Matumizi ya Ikulu mbili (Magogoni na Dodoma) siyo chanzo cha kutumia trilioni 33 kama OC huku 15Trln zikiwa za maendeleo?

Matumizi ya Ikulu mbili (Magogoni na Dodoma) siyo chanzo cha kutumia trilioni 33 kama OC huku 15Trln zikiwa za maendeleo?

wazungu wangekuwa wavivu na akili ndogo kama nyie leo hii USA isingesimama, ulishawahi kusikia chochote kuhusu the wild west USA? hiyo Dar yenyewe mnaing’ang’ania kwa sababu wazungu christians walijenga kila kitu, kama Mzungu christian angebakia tanzania na kuijenga dodoma leo hii mngegombania kwenda kuishi huko.

Christian (western) ndiyo suluhisho, tanzagiza haiwezi kuendelea bila ya ku-adapt christian phylosophy.

FIY Mzungu christian alikuwa na mpango wa kuifanya Tabora ndiyo mji mkuu wa nchi yetu na kuhama Dar sema mipango ilivurugwa na vita kuu wa dunia, laiti ingefanikiwa leo hii wote mngekuwa mnakimbilia kuishi Tabora …
 
Kama tu, wangeweza kuchakata hoja yako na kuchukua mazuri bandiko lako lingeleta mabadiriko.
Lakini sasa how? Who? When?
 
Mama Samia kwa vitendo hakubalini na Ikulu ya Chamwino. Kinadharia kwa mtu aliyewahi kukaa Dodoma siyo sehemu yakukaa ukafanya kazi za kuumiza kichwa kama kuongoza nchi.

Hali ya hewa ya Dodoma ni nzito sana na usipokinbia kimbia kwenda mikoani lazima utababuka ngozi na kuondoa kunawiri. Ni mji ambao unahitaji miti mingi na maji safi kutoka kwenye maziwa au mito.

Lakini pamoja na ubaya wa mji wenyewe tayari JPM aliweka Ikulu. Awali Majaliwa alitaka watu wasisafiri bila kibali kwa kutambua kwamba Dodoma haizoeleki. Hata wagogo tu wakina Malecela na Ndugai wanaishi DSM kuliko Dodoma. Upepo wa Dodoma unafifisha uzuri wa viumbe na hivyo hata mifugo haiwezi kustawi na kunawiri. Mimea nayo haikubali, yote hii ni kutokana na hali ya hewa . Factor hizi zilimfanya Majaliwa akwame kudhibiti watu na matokeo yake tunaona siku nne yupo Dar na siku tatu Dodoma. Tunamwona Makamu wa Rais akitumia muda mwingi DAR kuliko Dodoma . Mawaziri mbinu yao kubwa siyo kwenda DAR coz mabosi wapo DAR, wao wanapishana kwenye mikoa....Mawaziri wengi wamekwenda kuingilia majukumu ya RC na DC. Kila siku wapo mkoani.

Nimeweka mandhari hii hapo juu kama msingi wakujadili ukubwa wa bajeti iliyotengwa kwa mwaka ujao ya maendeleo against matumizi ya kawaida.

Tumeambiwa tutatumia trilioni 33 kama matumizi ya kawaida against Trilioni 15 za maendeleo. Moja ya eneo linalokula zaidi ya asilimia 30 ya bajeti ya matumizi ya kawaida ni safari za viongozi kuanzia kwenye wilaya hadi mkuu wa nchi.

Lakini safari hizi nyingi zitachangiwa sana na ukweli kwamba wadau wa maendeleo wanaishi DAR na hawapo tayari kuhamia Dodoma. Hivyo viongozi wakubwa wanapokuwa DAR maana yake mawaziri lazima wawepo, wakuu wa vyombo vya usalama wawepo, majaji wawepo, viongozi wa bunge wawepo , makatibu wakuu wawepo nk. Kwa mwezi mmoja naamini zaidi ya Trilioni moja inatumika kulipa safari za viongozi


Key Message; MHE RAIS baada ya bajeti kupitishwa fanya jaribio lituatalo mara tatu kwa mwaka.

Hazina wanapotoa OC waambie wachukue OC ya taasisi zote inayohusu safari then waweke kwenye akaunti let say iite SHULE. Kwa mwezi huo piga marufuku safari zote na fedha husika zipeleke kujenga shule

Baada ya miezi mitatu, fungua akaunti nyingine iite afya. Chukua fedha zote za safari ikiwemo mafuta then kajenge na kukarabati zahanati na vituo vya afya

Waruhusu wazurure miezi mitatu kisha mwezi unaofuata chukua fedha zote za safari ziweke kwenye akaunti kisha ziite maji; tumia fedha hizo kupeleka maji ya ziwa Victoria Dodoma, Manyara, Singida na baadhi ya maeneo ya Tanga kama Kilindi........

Awamu ya nne fungua akaunti iite Barabara za mitaa; chukua hizo fedha zipeleke kwa Tarura watengeneze barabara za vijiji.

Mama ukitumia mbinu hii hakuna kiongozi atakufa njaa kwa kutosafiri miezi minne kwenye mwaka mzima; hakuna shughuli ya serikali itaathirika kwa mawaziri na viongozi wengine kutosafiri kwa miezi minne ndani ya mwaka na hakuna kiongozi wa taasisi itakayoweza kuhoji kwanini umetumia fedha za OC kuwagawia wananchi.

Mwisho, ukifanya haya kati ya Julai 2024 na Julai 2025, badala ya kuzunguka kupiga kampeni utazunguka kwa miezi miwili kabla ya uchaguzi kufanya uzinduzi wa miradi iliyotokana na kupunguza gharama za safari za viongozi nchni.

Lakini pia mkakati huu unakwenda kukuweka karibu na wananchi na kujipunguzia tension na matishio ya makundi ya kisiasa yanayojiona yanakubalika kuliko wewe kwa wapiga kura.

Fanya haya naamini hautafeli.
Mkuu mimi hii njia yako ninaichukua na kuitumia kwenye maisha yangu binafsi. Siku moja nitakupa mrejesho. Hakika ni bonge moja la idea lakini je atakusikiliza? Hapa ndipo kazi ilipo.
 
Ni ngumu sana kwa mtu mpumbavu kukubali upumbavu wake.watawala wengi wa bara hili wanaingia katika kundi la wapumbavu,hivyo kuzingatia ya umuhimu hawawezi.
 
Unaposema OC ujue ndio imebeba dhana pana
Sio kwamba ni safar tu.sawa wanasafir ila ujue hapo hapo kuna mafuta ,ya doria kwa watu wa doria haya kuna malipo ya casual labor ambayo ni lazima,mikate je?
 
Back
Top Bottom