Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hayati inatumika kwa mtu maarufu ambaye amekufa lkn marehemu ni kwa watu wa kawaida na watoto wa mbwa kama sisi
Kama tutakwenda kwenye chimbuko la maneno Marhum na al hayat, Marehemu ni mtu aliyekufa au mwendazake wakati hayati ni maisha kwa ujumla mfano, Al-Hayat Al-Dunya (The Life of This World]. Ni bahati mbaya kuwa neno hayati hutumika vibaya na kinyume cha maana yake halisi. Si neno hilo tu. Hata neno kusudi. Wengi husema makusudi jambo ambalo ni kinyume cha dhana nzima ya neno husika. Siku hizi hata baada na badala zachanganywa na kukosewa mara nyingi ukiachia maneno mengine kama vile kumwita mwanamke binadamu wakati ni bintadamu. Anyways, leo sitongoi sana ingawa nimeishafunga nyama na nyasi zimeishatandikwa ugani tayari farasi kufungiana nyama na nyangwa.
Kumbuka kuwa hayo maneno yote mawili yametokana na lugha tamu ya Kiarabu,
Kwa maana halisi, Hayati ni "maisha yangu". Kiarabu ukisema Hayati "maisha yangu" kum address mtu akiwepo au asiwepo unamaanisha upendo wa hali ya juu na huyo ni mshirika wa maisha (shirka til hayaa) yako awepo au asiwepo.
Marehemu = Aliyesamehewa au ni kifupisho cha kusema "tunamuombea awe katika walio samehewa (Mercy) na Mwenyeezi Mungu".
Ukimwita mtu ambaye bado hajafa hayati si unaweza kuibua ugomvi mkubwa?. Sijawahi kusikia neno hayati likitumiwa kwa mtu ambaye hajafa.
Kwahiyo kwa Nyerere (Rais wa kwanza) hastahili kuitwa marehemu bali hayati? Basi kazi ipo.
Hili neno Hayat/ Hayati ni moja kati ya maneno yaliyokuwa yananisumbua maana yake .
Ninaona katika Kiswahili linatumika kwa mtu aliyekufa, lakini huku nilipo naona kuna magazeti yanaitwa al hayat
hapo ndipo nilipochanganyikiwa. Lakini kwa maelezo Mkuu Zomba sasa nimeelewa .Nashukura kwa aliyeuliza
maelezo ya juu ni sahihi ila ya mwisho si sahihi, kwani umejidunisha mtoto wa mbwa hawezi kuandika wala kutoa hoja!!! Wewe si mtoto wa mbwa!!!! Je ni sahihi?hayati inatumika kwa mtu maarufu ambaye amekufa lkn marehemu ni kwa watu wa kawaida na watoto wa mbwa kama sisi
Sisi tunaoishi nchi za kiarab hilo neno tunatumia sana kwa my dia, au kwa wapenzi wetu ndio tunawaita hayaty, au kwa kichombeza unamuita yaa hayaty, hata wanaume tunaitana habiby ni kawaida kabisa huku
Kumbuka kuwa hayo maneno yote mawili yametokana na lugha tamu ya Kiarabu,
Kwa maana halisi, Hayati ni "maisha yangu". Kiarabu ukisema Hayati "maisha yangu" kum address mtu akiwepo au asiwepo unamaanisha upendo wa hali ya juu na huyo ni mshirika wa maisha (shirka til hayaa) yako awepo au asiwepo.
Marehemu = Aliyesamehewa au ni kifupisho cha kusema "tunamuombea awe katika walio samehewa (Mercy) na Mwenyeezi Mungu".
Hakuna Hayatolah ila kuna Ayatollahneno hayati Linatokana na neno la kiarabu la Hayatollah maana yake ni mheshimiwa,wabongo wanali2mia kinyume kwa mtu alikufa.