Matumizi ya "L" na "R" kwenye kiswahili

Matumizi ya "L" na "R" kwenye kiswahili

majebsmafuru

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2017
Posts
454
Reaction score
636
Imefika wakati basi Baraza la Kiswahili lihalalishe tutumie "R" panapokuwa "L" na vice versa...
Maana watu tunashindwa kabisa kutumia hizi Letters panapotakiwa, mfano..
  • Karo = Kalo
  • Kura = Kula
  • Laini = Raini
  • Limbwata = Rimbwata
  • Mara = Mala
  • Leo = Reo
  • Rekebisha = Lekebisha
  • Vurumisha = Vulumisha
  • Mchele = Mchere
  • Analia = Anaria
  • Elfu = Erfu
  • Thelathini = Therathini..
  • Radio = Ledio
  • purukushani = pulukushani
  • Remmy Ongala = Lemmy Ongara
  • Dada Ritha = Da Lita
  • Barrick = Baliki
  • Wizara = Wizala
  • Halmashauri = Harimashauli
  • Baraka = Balaka
  • Ramadhani = Lamadhani
  • Robert = Lobati
  • Ricky = Liki
  • Railways = Lelwey
Kinyaa kabisa...
Tuongezee..
Si muda mrefu nami nafikiri ntatumbukia kwenye hili janga...😡🙁
 
hili ni tatizo kwa watu wengi
vizuli=vizuri
mirima=milima
 
Mi mtu anae andika au kuongea hivi huwa na kaa nae mbali
 
Wasukuma na wenzao wenye matatizo hayo wanatuharibia lugha yetu. Wakiongozwa na na ........ [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji1]
 
Inaudhi sana, mtu siku zote anasikia na kuona Rais wetu anaitwa Magufuli lakini utakuta yeye anaandika "Magufuri".

Halafu na yale ma "ga" wanayoongezea, yanakera sana.

Nahisi kama kuna usaliti wa lugha unafanyika kwa makusudi kabisa.
 
Faiza fox atakuja asaiv kuwafanyia masahihisho ni kibibi flan iv kinafanya kazi BAKITA
 
Kuna hizi herufi zinanichanganya toka la popo hadi leo a e i o u na ha he hi ho hu
Sasa zinakuchanganya nini wewe jamaa.

Wewe utakuwa mtu wa kusini tu. Watu wa Lindi na Mtwara ndiyo zao.
 
Hili tatizo lipo kwa makabila ambayo Kiswahili sio lugha ya kwanza. Pia malezi, sehemu uliyokulia na hata shule ulizosoma mtu. Ni janga la taifa.
 
Imefika wakati basi Baraza la Kiswahili lihalalishe tutumie "R" panapokuwa "L" na vice versa...
Maana watu tunashindwa kabisa kutumia hizi Letters panapotakiwa, mfano..
  • Karo = Kalo
  • Kura = Kula
  • Laini = Raini
  • Limbwata = Rimbwata
  • Mara = Mala
  • Leo = Reo
  • Rekebisha = Lekebisha
  • Vurumisha = Vulumisha
  • Mchele = Mchere
  • Analia = Anaria
  • Elfu = Erfu
  • Thelathini = Therathini..
  • ,,,
  • ###
  • ....
Tuongezee..
Si muda mrefu nami nafikiri ntatumbukia kwenye hili janga...😡🙁
Kwa watu wengi,hasa vijana wa kizazi kipya, hili ni tatizo kubwa.Google
"How to pronounce R and L sounds-comparison,"labda itakusaidia kutoka kwenye janga hilo.
 
Bahati njema kanda ya huku hatunaga watu wenye hivyo vilimi vizito!
 
Back
Top Bottom