Matumizi ya mafuta safari kutoka Dar es Salaam - Arusha

Kwa diesel engines?
 
acha uchokozi ....[emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]tuanzie hapo kwanza[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
mrejesho wa trip yangu ya arusha - dar kwenda nimetumia 60lt.. nilitembea mpaka korogwe kwa 26lt tu.. lakini wakati narudi chuga nimetumia 60 lt pia .. town trips za dar nimetembea 110km kwa 12 lt tu... so total nimetumia kama lita 132 imekaaaje hii wadau au ndio nikaguae plug???
 
Kwa subaru hapo naona ni kawaida..Ingekuwa IST, Spacio au hii Nissan yangu...tungeweka mkazo hapo kwenye plugs
 
Dar mbeya nilipiga 90,000 kipindi hiko hiko mafuta yameshuka 1.5 1NZ chuma nilikuwa nampelekea mtu baada ya kuitoa bandarini
 

Naenda mara kwa mara Dar -Rombo subaru forester 1990~2000cc natumia mafuta ya 110000~120000 kwenda tuu; kurudi 100000~110000 ( mafuta yakiwa sh 1989/ ltr). Sema nimegundua undeshaji wetu ndio tatizo ukiamsha juu ya speed 130 ndio inapiga sana. Kuna siku nilifika korogwe na mafuta ya 23000 na ni kama nusu ya safari niliponza kuipasua ile capet ya same [emoji23] shida tayari. Ila naamini siku nikiamua kwenda mwisho speed 120 asee hata mafuta ya laki 1 hayafiki.
 

ni sawah now mafuta 2303 nimetumia 132000 sh
 
Hahahah ile carpet inashawishi kinoma!
 
Kwan spid humaliza mafut?
Hahahah ukikaza mguu past 2 RPM ngoma inaanza kujiachia sasa inafyonza vizuri ukifikisha 3RPM jua uko speed ya 140KPH ama zaidi! Hapo unakung’utwa vilivyo inabwia utashangaa unapoteza fuel bars ndani ya muda mchache!

Hii kwa engine yangu uzoefu wake
 
Kwa gari ya cc2500 itakuwa ulicontrol sana revs na hukuzidi 100km/hr i assume ili upate angalau 15km/ltr
Alikuwa na soft foot! Maana kwa zile za kukaza mguu lazma angefika 3 RPM mara kwa mara!
 
Mi mwezi januari nikitumia gari yenye cc 1.5 nimetumia lita 50. Nilianza safari yangu usiku saa 2 dar nimeingia saa 9.30 alfajiri..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…