Matumizi ya kiingereza: "Somehow" na "Somewhat"

Matumizi ya kiingereza: "Somehow" na "Somewhat"

Lakini licha ya unyoofu wake ambao unafanya iwe hata rahisi kujifunza [huwa nawaambia watu Kiswahili ni lugha rahisi sana kujifunza], Kiswahili bado kinawapa tabu hata watu ambao ndo lugha yao ya kwanza.

Kinawapa tabu kwenye sarufi, tahajia, msamiati, matamshi, na mengineyo.

Sijui hasa sababu ya hilo ni nini. Ningeweza kusema labda ni athari za makabila mbalimbali tuliyonayo lakini kama hilo ndo lingekuwa tatizo basi wale ambao lugha waijuayo ni moja tu, yaani Kiswahili, wasingekuwa na tatizo kabisa.

Unakuta mtu kazaliwa Dar, kakulia Dar, kasomea Dar, lakini Kiswahili [sanifu] kinampiga chenga!
Kiswahili sanifu, kwa mantiki ya usanifishaji wa lugha, kiunguja ndio RP yetu. Hivyo wa Dar nao hawana budi kujifunza kiswahili fasaha. Hakizungumzwi Dar bali Unguja.
 
Kiswahili sanifu, kwa mantiki ya usanifishaji wa lugha, kiunguja ndio RP yetu. Hivyo wa Dar nao hawana budi kujifunza kiswahili fasaha. Hakizungumzwi Dar bali Unguja.

Hiyo ni kwa mujibu wa nini/nani?
 
Hiyo ni kwa mujibu wa nini/nani?
Nilisoma HKL mkuu, usanifishaji wa lugha ni mada moja wapo, na kwa mujibu wa lile somo na mwalimu wangu, lahaja iliyorasimishwa kwa matumizi ya kiswahili ni "kiunguja" na hoja zake zikatolewa. Niko huru kujifunza.
 
Nilisoma HKL mkuu, usanifishaji wa lugha ni mada moja wapo, na kwa mujibu wa lile somo na mwalimu wangu, lahaja iliyorasimishwa kwa matumizi ya kiswahili ni "kiunguja" na hoja zake zikatolewa. Niko huru kujifunza.

Hiyo lahaja ilirasimishwa lini, wapi, na nani?
 
Hiyo lahaja ilirasimishwa lini, wapi, na nani?
Mkuu, unataka nirudi tena darasani? Mwanangu yuko levo hizo sasa, nami niko na mengine kabisa. Ila kama kuna mapya ktk hilo, nimekwambia niko tayari kujifunza. Kama sikosei ni miaka ya 40s, kikao Nadhani Mombasa, enzi ya waingereza. Nirekebishe, Mi hata madaftari yake siyakumbuki yalikuwaje, hata mwandiko umeshabadilika mara kadhaa.
 
Mkuu, unataka nirudi tena darasani? Mwanangu yuko levo hizo sasa, nami niko na mengine kabisa. Ila kama kuna mapya ktk hilo, nimekwambia niko tayari kujifunza. Kama sikosei ni miaka ya 40s, kikao Nadhani Mombasa, enzi ya waingereza. Nirekebishe, Mi hata madaftari yake siyakumbuki yalikuwaje, hata mwandiko umeshabadilika mara kadhaa.

Kujadili mambo kama haya bila rejea hainogi kabisa.
 
Kujadili mambo kama haya bila rejea hainogi kabisa.
Nilitarajia wewe haya unayajua zaidi, post yako ya juu imeonesha hivyo. Halafu ni jambo la nje sana, sidhani kama linahitaji authority. Nitaitafuta.
 
Nilitarajia wewe haya unayajua zaidi, post yako ya juu imeonesha hivyo. Halafu ni jambo la nje sana, sidhani kama linahitaji authority. Nitaitafuta.

Acha maneno mengi. Lete rejea ili tujadili vizuri.
 
Namna gani ikiwa mtu akisema "Somehow it is cold today", akimaanisha kwa namna fulani leo kuna baridi. Akimaanisha baridi wakati wa msimu wa joto ama mahala ambapo kwa kawaida hapapashwi kuwa baridi. Kwa lugha nyingine hamaanishi kiwango cha baridi bali aki refer namna ilivyotokea kukawa na baridi.

Au akasema "Somehow it is a problem", kwa kumaanisha kwamba suala analoliongelea katika hali ya kawaida siyo tatizo lakini kuna namna fulani linaweza kuleta tabu kwa upande mwingine. Au a kwalugha nyingine akawa hana maana ya ukubwa ama kiwango cha tatizo bali ni kwamba kwa namna fulani hilo suala ni tatizo.

