Matumizi ya energy ni bomu kwa Vijana Afrika

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Ni kawaida VIJANA wa kileo kushindana katika kufakamia Red Bull, Monster Energy, MO Energy na vinginevyo, huku Wengine wakioneshana ubobezi wa kuchanganya Vinywaji Hivyo na Pombe.

Chombo Cha UMOJA wa ULAYA chenye Mamlaka ya kusimamia Usalama wa Chakula (European Food Safety Authority, kimebainisha kuwa Asilimia 30 ya Watu wazima hutumia Energy Drinks, Asilimia 68 Ni Watoto wa Umri wa Miaka 16-18 na Asilimia 18 ni Watoto CHINI ya Miaka 10.

Pamoja na Ongezeko la Watoto na VIJANA Wanaotumia, Tafiti zinaonesha kuwa Matumizi ya Vinywaji vya kuchochea nguvu maarufu Kama Energy Drinks, Yana athari Kubwa kwa Afya ya Mwanadamu.

Utafiti uliofanywa na Jopo Wataalam toka Shirika la Afya Ulimwenguni 'WHO,' umethibitisha kuwa vivywaji vya Energy, ambavyo ni mchanganyiko wa kichocheo Cha Caffeine, sukari, Sodium na Taurine ni Chanzo kikuu cha MATATIZO ya MOYO, Akili ikiwemo kukosa usingizi, Shinikizo la Juu la DAMU, Shambulio la MOYO, Mpapatiko wa MOYO(Heart Palpitations), sonona, Kukosa utulivu(Restlessness) na kuishiwa maji mwilini(dehydration, na vifo vya ghafla, kutokana na Shambulio la MOYO(cardiac arrest).

Kwa mujibu wa Matokeo ya Utafiti wa Chuo Kikuu cha Toronto ya Mwaka 2015, Matumizi ya Energy Drinks yaweza kupelekea Athari ya kuharibika kwa UBONGO.Brain Damage.

Hatari ya Matumizi yya Energy Drinks huongezeka Mara dufu pale vinywaji hivyo vinapochanganywa na Pombe. Kuto

Athari ya vinywaji Hivyo kwa Watoto zimepelekea Ushirikiano wa Madaktari wa Marekani(American Medical Association) kuzuia Watoto CHINI ya Miaka 18 kutumia Energy Drinks.

Dokta Stephen Nguyan MD, Palo Alto wa Taasisi ya Afya wanadai kuwa Matumizi ya vinywaji hivi si SALAMA kabisa. Wakati chupa Moja ya SODA(COKE, PEPSI) kina KIWANGO cha Caffeine cha miligramu 35, vinywa vya kuchochea nguvu maarufu Kama Energy Drinks vina Caffeine miligramu kuanzia 150 Hadi 280. Kiwango Cha juu Cha caffeine kwa MTU Mwenye kilo 70 Ni miligramu 210.

Kuhusu vifo vinavyotokana na Energy Drinks, Dalili za MWANZO Ni kifua kubana, uchovu, miguu kuvimba, kizunguzungu kikali, kuona giza la ghafla, Kukosa usingizi. Unapohisi Dalili hizo ni king'ora Cha HATARI.

Nimeshuhudia VIJANA wawili, wabobevu wa Matumizi ya Energy Drinks Wakipoteza MAISHA kwa Shambulio la MOYO. VIJANA walioshaurika na kuacha Matumizi ya vinywaji Hivyo Hadi Sasa wako hai.

Je, tunapoteza nguvu KAZI kiasi gani kutokana na JINAMIZI HILI? Je, tutakwepaje HATIA ya kukitoa KAFARA kizazi chetu kwa kigezo feki Cha Kulinda UCHUMI?

VIJANA wa Bara la AFRIKA wapaswa kulitegua BOMU hili HATARI kwa kwa kupaaza SAUTI Ili Nchi zao ziwe na SERA za Kulinda USALAMA WA WATU WAO. Katika hili Tanzania yapaswa kuongoza usukani.
 
Basi hali ni tete sana huko mitaani,maana kuna siku nilikaa sehemu kuna jamaa mtu mzima around 45yrs alikuwa anachanganya Redbull na KVant,nilijiuliza kama mchanganyiko huu ni salama sikupata majibu,na kama hii ni kweli basi wanaumia wengi...
 
Ukienda ufukwe wa Hindi utakuta mamilioni ya chupa za kopo 90% ni energy hasa Mo energy.lakini pia makopo haya hayawi recycled kama Yale ya maji.haya ya Mo na azam yanatupwa na kuleta uchafu usiooza
 
Hizo zababu mbili za mwanzo nakubaliana nazo kwa 100%.

Nilipokuwa natumia Energy drinks nilianza kuwa na tatizo la moyo, nikitembea barabarani ghafla mapigo ya moyo yanaongezeka nashindwa kujua sababu, na usingizi usiku ukawa wa kutafuta sana.

Mpaka nilipokuja kujiuliza nimebadilisha au kuongeza kitu gani kwenye mfumo
wangu wa maisha ndio nikahisi ni Energy drinks, nikaamua kuacha kuzitumia, mpaka leo sijawahi kuwa na matatizo hayo tena.
 
Nishati itokanayo na vyakula ni gharama mno .
Nishati ya makamba nayo haipatikani KWA uhakika.

Ni bora nishati ya mo na bakhresa ni shilingi mia 600 au mia tano na ni KWA uhakika
 
Back
Top Bottom