Matumizi ya Mbolea katika kilimo cha karanga

Matumizi ya Mbolea katika kilimo cha karanga

Vp mwanzo ulivuna kiasi gani , kwa nusu heka ?
 
Mkuu Tafadhari sana mimi nililima kwenye shamba lilikuwa limewekewa mbolea ya samadi kwa wingi sana na akalima mara1 nami masika yaliyofuata nikalima karanga.Ni kwamba karanga zilikubali mno zilinawili hakuna mfano na zilizaa watoto wengi sana tena wakubwa cha ajabu ni kwamba kile cha ndani(karanga yenyewe) ni kadogo mno na kanakuwa na mwonekano wa kunyauka. Ndipo nilipoambiwa karanga na viazi havihitaji mbolea sana.

Kwa upande wa Viazi majani yanaweza yakawa mengi sana juu lakini kiazi kwa ndani ukakosa ukaambulia mizizi minene ama unaweza kupata viazi oversize ukikipika kinakuwa na mji maji hakina unga na saa nyingine hakiivi
hasa.Hii ni kwa uzoefu wangu kwa kuona mwenyewe!
Inategemea na aina ya udongo kwanza katika kichanga weka mbolea na miziz inapata urahisi wa kupenya
 
Tuna shida kubwa sana ya wataalamu wa KILIMO ili kupata utaalamu wao kuhusu aina ya udongo na matumizi yake

Mara nyingi sana mazao yanakua treated tofauti kulingana na aina ya udongo

Kuna aina ya udongo ukiweka mbolea ya aina fulani shina la karanga linakua kubwa sana limemea vizuri na linaweka karanga nyingi chini tena kubwa kweli LAKINI ukiimenya karanga unakuta kakaranga kadogo kamesinyaa

Niliwahi kulima mahindi ya DK Singida sikupata vizuri kama nilivyokuja kulima tumbili

Nadhani serikali kupitia wataalamu wa kilimo wangefanya utafiti wa aridhi yote tanzania na kutupa muongozo wa kila aridhi inafaa mbegu gani na mbolea gani

Kenye wamejitahidi sana katika hili
 
Back
Top Bottom