SoC04 Matumizi ya nishati safi kwa matumizi ya kupikia na viwandani kwa maendeleo ya Tanzania

SoC04 Matumizi ya nishati safi kwa matumizi ya kupikia na viwandani kwa maendeleo ya Tanzania

Tanzania Tuitakayo competition threads

Perfomance47

New Member
Joined
May 20, 2024
Posts
2
Reaction score
0
Nishati ni ule uwezo au nguvu ya kufanya kazi inayoleta matokeo Fulani ambayo yanaweza kuwa chanya au hasi, nishati imegawanyika katika makundi makuu mawili ambayo ni nishati safi na nishati chafu. Nishati isiyo safi ni aina ya nishati ambayo husababisha madhara ya kimazingira mara baada ya kutumika ikiwemo matumizi ya kuni na mkaa ambayo hupelekea mabadiliko hasi ya tabia ya nchi, lakini nishati safi ni aina ya nishati ambayo ni salama na Rafiki katika mazingira yetu mara baada ya kutumika mfano nishati ya jua, nishati ya maji na nishati ya upepo.

Matumizi ya nishati safi ni muhimu katika mazingira yetu yanayotuzunguka kwa muonekano nadhifu, maendeleo ya kiuchumi na pia kujiepusha na magonjwa yasiyo ya lazima, lakini endapo tutakuwa tunatumia nishati chafu kwa wingi ikiwemo matumizi ya mkaa na kuni itatupelekea madhara lukuki yakiwemo ukame na njaa, magonjwa yakiwemo saratani na kifua kikuu(TB), ongezeko la joto na pia ongezeko la matukio yanayohusiana na unyanyasaji wa kijinsia na Watoto.

Kupitia hatua zinazochukuliwa na serikali juu ya utunzaji wa mazingira, mnamo mwaka 1986 baraza la ufuatiliaji wa mazingira salama liliundwa rasmi lililoitwa baraza la taifa la uhifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC) lililo anzishwa kwa sheria ya usimamizi wa mazingira namba 19 Ya mwaka 1983, hivyo baraza hilo lilikuwa likisimamia na kuratibu utekerezaji wa sera na sheria ya mazingira na kuimarisha msingi mzuri wa usimamizi hadi hivi leo.

Kutokana na mkakati wa matumizi ya nishati safi maeneo ya mijini na vijijini kupitia jitihada zinazofanywa na raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan, alieleza mkakati wa taifa unaohusisha matumizi ya nishati safi ya kupikia katika siku ya uzinduzi wa nishati safi uliofanyika tarehe 8/05/2024 kwa lengo la kuhakikisha kuwa asilimia 80 ya watanzania watakuwa wakitumia nishati hiyo ifikapo mwaka 2033.

Hata hivyo, pamoja na jitihada zote zinazofanywa na serikali ili kutokomeza matumizi ya nishati chafu zinazoleta athali nyingi katika mazingira, matumizi ya nishati chafu mfano matumizi ya mkaa na kuni katika mahitaji ya kupikia na pia matumizi ya Mafuta ya petroli na dizeli katika vyombo mbalimbali vya usafiri kama vile magari, pikipiki na bajaji yanayochangia uchafuzi wa tabaka la ozone, ikiwa utumiaji wa nishati hizi umekithiri kwa kasi hususani maeneo ya vijijini.

Takwimu zinaonyesha kuwa Zaidi ya asilimia 90 ya kaya za Tanzania hutegemea nishati chafu ambayo inatokana na kuni, mkaa pamoja na mabaki ya kinyesi cha Wanyama kwaajili ya shughuli za kupikia na shughuli nyingine za majumbani, hali ambayo wataalamu wanaonya kwamba imekuwa sehemu ya ongezeko la matatizo ya kiafya kwa watu wengi hususani vijijini na pia uharibifu wa mazingira ukivunja rekodi.

Screenshot_20240529-204559_1.jpg

UVUNAJI WA NISHATI CHAFU YA MKAA…Chanzo: picha na Nukta habari​

Ripoti zinaeleza kwamba kila mwaka nchini Tanzania watu 33,000 hupoteza Maisha kutokana na Mikasa inayosababishwa na matumizi ya nishati isiyo salama na kiwango hicho kimekithiri sana maeneo ya vijijini ambako upatikanaji wa nishati safi bado ni shida.

Tanzania yetu inayotakiwa ndani ya miaka 10 ijayo yaani kuanzia 2024-3034 ni Tanzania tunayohitaji mabadiliko makubwa ya utumiajiwa nishati safi katika shughuli mbalimbali mijini na vijijini, mabadiliko hasi ya tabia ya nchi kama vile ukame na ongezeko la magonjwa yanaweza kutatuliwa endapo njia zifuatazo zitafuatwa;

Kuwekwa kipaumbele juu ya bajeti ya uwezeshaji wa kiuchumi na ufikiwaji wa nishati safi maeneo ya vijijini; maeneo ya vijijini ni miongoni mwa maeneo yaliyoathiliwa na matumizi ya mkaa na kuni kutokana na hali duni ya kimaisha miongoni mwa kaya nyingi vijijini, hivyo serikali inatakiwa kutenga bajeti ya fedha kwa dhumuni la kusaidia kaya zisizojiweza kabisa kiuchumi ili kuacha kabisa matumizi ya nishati chafu.

