Sekta ya nishati na madini ni moja kati ya sekta muhimu na inayogusa maisha ya mwananchi mmoja mmoja hata mwananchi wa kipato cha chini.
Moja ya bidhaa za sekta hii ni mafuta ya petrol na dizel ambayo huagizwa kutoka nje ya nchi na kupelekea nchi kutumia fedha nyingi za kigeni katika uagizaji wake na kupelekea baadhi ya adhari za kiuchumi katika nchi yetu.
Nchi yetu imebarikiwa kuwa na gesi asilia katika bahari yetu na gesi hii inaweza kutumika kama mbadala wa mafuta ya petrol na dizel na kuweza kuongeza mapato ya nchi kukuza uchumi wetu na kupunguza gharama za maisha.
MADHARA YA KUAGIZA MAFUTA KUTOKA NJE YA NCHI
NINI KIFANYIKE

- Moja ni matumizi makubwa ya fedha za kigeni katika uagizaji wa mafuta na kupelekea shilling ya nchi yetu kushuka thamani.
- Pili kupanda kwa bei za mafuta mara kwa mara kutokana na adhari za moja kwa moja kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia pia kutokana na ufinyu wa ghala la kuhifadhi mafuta lenye uwezo wa kuhifadhi mita za ujazo millioni 1.25 zenye uwezo wa kutosheleza matumizi ya nje na ndani ya nchi kwa mwezi mmoja tu hivyo kukosa fursa ya kuagiza mafua zaidi pale bei ya mafuta katika soko la dunia inaposhuka.
- Tatu na mwisho kwa upande wangu ni kuongezeka kwa mfumuko wa bei za bidhaa na kupanda kwa gharama za maisha pale bei za mafuta haya zinapoongezeka hii inatokana na kupanda kwa bei za uzalishaji na usafirishaji zinazotumia mafuta haya.
- Moja ni kushuka kwa mfumuko wa bei za bidhaa na gharama za maisha
- Kuongezeka kwa mapato ya ndani ya serekali
- Kukua kwa uchumi wa taifa
NINI KIFANYIKE
- Serekali ipunguze tozo kwa magari ambayo waagizaji wake wameridhia kubadilisha mifumo ya magari yao kutoka kutumia mafuta kuja kwenye matumizi ya gesi.
- Pia serekali inaweza kuingia ubia na makampuni binafsi kwaajili ya kubadili mifumo ya magari ya wananchi kutoka kutumia mafuta kuja katika matumizi ya gesi kwa makubaliano ya kuwabadilishia bure wananchi na serekali kuwalipa kwa awamu kwa fedha zitakazo tokana na kuongeza tozo kiasi katika bei ya gesi ambayo mpaka sasa ni Tsh 1600 kwa kilo moja ya gesi yenye uwezo wa kwenda umbali mara mbili ya mafuta.
- Serekali kuweka sera ya kuweka pampu moja ya gesi katika vituo vyote vya mafuta ili upatikanaji wa mafuta uwe wa uhakika hii itasaidia kuwavutia wananchi kutumia nishati ya gesi asilia katika magari yao kwa kuwa kuna uhakika wa upatikanaji wake.
Upvote
2