingiliano ya multimedia, na mawasilisho ya infographics.

Kila mtindo wa kujifunza kidigitali una faida zake na unaweza kuendana na mahitaji na mapendeleo ya wanafunzi mbalimbali. Uchanganyaji wa mitindo hii pia unaweza kuongeza urahisi na ufanisi wa kujifunza.

Maoni Binafsi
Kwa mtazamo wangu naona kwamba elimu kidigitali inaweza kusaidia kupunguza tabia ya vijana mtaani ya kufuatilia maudhui yasiyofaa mtandaoni ambayo yan mchango mkubwa sana katika kuporomosha maadili ya jamii na taifa kwa ujumla
 
Upvote 0
Back
Top Bottom