Kubadilisha mifumo ya teknolojia chafuzi inayochangia uharibifu wa tabaka la ozoni kwa kiwango kikubwa; ujio wa teknolojia inayohusisha matumizi ya vilainishi katika vyombo mbalimbali vya moto mfano Mafuta ya dizeli na petroli vimepelekea uzalishaji mkubwa wa gesi ya kabondayoksaidi inayopelekea uharibifu wa tabaka la ozoni,

Screenshot_20240529-204609_1.jpg

UCHAFUZI WA TABAKA LA OZONI…Chanzo: picha na UN news​

hivyo teknolojia hii inatakiwa kubadilishwa na kuanza upya kutumia nishati safi kama vile nishati ya jua na maji ili kunusuru uharibifu wa mazingia nchiniTanzania. Pia inatakiwa kuhamasishwa Zaidi katika maeneo ambayo yameanza kutumia kwa asilimia chache mfano shirika la (UNDP) lilianzisha vituo vya kuchaji magari na bajaji zinazo tumia umeme Dodoma may 12, 2023.

Screenshot_20240529-204615_1.jpg

UZINDUZI WA MAGARI YA UMEME… Chanzo: picha na michuzi blog

Serikali inatakiwa kusimamia uhuru wa vyombo vya habari kuripoti na kuhamasisha utoaji wa maudhui yanayohusiana na matumizi ya nishati safi nchini; uwepo wa uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania utasaidia waandishi wa habari kuweka juhudi katika ukusanyaji wa taarifa za kimazingira, siku hizi waandishi wengi wa habari wanaziepuka habari za kimazingira kutokana na sababu za waandishi kukamatwa, kunyanyaswa na kuuwawa mfano kutokana na ripoti ya Anold Kayanda wa idhaa ya Kiswahili alieleza adha ya vifo vya waandishi wa habari 44 waliouwawa wakifuatilia habari za kimazingira (2013-2023 ).

Elimu inatakiwa kutolewa hususani maeneo ya vijijini inayohusiana na madhara ya kutumia nishati chafu; watu wanaoishi maeneo mbalimbali ya vijijini nchini Tanzania hawana elimu ya kutosha juu ya nishati safi mfano matumizi ya gesi, hivyo wananchi wapewe elimu kwa namna ambayo itawasaidia kujua hasara za kuni na mkaa na kuwaelekeza nama tunavyoweza kutumia gesi kwa kurahisisha shughuli mbalimbali.

Elimu ya matumizi ya nishati safi itumike kwenye mtaala wa elimu ya vitendo mfano mafundisho juu ya matumizi ya gesi na nishati inayowezakupatikana kupitia mwanga wa jua.

Serikali inatakiwa kuanzisha sera mbalimbali zinazohusu matumizi nishati safi ili kuhamasisha wananchi wa Tanzania kutumia nishati safi; kanzisha sera mbalimbali kupunguza adha ya utumiaji wa kuni na mkaa kwa kuanza kutumia gesi kama nishati safi mfano, moja ya kauli mbiu ya raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan alisema ‘’ taasisi zote zinazohudumia watu Zaidi ya 100, marufuku kutumia kuni au mkaa’’

Hivyo basi, matumizi ya nishati safi katika jamii zetu siyo njia pekee ya kutunza na kulinda mazingira yetu, pia kuna namna mbalimbali ambazo watanzania tunatakiwa kufanya ili kujitengenezea maendeleo endelevu
Njia hizo ni kama kuepuka uvuvi haramu na kuhjihusisha na shughuli za kilimo karibu na vyanzo vya maji.
 
Upvote 2
Hata hivyo, pamoja na jitihada zote zinazofanywa na serikali ili kutokomeza matumizi ya nishati chafu zinazoleta athali nyingi katika mazingira, matumizi ya nishati chafu mfano matumizi ya mkaa na kuni katika mahitaji ya kupikia na pia matumizi ya Mafuta ya petroli na dizeli katika vyombo mbalimbali vya usafiri kama vile magari, pikipiki na bajaji yanayochangia uchafuzi wa tabaka la ozone, ikiwa utumiaji wa nishati hizi umekithiri kwa kasi hususani maeneo ya vijijini.
Ni kwa kiasi fulani tunachafua mazingira ndiyo. Lakini hata hivyo usiogope? Bado kwa kiwango chetu cha tani 0.1 ni kidogo kulinganisha na nchi zilizoendelea unakuta nchi inatema tani milioni alfu mbili alfu tano za hewa chafu

Elimu ya matumizi ya nishati safi itumike kwenye mtaala wa elimu ya vitendo mfano mafundisho juu ya matumizi ya gesi na nishati inayowezakupatikana kupitia mwanga wa jua.
Jambo zuri hili, panapowezekana patumike nishati safi safi.

‘’ taasisi zote zinazohudumia watu Zaidi ya 100, marufuku kutumia kuni au mkaa’’
MAtokeo yake kwa ground mambo ni tofauti. Watu wanatumia mkaa na gesi wakiwa wachache. Lakini ikitokea dharula labda msiba au sherehe hapo kuni zinahusika.

Sijui tufanyeje hadi tufikie hatua mtu mwenye harusi badala aseme "Nina sherehe mbele niandae kuni za kutosha" aseme hivi; "nina sherehe kubwa mbele, niandae gesi mitungi yote iwe fullu🤯😎😅😅😅"
 
Back
Top Bottom