?
Binafsi nimekuelewa sana
 
Jifunze nami kingereza kwa kiswahili kwa bei cheee, kwa mwezi. Masomo ni online na ni kwa miezi miwili 2,Tunasoma kwa video, pich, audio no kupitia WhatsApp peke,Nipigie sasa na utokwe na aibu ya kutojua kingereza fasah ingali wew ni msomi, many a bias hara ama mtendaji wa serikali,Piga 0753093869,baada ya kuhitimu tutakupatia ajira ukitaka, katika mataw yetu yotee... Mfano wa masomo yetu:

Somo la 1

(SECTION A; TENSES IN THE ACTIVE VOICE )

(A)Simple Tenses ,:

1. Simple Past Tense ( ‘li’)
- Wakati huu huongelea jambo lililofanyika na kukamilika mara moja wakati uliopita.
Mifano ; tulikuja ,walitembea, alicheza.
- Wakati huu huashiriwa na silabi ‘li’ ambayo hufanya tutambue kuwa tunaongelea jambo lililofanyika mara moja na likamalizika kufanyika katika wakati uliopita. Hii silabi ‘li’ ni lazima iunganishwe na kitendo moja kwa moja kabla ya kitendo. Mfano ; ‘Tuliimba’, tofauti na ‘Tulikuwa tunaimba’ ambapo ‘li’ imefuatiwa na kifungu ‘kuwa’ na sio kitendo. Katika maneno ‘tulikuwa tunaimba’, kitendo ‘imba’ kimetanguliwa na ‘na’ na sio ‘li’ kwa hivyo maneno hayo hayapo katika wakati huu wa Simple Past Tense, ‘li’.

Kanuni za kutumia Simple Past Tense ‘li’

a) Sentensi za taarifa/kutoa taarifa
Katika wakati huu, huwa tunapoelezea jambo tunatanguliza mtendaji wa jambo, (I/We/You/They/He/She/It) kisha tunafuatisha kitendo moja kwa moja kikiwa katika umbo la wakati uliopita.
Mfano ; - kitenda ‘enda’ ni ‘go’. Umbo lake la wakati uliopita, yaani ‘-lienda’ ni ‘went’. Tutatanguliza mtendaji wa jambo kisha tufuatishe neno ‘went’.

Sentensi za mifano;
- Juma alienda. ………. Juma went.
- Tulienda. ……… We went.
- Basi liliondoka. ……. The bus left.
- Nilicheza. ……. I played.
- Uliimba. ….. You sang.
- Walikimbia. ….. They ran.
- Maria alipika. ……. Maria cooked.
NB : Hatuweki kitu chochote katikati mwa mtendaji na kitendo.

b) Kuuliza maswali katika Simple Past Tense

- Maswali katika wakati huu huanzia na neon ‘did’. ‘Did’ ikitumika ni lazima kitendo kiwe katika umbo la kawaida kwa sababu ‘did’ ina ‘li’ ndani yake hivyo ‘li’ nyingine haihitajiki. Ina maana hiyo ‘did’ tayari imeshawakilisha wakati uliopita.
- ‘Did’ hufuatwa na nafasi inayouliziwa swali.
Mifano ya tafsiri :
- ‘Did Juma _______ ?’ …….. ‘Je, Juma ali______?’
- ‘Did they _______ ?’ ………. ‘Je, wao wali______ ?’

Sentesi za mifano :

1. Did Juma go?
Je, Juma ali enda ?

Jibu ; ( Hapana, hakuenda)…..( Kukanusha)
No, he didn’t go.
Au ; ( Ndio, alienda)…. Kukubali
Yes, he went.

2. Did she cook?
Je, alipika?

Jibu ; ( Hapana, hakupika)…..Kukanusha
No, she didn’t cook.
Au ; Ndio, alipika….. (Kukubali)
Yes, she cooked.

** katika kitabu kuna michoro ambayo inaonyesha tafsiri ya moja kwa moja ya kila kipengele cha sentensi kutoka kiswahili hadi kingereza ila hapa hatujaionyesha.

NB ; Tukiongeza neno ‘did’ katikati mwa jibu la kukubali, huwa ni kuweka msisitizo kama vile ambavyo kwa Kiswahili huwa tunaandisha sauti ili kuweka msisistizo ila sasa kwa Kingereza sauti haipandishwi ila msisitizo upo pale pale.

Mifano ; 1. Did Juma go ? …… Je, Juma alienda?
- Yes, he did go. ….. Ndio, alienda! (KWA MSISITIZO)

2. Did they cook? …….. Je, walipika?
- Yes, they did cook. …… Ndio, walipika! (KWA MSISITIZO)

NB ; Tunapokanusha sentensi kwa kutumia ‘did not’/ ‘didn’t’ , huwa hatutumii kitendo kikiwa katika umbo la wakati uliopita maana ile ‘did’ inakuwa imeshawakilisha wakati uliopita (‘li’ ambayo kinume chake ni ‘haku’) kwa hivyo hatuhitaji wakati uliopita kwa mara ya pili. Tukitumia umbo la wakati uliopita pia kwa kuuliza swali lililoanzia na ‘did’ pia tunakuwa tumeweka ‘li’ mbili katika sentensi, jambo ambalo sio sahihi.

Mifano ; 1. She didn’t went yesterday. ( Badala ya ‘She didn’t go yesterday.’)
Haku lienda jana. ( Badala ya ‘Hakuenda jana.’)

Au; 2. Did she went yesterday?
( Badala ya ‘Did she go yesterday?’)

- Je, yeye ali lienda jana?
( Badala ya ‘Je, yeye alienda jana?)
 
Back
Top Bottom