Mkuu Tafadhari sana mimi nililima kwenye shamba lilikuwa limewekewa mbolea ya samadi kwa wingi sana na akalima mara1 nami masika yaliyofuata nikalima karanga.Ni kwamba karanga zilikubali mno zilinawili hakuna mfano na zilizaa watoto wengi sana tena wakubwa cha ajabu ni kwamba kile cha ndani(karanga yenyewe) ni kadogo mno na kanakuwa na mwonekano wa kunyauka. Ndipo nilipoambiwa karanga na viazi havihitaji mbolea sana.
Kwa upande wa Viazi majani yanaweza yakawa mengi sana juu lakini kiazi kwa ndani ukakosa ukaambulia mizizi minene ama unaweza kupata viazi oversize ukikipika kinakuwa na mji maji hakina unga na saa nyingine hakiivi
hasa.Hii ni kwa uzoefu wangu kwa kuona mwenyewe!