Matumizi ya mafuta kwa Toyota Ipsum

SPINE

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2017
Posts
1,068
Reaction score
1,150
Habari wadau, kama kichwa cha habari kinavyoeleza, naomba kujulishwa fuel consumption ya Toyota Ipsum kwa mdau yeyote anaeijua vizuri. Pia naomba maelezo zaidi kuhusu gari hii (mazuri na mabaya yake) maana ipo kwenye list ya gari nazotamani kumiliki.... Asante.
 
Nina uzoefu wa hii yenye cc2 elfu na mia zake ambazo ni VVTi injini zinaenda wastani wa km10 kwa Lita 1. Ni gari nzuri kuanzia kwenye bodi, nafasi ya gari, idadi ya siti, spea zinapatikana sana. Ila kumbuka kwa wakati huu mtu asikuogopeshe kwa ukubwa wa injini za magari kwani teknolojia imekuwa mno. Mfano mdogo tu ukichukua gari yenye cc 1900 kavu inatumia mafuta kiwango mengi kuliko hata gari yenye cc 2390 yenye vvti
 
Mkuu nashukuru sana kwa mchango wako, kwa hiyo haina tofauti sana na hizi zenye cc1900?
 
Mkuu una uzoefu wa kutumia IPSUM yenye 4WD? hii gari ni nzuri sana kwa matumizi ya familia au safari ambayo imezidi watu wa5, kingine injini yake ndo hiyo ipo kwenye baadhi ya harrier, klugger na rav4.
 
Hapana nimetumia 2wheal. Hivyo sina uzoefu na hiyo lakini kama ni injini yenye vvti siyo shida
 
Hapana nimetumia 2wheal. Hivyo sina uzoefu na hiyo lakini kama ni injini yenye vvti siyo shida
Una uzoefu wa kuweka matairi yenye size kubwa/au kuweka rim zenye size kubwa kwa ajili ya kulinyanyua ili kulifanya lipite vizuri kwenye mashimo?
 
Una uzoefu wa kuweka matairi yenye size kubwa/au kuweka rim zenye size kubwa kwa ajili ya kulinyanyua ili kulifanya lipite vizuri kwenye mashimo?
Niliwahi badili taili za Mbele nikaweka kubwa baada ya muda fundi alinishauri nizitoe kwani nimebadili mfumo orijino walioweka watengenezaji na kuniambia kuwa kuna madhara katika ulaji mafuta
 
Niliwahi badili taili za Mbele nikaweka kubwa baada ya muda fundi alinishauri nizitoe kwani nimebadili mfumo orijino walioweka watengenezaji na kuniambia kuwa kuna madhara katika ulaji mafuta
Lakini ulipoweka si liliinuka?
 
Teknolojia ya sasa wanajaribu kutumia umeme zaidi kwenye mfumo wa engine kupunguza ulaji wa mafuta.
 
Gari ukinyanyua uapoteza stability inakuwa inyumba kwenye mwendo mkali.
Mkuu Mani kukosa pesa mbaya sana, mtu unashindwa kununua gari ya juu maana bei imechangamka! mwisho wa siku tunaishia kuweka spacer, rim kubwa, tyre size kubwa! ila ni kweli gari likifanyiwa haya kuna athari kadhaa.
 
Kuna jirani wa mimi ameniuzia huu mkebe, ndio hapa nawaza kuhusu mafuta utafunaji wa mafuta....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…