Matumizi ya Neno "Kuweza"

Matumizi ya Neno "Kuweza"

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Neno "kuweza" limekuwa linatumiwa vibaya sana kwenye kiswahili cha siku hizi. Luna mifano mingiya matumizi hayo haramu kwa mfano kwenye sentensi hii ina makosa:

"Mchezaji wa zamani wa timu A ambaye aliweza kufukuzwa kwenye timu hiyo, sasa hivi kajiunga na timu B."

Naomba thread hii ikusanye matumizi yote haramu ya neno kuwez, nitayaweka pamoja na kiuyapeleka BAKITA kwa ufumbuzi
 
Duu wengi hawajaenda darasani kujifunza kujenga sentensi pia kwenye jamii zetu kuna watu wenye uelewa tofauti lakini ni Bora tuanze na waliomo humu
 
Umetumia wewe au sehemu/watu tofauti na wewe wametumia?
Nimesikia matumizi hayo kwenye vyombo vingi vya habari mitandani. Linatumiwa mahali lisipohijiwa kabisa. Wengine wanasema ".... Timu A ambayo iliweza kufungwa na timu B kwenye mchuano wa jana, leo hii itasafiri kwenda kupambana na timu C."
 
kuweza kupangiwa matumizi ya lugha nlozaliwa nayo.
 
kwanza wewe unajiitaje kichuguu,,matumizi mabaya ya neno kichuguu,,ngoja waje siafu na mchwa waanzishe thread yao humu.
 
Kama unaandika thesis ndio utapata shida ila kitaa bora ueleweke tena mara nyingine madogo (anti-administration) wanaharibu kimakusudi kabisa....

Ushanifahamu ?
 
Back
Top Bottom