Matumizi ya "L" na "R" kwenye kiswahili

Matumizi ya "L" na "R" kwenye kiswahili

Tena kuna makosa kama Feza - Fedha

Sent from my VF695 using JamiiForums mobile app
 
1.Hutumika 1.Utumika 2.Akuja 2.Hakuja

Mtumiaji wa lugha yoyote anakitu kinachoitwa language device(kitivo cha lugha) akilini mwake. Ambacho ndicho humwongoza kuzijua kanuni na sheria zote za lugha. Vitivo vya watu wengine sijui vipo wapi

Hapo Hutumika mkuu hakuna Utumika

Akuja haipo ni hakuja. Viambishi vya awali vinakupiga chenga saana. Mimi mvivu kuandika ningefafanua vizuri nilifundishwa form two nikaelewa.
 
Kosa hilo linajulikana ni typo. Lakini la R na L ni upunguani.
Huwa nakereka saana kukuta mtu kaandika chakura kurara lamani.

Na akilini nimeshajingea tabia mtu wa namna hiyo ni Mshamba na huwa simpi "attention" saana.
 
Kwa watu au watoto wengi/sio wote walio zaliwa Dar es salaam wana shida ya kuweka L penye R ,mf.Ramani watasema lamani n.k,hata watoto wangu pia wameingia kwenye hilo janga nimesema mpaka nimeamua kuwaacha waongee wanavyotaka,maana sasa wanakua vijana lakini mambo ni yale yale...
 
Wanikumbusha wanangu pia, aise wako kama Sadistics! Usemavyo na kuwakanya kwenye mambo kama haya au mengine ya kurekebishana ni kama wanakuona zuzu! Kwanza nahisi wanafurahi napokereka, naona ndio yawafanya wawe na furaha, ni maudhi kabisa, mzazi yafika muda wanyoosha mikono na kwenda pub kushusha bia ulale tu, shida ya nini eti?! Shauri yao...
 
Kuna hizi herufi zinanichanganya toka la popo hadi leo a e i o u na ha he hi ho hu

1. Kaka ATAKUJA kesho = Sentensi inaeleza kitendo cha ujio wa kaka KITAFANYIKA kesho ( kitendo KITATEKELEZWA)
2. Kaka HATAKUJA kesho = Sentensi inaeleza kitendo cha ujio wa kaka HAKITAFANYIKA kesho (Kitendo HAKITATEKELEZWA)
 
Clistiano Lonaldo, Wayne Looney, Lomelo Rukaku, Gorl mahia, Loss Barkrey, Yannick Borasie, Dal Es Saraam, Seamus Coreman, Davy Kraassen, Reighton Baines, Idlissa Gueye, Adomora Rookman, Kevin Milarras, Ashrey Wirriams, Mason Horgate, Phir Jagierka, Galeth Bally, Aalon Renon.....Hahahahaha sina mbavu🙂🙂🙂🙂
 
Ni kero kweli kweli. Mtu anayeongea hivyo asiniongeleshe tafadhali
 
Ni kero kweli kweli. Mtu anayeongea hivyo asiniongeleshe tafadhali
Rakini kabira zetu na rafudhi zatufanya kiswahiri kiongerewe hivi dada, hatuna jinsi, kira mtu twajuwa hawapendi ira mararamiko yenu tunayushughurikia, mala kwa mala twajuwa twawakela watu rakini tufanye nini mama?!
 
Lugha mama ndio chanzo

Sent from my SM-J100H using JamiiForums mobile app
 
Rakini kabira zetu na rafudhi zatufanya kiswahiri kiongerewe hivi dada, hatuna jinsi, kira mtu twajuwa hawapendi ira mararamiko yenu tunayushughurikia, mala kwa mala twajuwa twawakela watu rakini tufanye nini mama?!
Umeniudhi ujue...sasa jamani hata kama ni kabila, umepelekwa shule ya msingi, sekondari mpaka chuo hubadiliki tuuu? Huyo mwalimu wako wa kiswahili alikuwa anafanya kazi gani?
 
Umeniudhi ujue...sasa jamani hata kama ni kabila, umepelekwa shule ya msingi, sekondari mpaka chuo hubadiliki tuuu? Huyo mwalimu wako wa kiswahili alikuwa anafanya kazi gani?
Pore dada basi wacha nisienderee kuchat nawe naona utaudhika zaidi...😳🙁
 
Back
Top Bottom